YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Friday 7 September 2012

PATA KUONA VIDEO YA MUSIC VIDEO STAR WA BONGO.




MBWIGA NA SHAFFIH WASHINDWA KUTAMBIANA MJINI TABORA.



Mchezo maalum wa kuzipatanisha timu za Rhino Rangers na Police za hapa mjini Tabora umemalizika kwa timu hizo kufungana bao 1:1.
Mchezo huo ulioandaliwa na kampuni ya Clouds Media Group ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za tamasha la Fiesta linalotarajiwa kufanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora.
lengo la kuzikutanisha timu hizo lilikua ni kuondoa uhasama uliokuwepo hapo awali baina ya timu hizo mbili uliokuwa umedumu kwa muda sasa,watangazaji wa vipindi vya michezo vya Clouds Media Group bwana Shaffih Dauda (Polisi ) na Mbwiga Mbwiguke (Rhino Rangers ) walizichezea timu hizo ikiwa ni sehemu ya kuonyesha kwamba upinzani kwenye mchezo wa soka huwa ni uwanjani na mara baada ya hapo maisha mengine huendelea kama kawaida.
Lengo lingine la mchezo huu lilikua pia kuzichangia timu hizi pesa kwa ajili ya maandalizi ya ligi daraja la kwanza inayotaraji kuanza siku chache zijazo,o.
mapato ya mchezo huo yalikuwa ni Tsh 1,2170,000 kutokana na kiingilio cha tsh 1,000 kwa wakubwa na 500 kwa watoto.

    Dauda na Mbwiga wakisalimiana kabla ya mchezo.

   Hapa huyu jamaa alijipendekeza nikampiga kikoi kwa kutumia guu langu la dhahabu kama unavyoona hapo.
    Mbwiga kama anapigaaaaaaaaaa, anafinyaaaaaaaaaaaa
    sehemu ya mashabiki waliohudhulia mpambano huo.


   Bonge nae alikuepo kushow luv na wadau wake.
    Mgeni wa heshima akiikagua Rhino Rangers




 Hapa nilikua nawaeleza wachezaji wa timu zote mbili dhumuni hasa la mchezo huu!
 Kikosi cha Shaffih (POLICE TABORA )

Wednesday 5 September 2012

STORI 20 ZA FACEBOOK NA TWITTER, ALICHOANDIKA KIGWANGALLA KUHUSU VITISHO VYA BASTOLA NA BASHE, NIKKI MBISHI ALIVYOICHANA YMCMB NA STORI NYINGINE.




0
.
MBUNGE WA NZEGA KUPITIA CCM.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

PICHA ZA MADAME RITA PAULSEN NA PASCHAL KASSIAN MANZESE DAR ES SALAAM




0
.
.
.
.
.
.
Kassian na dancers wake.
.
.
.

TAHADHARI YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA KUHUSU MVUA ZA EL NINO NDIO HII.




0
Madhara ya mvua mabondeni.
Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania imetoa tahadhari ya uwepo wa mvua kubwa zinazofahamika kama El nino katika kipindi cha kuanzia wiki ya nne ya mwezi September hadi kufikia December 2012 katika maeneo mbalimbali Tanzania.
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Dr. Agnes Kijazi amesema hizo mvua zinatarajiwa kusababishwa na mgandamizo mkubwa wa mfumo wa hewa kutoka katika misitu iliyo katika ukanda wa bahari ya hindi, tahadhari iwafikie wote wakiwemo wakulima na wanaoishi kwenye maeneo ya mabonde.

HUYU NDIO MWANDISHI ALIEJISALIMISHA POLISI MWENYEWE KATI YA WALE WATATU WALIOTANGAZWA KUSAKWA BAADA YA KIFO CHA MWANGOSI.




