YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday 22 April 2014

BINTI MIAKA 16 AONYESHA UJASIRI WA HALI YA JUU,ATOA SIRI ZA FREEMASON MWANZO MWISHO:



Binti Fauzia akiwa amepozi nyumbani kwao maeneo ya Kigogo jijini Dar es Salaam.

Na Waandishi Wetu

NI lipi hujasikia? Linaweza kuwa hili! Binti mmoja aliyetambulishwa kwa jina la  Fauzia (jina la mbele lipo), mwenye umri wa miaka 16, mkazi wa Kigogo jijini Dar amedai kutumikia nafasi ya umalkia katika imani yenye utata duniani ya Freemason, Uwazi linakudondoshea.

Binti huyo alikwenda mbele zaidi kwa kudai kwamba ili kujiunga na imani hiyo, alimuua mama yake mdogo kwa ajili ya kafara.

Akizungumza na gazeti hili siku chache baada ya kuokoka akiwa nyumbani kwa baba yake mdogo, Kigogo, Fauzia alisema alitokea Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga alipokuwa akiishi na bibi yake.

Alikuja Dar kwa lengo la kuendeleza mauaji ya kafara ambapo safari hii ilikuwa amuue mama yake mdogo mwingine ambaye ni mjamzito kwa sasa.

Alisema kama angefanikiwa kumuua, angepandishwa cheo na kuwa malkia kamili katika jamii hiyo inayotafsiriwa vibaya duniani.

ALIKOTOKEA
Fauzia alisema kuwa mara ya kwanza hakujua kama amekuwa mwanachama wa Freemason bali alichojua yeye alijiunga na uchawi wenye ushirika wa Kahama na Kigogo jijini Dar es Salaam ambapo mara kwa mara alikuwa akija Dar usiku na kufanya mambo ya kichawi kwa watu mbalimbali.

Alisema siku moja aliambiwa lazima amtoe uhai mama yake mdogo, naye kwa uwezo aliokuwa nao alifanya hivyo, mama yake mdogo akafa kwa kuugua ghafla.

Baada ya kifo cha mama yake mdogo, ndipo usiku mmoja bibi kizee mmoja (alimtaja jina) alimtokea katika ulimwengu wa kiroho na kumwambia alitakiwa aende kwenye Jiji la Lagos nchini Nigeria kwa ajili ya kutambulishwa rasmi na kupewa umalkia mdogo.

Baadhi ya vitu vinavyotumika kwa ajili ya kafara.
SAFARI YA NIGERIA ILIVYOKUWA
Akiendelea kuzungumza huku akionekana kujiamini licha ya umri wake mdogo, Fauzia alisema:
“Siku nilipoondoka kwenda Nigeria nilikuwa na wenzangu walionisindikiza. Ilikuwa ni safari ya kimiujiza. Tulipofika kule, wao waliniacha mahali, mimi nikajikuta nikitokea ndani ya jengo kubwa ambalo ndani yake nilikuta mtu mwenye asili ya Kiarabu.
“Yule mtu alinipokea na kuishi naye. Siku moja aliniambia Fauzia wewe una na nguvu mbili, za Freemason na uchawi,” alisema.
ASIMIKWA KUWA MALKIA MDOGO
Aliendelea kusema: “Ndipo siku moja ikafika, nikasimikwa kuwa malkia mdogo kwa kukabidhiwa gauni fupi jeupe na kitambaa cheupe cha kuvaa kichwani  (vilioneshwa kwa waandishi wa habari hii).
Hizi nguo ni dalili kwamba anayemiliki ni malkia mdogo. Unakuwa na uwezo wa kujua mambo yote ya siri ya kidunia yanayoendelea.
“Baada ya hapo,  nilirejea hapa nchini kwetu. Nilipokewa na bibi ambaye alikuja kimazingara. Bibi aliniuliza ni wapi nilikokuwa mpaka nimepata nguvu za Freemason wakati yeye alinikabidhi uchawi wa kawaida? Sikumjibu,” alisema Fauzia mbele ya baba yake mdogo na mama yake mdogo aliyekuwa amuue.
AKUMBUKA SIKU YA KWANZA KUJIUNGA NA FREEMASON
Katika mazungumzo hayo yaliyohudhuriwa pia na majirani, binti huyo akakumbuka jambo zito lililomtokea akiwa darasa la saba na kusema:
“Nakumbuka nikiwa darasa la saba, siku moja usiku niliota ndoto. Nilimwona mzee mmoja mwenye mapembe akinijia na kunikabidhi mikoba. Naamini yule mtu ndiyo aliniingiza kwenye Freemason kwani kuanzia pale ndipo nilipobadilika na kuwa na uwezo wa kuja Dar na kurudi Kahama kwa usiku moja.
“Basi, baada ya kurudi nyumbani Kahama, siku moja nikaambiwa na wakubwa wangu natakiwa kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kuongeza nguvu za Freemason.
“Kule nilikaa kwa siku kadhaa na nikafundishwa mambo mengi ya ajabu, pia nilikutana na viongozi wakubwa wa kidini na kiserikali wa hapa nchini Tanzania (aliwataja majina).
MAISHA YA NYUMBANI AKIWA SAFARINI
“Ilivyokuwa ni kwamba, kila nilipokuwa safarini, nyumbani nilikuwa naacha jini lililofanana na mimi kwa kila kitu. Jini hilo lilifanya kazi nyumbani badala yangu pasipo mtu yeyote kufahamu wakijua ni mimi. Niliporudi na jini liliondoka.

