YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Monday 7 October 2013

MZEE ZAHIR ZORRO ALA SHAVU TUSKER PROJECT FAME, HAMMY B IS NO LONG A JUDGE



Mwanamuziki Mkongwe Hapa Tanzania Mzee Zahir Ali Zoro ambae pia ni Baba wa Banana Zoro Amepata shavu la kuwa Mmoja wa Majaji wa Shindano Kubwa la Tusker Project Fame ...Kuchaguliwa kwake kumekuja kwa kuondolewa kwa Producer Hammy B ambaye kwa miaka mingi alikuwa Judge katika Shindano hilo....

Hii ni Message iliyoandikwa na kituo kikubwa cha TV huko nchini Kenya kuhusu Ali Zoro,,

“Tanzanian music legend Zahir Ali Zoro joins the #TPF6 judging team. He’ll be one of the judges alongside @IanMbugua and @JKanyomozi,” kimeandika kituo cha runingo cha Citizen TV cha Kenya kinachorusha mashindano hayo.

ZITTO KABWE AMPONDA HADHARANI PINDA NA KUDAI KUWA NI MZIGO USIOBEBEKA SERIKALINI...!!




NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, amesema Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ni mzigo katika serikali. 
Amesema kuwa hii ni kutokana na kushindwa kufanya uamuzi mgumu katika masuala yanayolihusu taifa licha ya baadhi ya mambo kuwa katika mamlaka yake.
  
Zitto alisema kuwa hivi karibuni Pinda alishindwa kusimamia muswada wa sheria ya marekebisho ya mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013, hali iliyosababisha kutokea vurugu bungeni.
  
Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini, alitoa kauli hiyo juzi wakati akihutubia mikutano ya hadhara katika kata ya Inyonga na Songambele wilayani Mlele, mkoa wa Katavi, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara ya kuimarisha chama Kanda ya Magharibi.
  
Alisema ni jambo la kusikitisha kuona Waziri Mkuu akishindwa kukutana na kiongozi wa upinzani bungeni na kujadili masuala muhimu ya kitaifa kabla ya Bunge kuanza kwa ajili ya mustakabali wa taifa.
  
Akitolea mfano masuala kadhaa ambayo Pinda ameshindwa kuyasimamia na kumsubiri Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuyafanyia uamuzi, Zitto alitaja sakata la aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, na Yule wa Wizara ya Afya na sasa suala la kuhakikisha muafaka unapatikana katika suala muhimu la Kikatiba. 
“Kama tunaye Waziri Mkuu anayekaa bungeni na kushika tama wakati nchi ikiwa katika hali ngumu ni tatizo. Huyu kila jambo anasubiri Rais atoke UN kuja kufanya uamuzi ambao yeye angeweza kuusimamia. Basi tuna kazi ya ziada katika kupata maendeleo,” alisema. 
Zitto alifafanua kuwa mwanzoni alidhani Pinda anashindwa kusimamia majukumu ya serikali kutokana na kukabiliwa na jitihada za kuboresha miundombinu na maisha ya wakazi wa jimbo lake hali aliyoelezea kuwa ni tofauti na aliyoikuta. 
Alisema kutokana na hali hiyo ya Pinda kutokuwa na mamlaka, wakulima wa Katavi wameendelea kununua mbolea kwa gharama ya juu licha ya serikali kutenga kiasi cha bilioni 60 kwa mwaka kwa ajili ya ruzuku ya mbolea kote nchini.
  
Alisema fedha hizo zinaliwa na wajanja huku serikali ikiendelea kuwa katika hali ya usingizi wa pono.
  
Tofauti ya CCM, CHADEMA Akizungumzia sababu ya ziara yake katika kanda hiyo, Zitto alisema ni kwa ajili ya kuhimiza mbegu ya ukombozi wa fikra na maendeleo kutoka katika mikono ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
  
Alisema wakati CHADEMA inapambana katika kila kona kuhakikisha udhalimu unaofanywa na serikali unaondoka, CCM inatumia kila njia kuhakikisha inawanyonya wananchi.
  
“Tofauti kubwa kati ya vyama hivi ni kwamba CCM inaishi kwa kuwanyonya wananchi na CHADEMA imesimama kidete kutaka udhalimu huo uondoke; na kwa ajili hiyo chama hicho tawala kinatumia kila propaganda kuhakikisha wananchi hawatuungi mkono,” alisema. 
Kwa mujibu wa Zitto, kazi ya CHADEMA siku zote imekuwa ni kuwafumbua macho wananchi juu ya unyonyaji unaofanywa na serikali ya CCM na kuwataka waepukane na propaganda za kwamba kuiunga mkono CHADEMA ni kukaribisha vita nchini.
  
