YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Thursday 11 July 2013

KITUKO ALICHOKIFANYA ZAHA SIKU YA KWANZA YA SAFARI YAKE NA MANCHESTER UNITED


MCHEZAJI  mpya aliyesajiliwa na Manchester United kutoka Crystal Palace, Wilfred Zaha alijikuta akiwa kituko na kutia aibu pale alipotinga Uwanja wa ndege na mavazi ya” kibrazamen” wakati wenzake  walitakiwa kuvaa suti kama sare ya kuwatambulisha walipokuwa wakijiandaa kuondoka kwa ajili ya ziara yao ya kujiandaa na msimu unaokuja. 

Alipoulizwa kuhusu wapi alipoacha vazi hilo Zaha hakukumbuka na ndipo msaada wa kumsaidia kutoka kwa maofisa wa Manchester kuanza kushughulikiwa

Hali hiyo ilimfadhaisha mchezaji huyo na kutaka kupanda ndani ya gari lake kuondoka na ndipo akasaidiwa na maofisa wa klabu hiyo waliompatia vazi hilo na kulitinga kabla ya safari hiyo.

Ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya ziara na klabu hiyo toka asajiliwe zaha alijikuta kama mtu mwenye mwanzo mbaya lakini tatizo hilo liliisha mara baada ya kupewa suti nyingine alizozitinga na kupendeza.
ZAHA AKIINGIA UWANJA WA NDEGE NA BEGI LAKE AKIWA NA MAVAZI YASIYO RASMI KWA SAFARI.


WACHEZAJI WA MANCHESTER UNITED WAKIWA  WAMEVAA SUTI KUJIANDAA NA SAFARI
ZAHA AKIWA NA FURAHA MARA BAADA YA KUVAA VAZI LA SUTI LIOLILOWEZA KUMLIONGANISHA NA WENZAKE

CHECK HAPA TID ALIVYOJIACHIA UK, WAZUNGU WAMSHANGAA WAMGEUZA KIVUTIO:


1
T.I.D msanii wa long time kwenye game ya bongoflava tangu enzi za Zeze,Siamini hadi leo hii na Kiuno na bado anafanya vizuri. Wiki kadhaa zilizopita baada ya kumaliza msiba wa mshikaji wake Mangwea, T.I.D alisafiri kwenda England kufanya show ambako huko pia ndiyo alifanya interview inayozungumziwa sana hivi sasa kwenye mitandao. Chukua time kidogo kumcheki T.I.D akiwa kwenye mitaa ya huko UK.

2

3

4

5

6

WEMA NAE AANIKA NYETI ZAKE TENA.








Hii inaonyesha ni jinsi gani mkorogo ulivyomtafuna mmlimbwende Wema sepetu,akija kupata kansa ya ngozi utasikia ohhh nimerogwa mie kumbe mkorogo.

 

MAMA MZAZI WA PROFESA J AFARIKI DUNIA KWA KUGONGWA NA GARI DAR


Profesa J akiwa na mama yake mzazi Bi Rosemary Majanjara Haule enzi za uhai wake.  Picha hii ilipigwa April 4, 2008 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam  wakati wa sherehe ya uzinduzi wa albamu mpya ya Profesa J ya 'Aluta Continua'
Habari Zilizopokewa Usiku Huu Ni Kwamba Mama Yake Mzazi Msanii Maarufu Wa Muziki Nchini, Joseph Haule A.Ka. 'Profesa J' Amefariki Dunia Usiku Huu Baada Ya Kugongwa Na Gari  Maeneo Ya Mbezi Juu, Jijini Dar es Salaam, Alikokuwa Anaishi Na Mwanae.
Habari Zinasema Marehemu, Bi. Rosemary Majanjara Haule, Aligongwa Na Gari Akiwa Anavuka Barabara Kuelekea Dukani Kiasi Cha Saa Mbili Usiku, Na Kwamba Baada Ya Kugongwa Wasamaria Wema Walimkibiza Hospitalini Tumbi Kwa Kutumia Bajaji Ambako Alifariki Dunia. Taarifa Za Awali Hazijataja Aina Ya Gari Na Kama Baada Ya Ajali Hiyo Lilisimama Au La.
Profesa J Amethibitisha  Hilo Muda Mfupi Uliopita, Na Kusema Inamuia Vigumu Kuamini Imetokea Kwani Anasema Marehemu Mnamo Saa Mbili Hivi Alimpigia Simu Na Kumweleza Kuwa Amepata Ajali Na Kwamba Wakati Huo Yuko Kituo Cha Polisi, Bila Shaka Kupata Fomu Ya Pf 3 Ya Kumuwezesha Kwenda Kutibiwa Hospitali.

