YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Sunday 2 September 2012

MAGAZETI YA LEO TAREHE 3, September 2012



Posted: 3rd September 2012 by MillardAyo in News
0
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

YALIYOTOKEA IRINGA NA KIFO CHA MWANDISHI WA HABARI, PICHA NYINGI ZAIDI HA JINSI MWANDISHI HUYO ALIVOFARIKI


                                    Mwili wa mwanahabari Daud Mwangosi ukiwa chini


Hapa polisi wakiwataka wafuasi wa Chadema kutawanyika eneo la tukio ofisi za Chadema Nyololo Mufindi

                                     Mwili wa mwanahabari Daud Mwangosi ukiwa chini


                      Daud Mwangosi kulia enzi za uhai dakika 20 kabla ya kuuwawa kwake
Mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chama chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za Polisui i na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo

Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi .

Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa hawapo tayari kuondoka katika ofisi yao.

Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuawa kilitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini .

Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti .

Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.

Hii ni taarifa ya Jeshi la polisi kabla ya tukio kwa vyombo vya habari 

JESHI la polisi mkoa wa Iringa limesema limezuia mikutano ya vyama vya siasa kwa vyama vyote na sio kwa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) pekee hivyo laonya vyama vyote kutii sheria bila shuruti.

Hata hivyo jeshi hilo la Polisi limesema kuwa halifanyi kazi kwa matakwa ya chama chochote cha siasa na kuwa si kweli kama wanavyodai viongozi wa Chadema kuwa jeshi la polisi linatumiwa na chama cha mapinduzi (CCM) kuzuia mikutano hiyo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuanda ametoa kauli hiyo leo ofisini kwake alipozungumza na waandisha wa habari kuhusu zuio la mkutano wa Chadema uliopangwa kuanza leo katika wilaya ya Mufindi.

" Nawatangazia wanasiasa na vyama vyote vya siasa pamoja na wananchi wa mkoa wa Iringa kuwa hakutakuwa na mikutano ya kisiasa kutokana na shughuli za sensa zinazoendelea ....hivyo basi nawaomba wananchi wote kutoshiriki mikutano yoyote ya kisiasa itakayoitishwa na wanasiasa "alisisitiza

Kuwa mikutano hiyo imezuiliwa kwa kipindi hiki cha sensa kilichoongezwa hadi hapo tamko litakapotolewa tena na msajili wa vyama vya siasa John Tendwa kama alivyokwisha kutoa tamko la kuzuia shughuli hizo za vyama vya siasa kwa kipindi hiki cha sensa.

"Wananchi wote wa mkoa wa Iringa mnaombwa kutii sheria bila shuruti hii ni amri ....nawaombeni sana wananchi kutodanganywa na wanasiasa kwa kuvunja sheria "aliongeza kamanda huyo wa polisi.

Hata hivyo alisema kuwa kimsingi zoezi la sensa lilipaswa kuhitimishwa Septemba mosi mwaka huu ila kutokana na serikali kuongeza muda wa zoezi hilo bado jeshi hilo la polisi linazingatia maagizo ya Msajili wa vyama vya siasa kama alivyoyatoa kwa jeshi hilo.

Kamanda Kamuanda alisema kuwa jeshi hilo la polisi wala msajili wa vyama vya siasa hajazuia vyama vya siasa kuendelea na vikao vyao vya ndani kwa kipindi hiki na kuwa hata Chadema wakiwa mkoani Iringa wameendelea kufanya vikao vyao vya ndani katika kata mbali mbali za mkoa wa Iringa na hakuna mtu aliyewazuia kuendelea kufanya hivyo.

Majibu ya Dkt Slaa
Wakati jeshi la polisi likipinga shughuli hizo za vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara katibu mkuu wa Chadema Taifa Dkt Willbroad Slaa ameibuka na kusema kuwa chama chake kitaendelea na mikutano kama kilivyojipangia na kuwa wapo tayari kwa lolote litakalojitokeza .

Dkt Slaa alisema kuwa walivumilia mara ya kwanza walipozuiwa mikutano hiyo mkoani Iringa na kuvuta subira hadi jumamosi zoezi hilo lilipomalizika sasa anashangazwa kuona jeshi hilo likiendelea kuzuia mikutano hiyo tena.

"Tumemsikiliza kamishina wa sensa Hajati Amina Mrisho Said kuwa hadi sasa watu asilimia 95 wameandikishwa huku akiwata wale ambao bado kuwapigia simu wenyeviti wa mitaaa na vijiji ili wakaandikishwe na makarani wa sensa ....sasa jeshi la polisi linataka kutuambia kuwa hao watu asilimia 5 waliobaki wapo Iringa peke yake hadi wakazuia mikutano yetu? tunasema hatutakubali tutaendelea na mikutano yetu kama kawaida hatupotayari kabisa kusubiri hadi tarehe nane" alisema Dkt Slaa.