1
Kwa sababu za kiusalama ilikua picha yake isiwekwe hapa lakini yeye mwenyewe ameidhinisha iwekwe kwa sababu haogopi, Francis Godwin ni huyo mwenye nguo nyeusi.
Siku mbili baada ya kifo cha mwandishi mwenzao wa habari (Daudi Mwangosi) aliefariki kutokana na kulipukiwa na bomu akiwa mikononi mwa polisi waliokuwa wanatawanya wafuasi wa Chadema huko Iringa, mwandishi wa habari Francis Godwin ambae alikua rafiki wa marehemu amejisalimisha polisi kufata masharti ya taarifa iliyotolewa kwa yeye na wenzake wawili kusakwa na polisi.
Exclusive na millardayo.com namkariri Godwin akisema “kutokana na hali halisi ya kushuhudia tukio la mauaji ya Mwangosi, nilifukuziwa kwa nyuma na gari lisilokua na namba pia nilipofika nyumbani niliambiwa kuna watu walikuja kuniulizia lakini hawafahamiki, na taarifa zikatoka kwamba tunasakwa”
Kuhusu kujisalimisha, Godwin amesema aliamua kufanya huo uamuzi baada ya kusikia taarifa za kusakwa kwake pamoja na waandishi wengine wawili, jana (september 5) aliamua kujisalimisha mwenyewe Polisi akiwa amesindikizwa na waandishi wa habari kama hamsini ambapo baada ya kufika pale walikutana na  kamishna wa makosa ya jinai Tanzania Robert Manumba ambae ilibidi ahoji polisi Iringa kama ni kweli wanamtafuta Godwin na wenzake.
.
Namkariri Godwin akisema “baada ya kumuuliza mmoja kati ya maofisa wake kama ni kweli wanamtafuta Godwin ofisa huyo alijiumauma na baadae akasema hatumtafuti, baada ya hapo waandishi wa habari tulisimama tukaondoka kwa sababu ya kutokubaliana na kilichotaka kuendelea kuhusu taarifa ya uchunguzi ya Manumba”
Kingine kilichoendelea baada ya hapo ni Club ya waandishi wa habari Iringa kuziomba redio mbalimbali za iringa ambazo zimekua zikirusha matangazo ya polisi jamii kusimamisha matangazo hayo ambapo wamiliki wa vyombo hivyo wamekubali ombi.
Francis Godwin ambae alikua karibu na marehemu Daudi Mwangosi muda mfupi kabla ya kuuwawa kwa bomu amesema “Nilijua kwamba mimi ni miongoni mwa waandishi watatu wanaotafutwa kwa sababu marehemu kabla ya kifo akiwa amekamatwa nilitaka kwenda kumuokoa pale lakini nilipokua namsogelea Daudi akaniambia Godwin mdogo wangu kimbia… wakati nakimbia kama hatua 20 mbele nyuma nageuka nasikia mlipuko mkubwa, kuangalia ni Wangosi amekufa na nilibahatika kupiga baadhi ya picha ambapo askari waliokuwepo walipoona narudi kwenye eneo hilo walinionyeshea bunduki ikabidi ninyooshe mikono juu kwamba jamani mimi nakuja kwa heri wakaniambia potea”
Muda mfupi baada ya Marehemu Daudi kulipukiwa na bomu.
Godwin amesema baada ya kugeuka na kuanza kukimbia walianza kumfukuzia ila bahati nzuri gari yake ilikua mbali, baada ya kutishwa na polisi walipokwenda hospitali ulipopelekwa mwili wa marehemu ilibidi waanze kutoa mabango ya wanahabari yaliyobandikwa kwenye gari yao pamoja na kutoa namba za gari, alianza safari ya kuondoka lakini kuna gari zilikua zinamfukuzia kwa nyuma mpaka alipofika nje kidogo ya mji wa Iringa na kuingia mitaani ndio akafanikiwa kukimbia.
Kwenye sentensi ya mwisho Godwin anasema ameibiwa siri na askari mmoja ambae alimwambia kuhusu kutafutwa kwake yeye na waandishi wa habari awengine mbapo alimuonya kwamba msimamo na kauli aliokua ameutoa pamoja na ushahidi wa tukio la mauaji ndio vimefanya atafutwe.
Kwa maelezo marefu zaidi unaweza kumsikiliza Godwin hapo chini…..

YALIYOJIRI KATIKA MAGAZETI YA LEO TAREHE 6, September 2012




0
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.