"Mama Aliniambia Mwanangu Nimegongwa Na Gari....Njoo Niko Polisi Naandikisha....Mwanangu Nakufa....Aliniambia Mama Na Mara Simu Ikakatika. Kila Nilipojaribu Kupiga Ikawa Haipatikani..." Alisema Profesa J Kwa Uchungu.

Anasema Wakati Anapigiwa Simu Na Mama Yake Yeye Alikuwa Katika Mgahawa Wa Nyumbani Lounge, Namanga, Dar es Salaam, Alikokuwa Katika Kikao Na Lady Jay Dee Na Mumewe Gadna G. Habash, Ambao Baada Ya Taarifa Hiyo Walimsindikiza Hadi Hospitali Ya Tumbi.

"Tulipofika Hospitali Sikuamini Kuona Badala Ya Kupelekwa Wodini Ambako Nilidhani Mama Atakuwa Amelazwa Nikapelekwa Chumba Cha Maiti Ambako Nilimkuta Mama Akiwa Marehemu", Alisema Profesa J Kwa Majonzi.

Global Publishers Inatoa Mkono Wa Pole Kwa Profesa J Kwa Msiba Huu Mzito Na Wa Kusikitisha. Tunamwomba Mola Ampe Nguvu Yeye Na Familia Yake Katika Wakati Huu Mgumu.

Tutaendelea Kuwapasha Kinachojiri Kadri Habari  Zaidi Zitapopatikana. Kwa Sasa Profesa J Na Wadau Wengine Wako Nyumbani Kwake Mbezi Juu.

HABARI MBAYA USIKU HUU: WASANII WATATU WA KIZAZI KIPYA WAFIWA NA MAMA ZAO:



525725_10151289889606495_368789305_n1
Habari ambazo sio nzuri lakini inakupasa kuzipata ni kwamba kiwanda cha bongoflava kipo kwenye majonzi baada ya wasanii watatu kupoteza mama zao katika kipindi cha siku mbili mfululizo.Salamu za rambirambi kutoka millardayo.com ziwafikie wasanii hawa ambao ni Prof Jay na mdogo wake Black Ryhno kwa kumpoteza mama yao pamoja na Z anto ambaye sources zinasema kwamba amempoteza mama yake kwa saratani ya ini. Roho za marehemu zilazwe mahali pema peponi amen.
971487_10151525841873517_471592447_n
Picture
Black Rhyno aliandika haya maneno kupitia ukurasa wake wa facebook

zanto_pointing

HAWA NI WANAFUNZI WA CHUO CHA.....WAKIFANYA MAPENZI LIVE.MZAZI ANAYELIPA MAMILIONI YA HELA SIJUI AKIONA HII VIDEO ATAJISIKIAJE!!


Kiukweli inauma sana kuona wazazi wanamlipia mtoto hela nyingi sana kumbe alichofuata ni Ngono tena anafanya hadharani tena kwa kujirekodi.
Credit:Skendo za mjini

Friday 5 July 2013

LOWASA AONGEA NA WAFANYA BIASHARA WA JIJIO LA MWANZA.

Hallow people...

WAZIRI MAGUFULI ATAMANI KUWA RAIS WA TANZANIA......ANADAI KWAMBA YUPO TAYARI KUGOMBEA MWAKA 2015 ENDAPO ATAKIDHI MASHARTI


 Katika hali inayoonyesha kuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, anautamani urais, amesema anaweza kutangaza nia hiyo kama atakidhi masharti yatakayowekwa kwenye Katiba mpya.
Alisema iwapo Katiba ijayo itakuja na sifa ambazo atakidhi vigezo kuna uwezekano mkubwa wa kuwania nafasi hiyo na kwamba iwapo atapungukiwa sifa zinazohitajika kwa mujibu wa Katiba hataingia kwenye kinyang’anyiro hicho.

Dk. Magufuli ambaye pia ni Mbunge wa Chato alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wazee wa wilaya hiyo kwenye ukumbi wa ‘Mshikamano Saccos’, muda mfupi baada ya mzee Paschal Nyambibo (87) kumsihi agombee nafasi hiyo mwaka 2015 kutokana na sifa zake za uchapakazi ndani ya serikali.

Nyambibo alisema kutokana na uwajibikaji mzuri aliouonyesha Dk. Magufuli tangu mwaka 2000 akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na katika wizara mbalimbali, Watanzania wamekuwa na imani kubwa na uwajibikaji wake na kwamba anastahili kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ifikapo mwaka 2015.