Alisisitiza kuwa kwa sasa CHADEMA inajiandaa kushika dola mwaka 2015 na kwamba wanasimamia upatikanaji wa Katiba bora itakayowafanya wanasiasa kuwa watumishi wa wananachi badala ya kuwa watawala.
  
“Mmetuona kwa uchache wetu bungeni tumeweza kufanya mambo makubwa kwa nchi kila kashfa ya ufisadi mnayoisikia leo ni wabunge wa upinzani wameibua na si wa chama tawala,” alisema. 
-Tanzania daima

UJENZI WA DARAJA LA KIMARA WAENDELEA KWA NGUVU


Kwa mbali kama linavyoonekana jinsi linavyoanza kujengwa
Ujenzi wa Daraja la Waenda Kwa miguu lilipo Kimara Mwisho ukiendelea vu huku hatua iliyofikiwa ni ya kuweka vyuma tayari kwa kujenga sehemu watakayopita waenda kwa miguu kama linavyoonekana katika picha mara baada ya kumalizika kwa ujenzi wa nguzo za daraja hilo

PICHA 6 ZA JENGO LA TTCL MAKAO MAKUU LILIPOKUWA LIKIWAKA MOTO LEO ASUBUHI



Jengo la TTCL, Makao makuu, EXTELECOMS limeungua moto kuanzia majira ya leo saa 12:00 asubuhi hadi saa 1:20.

Moto huo ulikuwa unawaka katika ghorofa ya sita ya jengo hilo na ulikuwa unawaka katika vyumba vitatu kwa mara moja.

Mwandishi wetu alifanikiwa kufika  katika jengo hilo na kujionea   mishe mishe za  wafanyakazi  wakiondoa magari yao na magari ya shirika hilo kongwe nchini.

Magari ya kikosi cha zimamamoto kutoka kikosi cha ukoaji cha Jiji la Dar es Salaam yaliwasili saa 12:20, lakini kulikuwa na ubishani kati ya wafanyakazi wa zima moto na wale wa TTCL, baada ya wafanyakazi wa Zimamoto kulaumu kuwa walienda pale siku kadhaa zilizopita kukagua jengo lakini walifukuzwa kama mbwa,

Licha ya Kikosi hicho kuwahi hawakuwa na maji yenye pressure na ngazi za nje kufika hadi ghorofani, hali iliyopelekea watu kutumia ngazi za ndani kuingia kwenye jengo hilo hali ambayo ni hatari kwa maisha yao.

Gari ya Ultimate Security walifika mnamo saa 12:30 na kwa ushirikiano moto uliweza kufanikiwa kuzimwa.




HAWA NDIO WASHIRIKI WANNE WANAO IWAKILISHA TANZANIA TUSKER PROJECT FAME



Hatimae Washiriki watakao iwakilisha Tanzania katika Mashindano ya mziki yanayo andaliwa na kinjwaji cha Tusker ,Tusker Project Fame wamejulikana ,
Washiriki hao ni  Angel, 23 yrs, Hisia, 21 yrs Tanah, 21 yrs na Dubson, 25yrs. Washiriki hao watakaa katika Academy ya music huko Nairobi kwa kipindi fulani huku wakichuana kupata washindi...Mashindano hayo ndio yamezaa wakali katika Bongo Flava kama Hemed na Peter Msechu.

Tuesday 1 October 2013

HII KALI YA MWAKA..MWANAMKE AVUA NGUO KATIKA MAZISHI NA KUANZA KUCHEZA KATIKATI YA WAOMBOLEZAJI



Members of BMW clubs across South Africa came in numbers to the 
funeral of skilled spinner, Bongani Makhubo (40) of Soshanguve, Tshwane....

As the cars spun around in circles, spectators cheered.Then a young woman took off her pánties and began dancing in the middle of the spinning cars.But not everyone was pleased to see her waving her underweár in the air.John Lelaka said: "People are allowed to celebrate but not in a way that disturbs other people's peace."Bongani died last week after a short illness.



The drivers respected the family during the formal burial ceremony at Soshanguve Cemetery.After the funeral, they had a spinning competition.About 300 gusheshe engines roared and the smell of burning rubber filled the air at Spin City.

The funeral was attended by spinning clubs from Mpumalanga, Limpopo and Pretoria.Puff Selotela, chairman of the Botsotso Social Club, told Daily Sun: "This is a way of celebrating one of our own and honouring his love for the game of spinning."Spinning is not only a thug sport. We have attorneys, doctors and businessmen in our spinning clubs.

"We all do it for the love of it."Reikhutise Malala, a longtime friend of Bongani, said in his farewell message: "You taught me how to be humble and inspired me to venture into business. I will remember you for your charisma, bravery and passion. "It is sad when someone dies and you never have the chance to tell them the impact they made on your life."I guess life is too short and we all need to live while we can."