ATOBOA SIRI ZA SCREEN TOUCH

“Nikiwa katika jengo la ajabu la Freemason nchini Marekani, niliona watu wengi wakitengeneza simu za kisasa ‘screen touch’ na televisheni za ‘flat screen’ nilipowauliza za nini? Walinijibu kuwa simu hizo zimewekwa kifaa maalumu cha kunyonya damu ya mtumiaji kutoka kwenye kidole chake kila mara atakapobofya.
“Zamani kulikuwa na simu zikitumia peni maalum kwenye screen lakini Freemason waliamua kuziondoa kwa kuwa hazikuwa zikiwapelekea damu. Hivyo mtumiaji wa simu za screen touch za sasa lazima aguse kwa kidole chake na si kwa kitu kingine ndipo ataweza kutumia simu yake ilimradi tu achangie damu yake kwenye benki za damu za Freemason zilizopo Marekani.”
KUHUSU TV FLAT SCREEN
Akifafanua kuhusu runinga za flat screen, Fauzia alisema kuwa, hizo zimewekewa kifaa chenye mionzi ya ki-Freemason ambacho humfanya mtu anayeangalia kila wakati kuwa zezeta huku vifo vya ghafla akivitaja kama matokeo makuu ya kuangalia televisheni hizo.
AZUNGUMZIA SURUALI MAARUFU ZA SKIN TIGHT
Mbali na hayo, binti huyo alizizungumzia suruali maarufu za wasichana zinazotambulika kwa jina la  ‘skin tight’ ambazo hubana.
Alisema suruali hizo zimewekwa nyuzi maalum za kijini ambazo husababisha mwanaume yeyote ambaye atamuona msichana akiwa katika vazi hilo amtamani kingono hata kama msichana huyo havutii.
PASAKA NA X-MASS
Binti huyo alizidi kutia hofu watu pale aliposema kuwa Sikukuu za Pasaka na X-Mass zimekuwa kubwa duniani kwa sababu Freemason wametia mkono kwa kuzikuza na kutumbukiza akilini mwa watu tabia ya dhambi.
“Wengi wanaziona sikukuu hizo ndiyo za kufanyia maasi, kama vile ngono, ulevi kupitiliza na kufuru nyingine na wanaopotezewa uhai kwa ajili ya sikukuu hizo ni wengi sana,” alisema.
KUHUSU KUMUUA MAMA YAKE MDOGO
Kuhusu jaribio la kumuua mama yake mdogo, Fauzia alisema alishindwa mara zote kwa kuwa alikuwa ‘mzito’. Aliwataarifu Freemason wenzake wamuue lakini nao walishindwa na kudai kuwa alikuwa akiwaka moto.
Alidai kuwa mama mdogo huyo hakujua lolote lililokuwa likiendelea mpaka pale alipofika mpwa wao ambaye ni mlokole na kumuombea Fauzia.
MJOMBA MTU AZUNGUMZA
Akizungumza na waandishi wetu, mjomba wa Fauzia aliyejitambulisha kwa jina la Gervas ambaye ni mlokole, alisema kuwa kila mara alipokuwa akimuangalia binti huyo, alihisi ana mambo tofauti na binadamu wengine.
Alisema: “Siku moja nilimsikia roho wa Mungu akiniongoza kufika nyumbani hapa na kuomba. Nilijikuta nikimuita Fauzia na kuanza kumuombea.
“Nilishangaa sana kumwona  akipandisha mashetani na kuzungumza mambo ya kutisha aliyodai kuyafanya kwa siri. Baada ya  maombi ya muda mrefu nikisaidiwa na familia yangu ndipo nilipovitoa vifaa vya ajabu.”
BABA MDOGO AZUMGUMZA
Akizungumza na waandishi wetu, baba mdogo wa Fauzia aliyejitambulisha kwa jina la Amos Deda ambaye anaishi na binti huyo Kigogo na ambaye mke wake ndiyo alikuwa auawe, alisema:
“Sikuwa nikiamini kabisa kuhusiana na masuala haya mpaka nilipojionea mwenyewe vifaa hivi vya kichawi vya Freemason vikitolewa na mjomba wake.
“Fauzia ameniomba msamaha, pia ameomba msamaha kwa familia. Lakini pia akasema ajali iliyomvunja miguu shangazi yake miaka ya nyuma na kumuua mtoto wa shangazi yake huyo aliisababisha yeye, pia akaomba msamaha. Tumeupokea.”
Pia Fauzia aliiomba radhi kwa familia ya mama yake mdogo ambapo alidai kumuua mama huyo kwa kushirikiana na mkubwa wake mwingine.
NENO LA MWISHO
“Kwa sasa nimeokoka, nimeachana kabisa na mambo haya,  zaidi ninamtumikia Mungu kwa nguvu zangu zote,” alisema Fauzia.

