YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday 4 September 2012

BLOGGER MYSELF NIKIWA NA WADAU DULLAH NASSORO PAMOJA NA AMBER LABANI DURING THE HOLIDAY...

Afrika Msiba Ni Wa Wote; Dr Na Profesa Wamekutana Msibani

Dr. Wilbroad Slaa na Profesa Mark Mwandosya.  Kwenye msiba wa mwandishi Daud Mwangosi. Picha na Said Ng'amilo wa Mjengwablog.

Tafakuri Ya Usiku; Je, Uwezo Wetu Wa Kufikiri Umepungua?

Ndugu zangu,

Yanayotokea nchini mwetu yanatutaka sio tu tufikiri, bali, tufikiri kwa bidii. Lakini swali ni hili; Je, uwezo wetu wa kufikiri umepungua?
 
Yumkini si kwa aliyekuwa na 

ujasiri wa kuipiga picha hiyo hapo juu. Alifikiri sana pia. Na si kwa aliyekaa chumba cha habari na kuumiza kichwa, kisha akaamua picha hiyo ipambe sura ya mbele ya gazeti la Mwananchi la juzi. Hapa Iringa gazeti hilo liligombaniwa kama njugu, na bila shaka sehemu nyingine za nchi. 

Naam, siku hizi utasikia ikisemwa; " Tumefika pabaya!" Mwingine atasema; " Tunakokwenda ni kubaya!". Lakini, ni Watanzania wangapi wenye kuuliza maswali haya; " Tumefikaje hapa?" Na " Je, tunaendaje?" Maswali hayo yanamtaka mwanadamu afikiri kwa bidii. 

Wakati mwingine nafikiri, kuwa Watanzania tumechoka kufikiri. Hata kwenye maswali magumu yenye kutuhusu tunataka wengine wafikiri kwa niaba yetu. Unaweza kukutana na Mtanzania mwenzako ukamwuliza; " E bwana ee, unafikiri nini juu ya jambo hili?". Jibu lake; " Kwani wewe unaonaje?"- Ni moja ya maswali yenye kuashiria anaykujibu swali lako amechoka kufikiri.
 
Na wakati mwingine tatizo si kutofautiana kifikra, bali kutofautiana namna au jinsi ya kufikiri. Swali moja, lakini unaweza kuona namna tunavyotofautiana katika kuchagua njia ya kulisogelea ( approach) swali husika. 

Na kuna wenye kukimbilia kutafuta njia za mkato. Ndio, majawabu ya mkato. Na baadaye itakuwaje? Inshallah na BwanaYesu Asifiwe!
 
Wanahabari Iringa Wanusurika Kifo Wakitoka Kumzika Mwenyekiti Wao Dudi Mwangosi

Wanahabari hao wakijiokoa kwa kutokea mlango wa dereva baada ya gari yao kutaka kupinduka huko Tukuyu Mbeya wakitoka kumzika mwenyekiti wo Daudi Mwangosi kijiji cha Busoka Tukuyu

KILICHOMUUA DAVID MWANGOSI HIKI HAPA!!!

MAREHEMU DAVID MWANGOSI AMEUWAWA KWA BOMU LA MACHOZI

BARAZA la Habari Tanzania (MCT), limearifiwa kuwa Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten mkoani Iringa, Daudi Mwangosi ameuawa kwa bomu la machozi.

Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga alisema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wahariri pamoja na mameneja wa vyombo vya habari yaliyoanza mkoani Morogoro jana.

Mukajanga alisema baada ya kupata taarifa za awali za kifo cha Mwangosi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa ( IPC), alilazimika kumtafuta kwa njia ya simu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi.

Alisema katika mazungumzo yao, Dk Nchimbi alimfahamisha kuwa yupo nje ya nchi, Afrika Kusini kikazi na kukiri kupata taarifa za kifo hicho.

Mukajanga alinukuu mazungumzo yake na Waziri huyo kwa kusema; “Nimepata taarifa za kifo hicho na taarifa za awali zimesema ni bomu la machozi halikulipuka kitaalamu na limemuua (Mwangosi) na kuwajeruhi watu wengine wa tatu.” 

Alisema Dk Nchimbi alitoa rambirambi kwa waandishi wote wa habari nchini kutokana na kifo cha mwandishi mwenzao.

Kauli zakinzana “Hapa tunaona kauli ya Waziri inapishana na Polisi ambao wanadai amekufa kwa kupigwa na kitu kilichorushwa, wakati Waziri anadai ni bomu la machozi ambalo halikulipuka kitaalamu na kusababisha kifo na majeruhi watatu,” alisema Mukajanga.

Alisema MCT imefedheheshwa kwa kuwa mwandishi aliyeuawa, alikuwa kazini akitekeleza wajibu wake wa kukusanya habari.

Mbali ya kufedheheshwa huko, Mukajanga alisema mauaji hayo yametoa picha mbaya kwa Tanzania wakati huu ambao wajumbe wa Umoja wa Mabaraza ya Habari Duniani wapo nchini kwa ajili ya mkutano ambao Tanzania ni mwenyeji.

“Mimi ni Makamu wa Rais wa Mabaraza ya Habari Duniani, nimefedheheka sana kwa tukio hili, limefanyika wakati wajumbe kutoka nchi mbalimbali duniani wa mabaraza ya habari wapo hapa nchini kuhudhuria mkutano… wanakutana na vichwa vya habari kwenye magazeti na televisheni kuhusu kuuawa kwa mwandishi wa habari akiwa kazini,” alisema Mukajanga.

MCT imewataka waandishi wa habari kuchukua tahadhari ikiwemo kulindwa na Serikali wanapokuwa kazini. Alisema mauaji hayo yameandika historia mbaya na ya kwanza tangu kupata Uhuru.

“Kwa mara ya kwanza tangu Uhuru mwandishi wa habari anauawa akiwa kazini kutekeleza wajibu wake ... tukio hili limetoa sura kwamba waandishi wa habari wanatakiwa kupatiwa mafunzo ya kuchukua tahadhari kwenye matukio ya hatari,“ alisema Mukajanga. HABARI NA TSN

USAILI WA MAISHA PLUS 2012 WAENDELEA

Heka heka za Maisha Plus.
 ---
Usaili wa Maisha Plus umeendelea leo (Septemba 4) mkoani Mwanza; baada ya hapa timu nzima itaelekea Morogoro katika wilaya ya Mvomero na siku inayofuata itaibukia Igula, Mkoani Iringa.

"Tukitoka Iringa tunahamia Sumbawanga huko Kantalamba then tutarudi Mbeya, baadaye tutaelekea Kilwa kisha Masasi na Zanzibar itafuatia.

Kaka Bonda akimhoji mshiriki.
---
Dar es Salaam itakuwa ya mwisho ambayo usaili wake utafanyika Septemba 22 na 23," anasema Masoud Kipanya.

Fomu za kushiriki shindano hili kwa Dar es Salaam zinapatikana katika Duka la KP lililopo Millenium Towers Kijitonyama. Kama unahitaji fomu piga namba 0717104303 uelekezwe.
 Mama Shujaa wa Chakula akionyesha ushujaa wa chakula.

HIZI NDIO HABARI KUBWA ZA MAGAZETI YA LEO SEPT 5, UDAKU, MICHEZO NA HARDNEWS.

0
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

HIZI NDIO HABARI KUBWA ZA MAGAZETI YA LEO SEPT 5, UDAKU, MICHEZO NA HARDNEWS.

0
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.