Pia alisema kuwa kama ni uzalendo sasa umefika kikomo na kuwa wataendelea na ratiba zao za mikutano kama ilivyopangwa na watapambana kwa lolote .

VIDEO YA MKUTANO WA CHADEMA READING

Mkutano wa Chadema wa Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) uliofanyika Reading Agosti 26,

UTAMBULISHO WA KALALA WAFANA MZALENDO PUB



   Kalala Junior (katikati) baada ya kutambulishwa rasmi. Kusoto ni mwimbaji wa bendi hiyo, Janeth Isinika na kulia ni Haji.…

ROSE LUCAS ATWAA TAJI LA REDD'S MISS KANDA YA MASHARIKI 2012



Mshindi wa Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2012, Rose Lucas ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwa katika pozi baada ya kutwaa taji hilo usiku wa kuamkia leo.…

MASHINDANO YA MBUZI YA HISANI DAR ES SALAAM 2012 YATIMUA VUMBI JIJINI DAR



Meneja Biashara wa Shirika la Ndege la Uingereza  (BA) nchini, Saada Juma (kulia) akikabidhi tiketi ya kwenda na kurudi London Uingereza kwa, Emma Leclercq, aliyeibuka mshindi wa bahati nasibu katika mashindano ya  Mbuzi ya Hisani Dar es Salaam 2012, katika viwanja vya The Green, Barabara…

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA USIKU HUU NDANI YA UWANJA WA CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA



Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti…

PRODUCER NA RAFIKI WA MR EBBO ANAETAKA KUACHIWA STUDIO YA MR EBBO.




2
Producer Jeff.
Ni zaidi ya miezi nane imepita sasa hivi toka kufariki kwa msanii Mr Ebbo ambae alifariki usiku wa kuamkia mwaka 2012 kutokana na kuugua kansa.
Jeff ambae alikua rafiki wa Ebbo kwa karibu miaka 20 pia akiwa ni Producer wake wa video kadhaa, siku chache baada ya kifo cha Ebbo ndio alikua akabidhiwe na familia ya Ebbo kuiendesha studio ya Motika iliyokua ikimilikiwa na Ebbo lakini baadae familia ikabadili huo mpango.
Baada ya hayo mabadiliko iliamuliwa kwamba studio hiyo iliyokua na makazi Tanga, sasa itahamishiwa Arusha na itasimamiwa na watu wengine.
Producer Jeff ameongea exclusive na millardayo.com na kueleza masikitiko yake kuhusu hiyo studio kutokufanya kazi mpaka sasa hivi huku bado akiwa na nia ya kuiendesha.
Hii ndio nyumba iliyokua inamilikiwa na marehemu Mr Ebbo Tanga ambapo studio iko hapohapo.
Jeff amesema hataki kulipwa wala kuchukua pesa yoyote kutokana na hiyo studio, anachotaka yeye ni kuisaidia familia ya Ebbo ambayo imebaki, wakiwemo watoto.
Namkariri akisema “kwa sasa studio imehamishiwa Arusha lakini vifaa vyote vimefungiwa stoo, mke wake Ebbo alikuja kuchukua vitu Tanga lakini hakuna kinachoendelea hata ndugu yake Ebbo aitwae Maukweli nimeongea nae anasema yule mwanamke haeleweki”
“Baba mzazi wa Mr Ebbo ndio alinikabidhi funguo za studio niisimamie kwa sababu yeye hana idea na hii kazi, nilipanga kumleta producer mkali kutoka Dar es salaam ili afanye kazi tuifufue studio… ila mpaka sasa pia niko tayari hata kama wakiamua kuileta tena kwangu, pale ambapo alikua akiishi Mr Ebbo sasa hivi pamepangwa anaishi mtu mwingine na hata chumba cha studio kimevunjwa na analala mtu sasa hivi”

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA PREMIER LEAGUE, PRIMERA DIVISION NA BUNDESLIGA SEPT 2 2012 NDIO HAYA.




0

MWILI WA ALIYEKUA WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA MELES ZENAWI UNAAGWA..




0
.
.
.
.
.
Hawa ni baadhi ya waliohudhuria akiwemo Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania na Paul Kagame wa Rwanda.
.
Rais Paul Kagame akisain kitabu cha maombolezo.
.
.