Licha ya kauli hiyo kusababisha minong’ono mingi kwa wazee waliohudhuria kikao hicho, Dk. Magufuli alionekana kutuliza hali hiyo kwa kusema isubiriwe Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano iwapo itakuwa na masharti ambayo yatamfanya kujitathimini iwapo ana sifa za kugombea au vinginevyo.

Hata hivyo, Dk. Magufuli hakusita kuonyesha hisia zake za kukerwa na baadhi ya wananchi wanaobeza maendeleo aliyotekeleza katika jimbo lake tangu alipochaguliwa kuwa Mbunge.


Alimshutumu hadharani aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Chato kabla ya kuhamishiwa wilayani Mbogwe, Gervas Stephano, kuwa hana shukrani.

Dk. Magufuli alimwelezea katibu huyo kuwa hana fadhila kutokana na mambo mengi aliyomtendea tangu akiwa katibu wa ofisi yake ya jimbo ambapo alimsaidia kupanda ngazi na kuwa Katibu wa CCM wilaya Chato, Kwimba, Kasulu, Kilosa na kurejea tena Chato kabla ya kuhamishiwa wilaya ya Mbogwe mkoani Geita  kuendelea na wadhifa huo.

“Tatizo lenu watu wa Chato hamna shukrani…mambo mengi nimefanya hapa Chato, lakini yote mnaona ziro…hata niliowasaidia kama Gervas naye sasa hivi ananiponda…lakini nawashukuru sana wazee wangu kwa kunikumbusha niliyoyafanya kwenye jimbo letu kupitia risala yenu nzuri,
” alisema Dk. Magufuli.

“Kutokana na hali hiyo ninawazawadia Sh. 1,000,000 mfanye sherehe ya kujipongeza kwa kuwa natambua mmejitesa sana mpaka kufanikisha kikao hiki cha leo…na kwa kuwa hamna mradi wowote wa kuwaingizia kipato kama wazee, ninaahidi kuwapa Sh.   3,000,000 kutoka mfuko wa jimbo, ili muanzishe walau saccos ya kukopeshana,” alisema.

Baadhi ya viongozi na wananchi wamekuwa wakilitaja mara kwa mara jina la Waziri Magufuli miongoni mwa watu wanaodhaniwa kutaka kugombea nafasi ya urais wa Tanzania mwaka 2015, ingawa mwenyewe amekuwa akikanusha uvumi huo.

Mbali na Dk. Magufuli, wengine ndani ya CCM wanaotajwa  ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa; Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye anajiita mtaji wa urais; Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe; Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Ushirikiano wa Kimataifa –CCM, Dk. Asha-Rose Migiro na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Mambo ya Nje, Bernard Membe, ambaye alipata kusema anasubiri kuiteshwa na Mungu kuwania nafasi hiyo.

"GEREZANI KUMENIFANYA NIMJUE MUNGU VIZURI SANA"....HII NI INTERVIEW YA LULU MICHAEL





Kwa mara ya kwanza muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael aka Lulu jana alifanya interview ya kwanza tangu atoke gerezani January mwaka huu. 

Lulu aliye na muonekano wa ‘udada’ zaidi alihojiwa jana kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV kinachoendeshwa na Zamaradi Mketema.
 Katia interview hiyo, Lulu aliongea masuala mengi kuhusu maisha yake ya sasa, mipango yake na mengine lakini akidai kuwa hatopenda kuongelea suala la uhusiano wake na Kanumba kwakuwa anahisi bado hajawa tayari ila muda ukifika atafunguka mengi. Haya ni baadhi ya masuala aliyoyazungumza.

Kuhusu uzinduzi wa filamu yake mpya Foolish Age


Ninaplan kufanya uzinduzi kwaajili ya movie yangu, lengo kubwa la kufanya uzinduzi ni kwamba kwanza nitajiskia vizuri kukutana na ‘okay these are my fans’ kukutana nao sehemu moja. Kuna vitu sitaweza kuongea kwenye interview ntahitaji kuviongea mwenyewe kama mwenyewe. 



Nitahitaji watu waone baadhi ya vitu vilivyopo kwenye movie. Movie inaitwa Foolish Age. Nitaizindua chini ya kampuni ya Proen (????) Promotions Ltd na ni kampuni ambayo ndio inanimanage kwa sasa.

Kuhusu kama ana boyfriend aliyemnunulia vitu vya thamani

Watanzania wengi tulishajiwekea ile dhana kwamba ‘ukiona mwanamke amefanya kitu basi there is a man behind, yaani ni ile dhani ipo tayari ndani yetu kwahiyo hata kama mtu atastruggle kutafuta kitu chake mwenyewe lakini hiyo itakuwa ni ukweli wako na unaujua mwenyewe . 



Kiukweli ni kwamba hakuna mwanaume yeyote ambaye amenifanyia chochote till now. Nachoshukuru tu ni menejimenti yangu, kampuni ambayo nafanya nayo kazi.


 Ni kampuni ambayo inanijali, inajali kazi zangu, inajali msanii wao kwahiyo whatever I’m having, whatever I’m doing ni mimi mwenyewe, ni kazi zangu ni biashara yangu.

Uhusiano wake na Mama Kanumba na jinsi alivyompata kufanya naye movie ‘Mapenzi ya Mungu’

Kwa sasa hivi tupo kama familia kwa hiyo it wasn’t hard mimi kumpata na nilijisikia vizuri kama ntaweza kufanya naye kazi. Kuna spirit ambayo ilinivuta zaidi nifanya kazi na Mama Kanumba kuliko labda mama mwingine.

Anachomiss kwa Kanumba

Busara zake, he was a person ambaye akikuona unaenda hivi he takes you in the right way.

Kuhusu kwanini mapenzi yake na Kanumba yalikuwa siri
Ni makubaliano tu and there was no need like to let people know yaani kumfanya kila mtu ajue nadhani haikuwa na maana kwetu.

Kuhusu kwanini alinenepa alipokuwa gerezani


Labda kwasababu nilimwachia Mungu kila kitu, nilimkabidhi Mungu kila kitu so I had this peace of mind. Niliacha kwamba yeye ni msimamizi wa kila kitu. Let me confess kwamba gerezani kumenifanya nimjue Mungu vizuri sana,. 



Kumenifanya nimjue na nimwamini na kumjua na kumwamini kumetokana kwamba kuna vitu vingi vimekuwa vinafanyika like naviona hivi kwa macho na naona kabisa kwamba hapa ingekuwa mimi kama mimi ama binadamu yeyote haiwezekani... 

So ni Mungu tu ndio ameweza kufanya hili likapita. Kwahiyo niliamua tu kumwachia yeye kila kitu nikajikuta tu nina amani.

KAJALA NA MZEE JENGUA HAWA HAPA USO KWA USO:






CONTINUE READING:









AJALI ZAENDELEA KUTUMALIZA WATANZANIA.....TUNAOMBA RADHI KWA PICHA


 Ajali hii ilitokea jana jioni  tarehe 02/07/2013, baada ya gari dogo lililokuwa linatokea maeneo ya Ubungo kwenda uelekeo wa Buguruni kumgonga mwenda kwa miguu aliyekuwa anavuka barabara katika maeneo Gereji (garage)...
Damu ilimtoka kwa wingi sana mara baada ya ajali katika maeneo ya kichwani, na hapo ilipotokea ajali kuna kivuko cha waendeo kwa miguu
Darubini Leo

DENT WA MWAKA WA KWANZA AIBA SIMU AINA YA BLACKBERRY NA KUIFICHA SEHEMU ZA SIRI:BALAA LAKE SASA SHUHUDIA MWENYEWE:


Tukio hili limetokea huko Nigeria ambapo binti anayesemekana ni wa mwaka wa kwanza alikwenda kutembea katika hostel za wenzake na alipopata mwanya akaiba simu aina ya Black Berry.

 Hata hivyo baada ya mwenye simu kushtuka binti huyo aligoma kuichukua simu hiyo na

ndipo watu
walipoamua kuipiga simu na kuanza kuita ikiwa sehemu za siri. Baada ya tukio hilo wavulana kutoka vyumba vya pembeni walikuja na kumsachi huku wakimvua nguo, hakuwa na la ziada zaidi ya kuwa mpole wakati watu wakimpiga picha hizo za aibu.

HAPA NDIPO ATAKAPOZIKWA MZEE MANDELA PINDI ATAKAPOFARIKI..



Hatua hiyo inatokana na uamuzi wa Mahakama wa kuamuru miili ya watoto wake watatu iliyohamishiwa Mvezo, ifukuliwe na kwenda kuzikwa tena Qunu
Pretoria.
Vita ya wapi atakapozikwa  Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela imefikia tamati na sasa ni rasmi kwamba atazikwa Qunu uamuzi ambao umeacha ufa na uhasama mkubwa katika familia ya kiongozi huyo.
CONTINUE READING
Jana, mabaki ya miili ya watoto watatu wa Mandela ambao ni marehemu ilitarajiwa kuzikwa upya katika eneo la Qunu, yakiwa ni mazishi ya mara ya tatu tangu walipofariki dunia katika vipindi tofauti, ukiwa ni utekelezaji wa amri ya Mahakama Kuu ya Eastern Cape.


Uamuzi huo ulimaanisha kushindwa kwa mjukuu wa Mandela, Mandla ambaye jana katika mkutano wake na waandishi wa habari alisema: “Sikusudii kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama,” lakini akahusisha ugomvi katika familia ya babu yake kwamba ni vita ya fedha na mali za Mandela.
Mabaki hayo ni ya mtoto wa kwanza wa kiume wa kiongozi huyo, Makgato aliyefariki dunia 2005, binti yake wa kwanza Makaziwe (mkubwa) ambaye alifariki akiwa mchanga mwaka 1948 na mtoto wake wa pili wa kiume, Madiba Thembekile aliyefariki katika ajali ya gari 1969.
Mahakama Kuu ya Eastern Cape ilitoa uamuzi uliowapa ushindi wanafamilia 16 wa Mandela ambao walifungua madai wakiongozwa na shangazi yake Mandla, Makaziwe.
Jaji Lusindiso Pakade katika hukumu yake, mbali na kutoa amri hiyo alitaja vitendo vya Mandla kuwa ni vya aibu visivyo vya kibinadamu hivyo kutoa amri ya kufukuliwa miili hiyo na kisha kurejeshwa Qunu. Mabaki hayo yalihamishwa kutoka kijiji cha Mvezo ambako yalizikwa mara ya pili kwa kificho miaka miwili iliyopita na mjukuu mkubwa wa Mandela, Mandla ambaye pia ni kiongozi wa kimila katika kijiji hicho.
Kazi ya kufukua makaburi ya watoto wa Mandela katika eneo la Mvezo ilifanyika hadi juzi usiku chini ya ulinzi wa polisi baada ya madalali wa mahakama kutumia sururu kuvunja lango (geti) kuu la kuingia katika makazi ya Mandla.
Kwa mujibu wa msemaji wa polisi wa eneo hilo, Luteni Kanali Mzukisi Fatyela, uchimbuaji wa makaburi ulifanywa na wataalamu wa Kituo cha Afya cha Mthatha na baadaye kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha kituo hicho juzi usiku na jana asubuhi mabaki ya marehemu hao yalifanyiwa uchunguzi wa kimaabara kabla ya kupelekwa Qunu kwa maziko.
Madaraka au fedha?
Makaziwe (60) ambaye ni binti mkubwa  wa Mandela na wenzake 15 kutoka katika familia hiyo, walifungua madai wakitaka kurejeshwa kwa mabaki ya miili hiyo Qunu wakisema Mandla aliyahamisha bila makubaliano ya familia. Mandla katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Mvezo jana alisema ugomvi uliopo ni wa kimasilahi na kwamba familia inawania fedha za babu yake.
Alisema chimbuko la kuandamwa linatokana na msimamo wake wa kukataa kuondolewa katika bodi ya ya mfuko wa Mandela baadhi ya watu wakiwamo Wakili George Bizos na Waziri wa Makazi Tokyo Sexwale. “Sasa wameamua kunilenga mimi kama mlengwa dhaifu.

DENT WA MWAKA WA KWANZA AIBA SIMU AINA YA BLACKBERRY NA KUIFICHA SEHEMU ZA SIRI:BALAA LAKE SASA SHUHUDIA MWENYEWE:


Tukio hili limetokea huko Nigeria ambapo binti anayesemekana ni wa mwaka wa kwanza alikwenda kutembea katika hostel za wenzake na alipopata mwanya akaiba simu aina ya Black Berry.

 Hata hivyo baada ya mwenye simu kushtuka binti huyo aligoma kuichukua simu hiyo na

ndipo watu
walipoamua kuipiga simu na kuanza kuita ikiwa sehemu za siri. Baada ya tukio hilo wavulana kutoka vyumba vya pembeni walikuja na kumsachi huku wakimvua nguo, hakuwa na la ziada zaidi ya kuwa mpole wakati watu wakimpiga picha hizo za aibu.

KUNDI LA BAIKOKO TOKA TANGA NI BALAA TUPU...WAPI TUNAKWENDA?


Hizi  ni  baadhi  ya  picha  za  kundi  la  wacheza  uchi / nusu  uchi  maarufu  kwa  jina  la  Baikoko  lenye  maskani  yake Tanga....