Monday 21 April 2014

EXCLUSIVE DODOMA:PASAKA YAWA MBAYA,TAZAMA PICHA 15 MADUKA YAKITEKETEA KWA MOTO USIKU WA KUAMKIA LEO DODOMA MJINI:


PASAKA ILIKUWA MBAYA MJINI DODOMA BAADA YA MADUKA ZAIDI YA 4 KUTEKETEA KWA MOTO MJINI DODOMA MAENEO YA PARADISE
KIKOSI MAALUMU CHA ZIMA MOTO KILIFANYA JITAHADA ZA KUUDHIBITI MOTO HUO ILI USIWEZE KUSAMBAA ZAIDI












BAADHI YA VITU VILIVYOOKOLEWA

JITAHADA ZA KUDHIBITI MOTO ZIKIENDELEA

MWAFRICA HALISI AKISAIDIA KUZIMA MOTO

KIKOSI CHA ZIMAMOTO  KIKIENDELEA KUFANYA JITAHADA ZAKE KUDHIBITI MOTO HUO

Wednesday 16 April 2014

TUNDU LISSU " MWALIMU NYERERE ALIZOEA KUISHI KWA UONGO NA UDANGANYIFU"


Katika mwendelezo wa kupinga mawazo na mfumo wa utawala wa Mwl. Nyerere. Tundu Lissu amepasua jibu ambalo wengi huwa wanaogopa kulipasua pale aliposema kuwa Mwl. Nyerere alikuwa ni "msanii wa kisiasa" kwa sababu aliyokuwa anayasema siyo yale aliyokuwa anayatenda kuhusiana na suala la Muungano. Haya ameyabainisha wakati akitoa hoja kwenye Bunge Maalum.

Mh. Tundu Lissu ameenda mbali na kusema, Mwl. Nyerere alizoea vya halamu na vya halali hakuviweza. Katika kuthibitisha maneno yake, Mh. Tundu Lissu alisema, mwaka 1968, Mwl. Nyerere aliudanganya ulimwengu pale aliposema kupitia gazeti la Observer la UK, “Iwapo umma wa Zanzibar bila ya ushawishi kutoka nje, na kwa sababu zao wenyewe, wataona kuwa Muungano una hasara kwa uhai wao, sitawapiga mabomu kuwalazimisha......Muungano utakuwa hauna tena sababu ya kuendelea iwapo washiriki wake wataamua kutathmini na kuthibitisha jambo hasa tukio la kihistoria kama Muungano'.

Mwaka 1984, Wazinzibari walipohoji Muungano, Alhaji Aboud Jumbe akafukuzwa kazi kwa amri ya Mwl. Nyerere na amewekwa kizuizini Mjimwema mpaka leo. Wolfgang Dourado akawekwa kizuizini, Bashiri Swanzy akapakiwa kwenye ndege ya kwanza akapelekwa Ghana. 

Mh. Tundu Lissu aliendelea kusema, kwa vile Mwl. Nyerere alizoea vya kunyonga, kwenye Kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, Mwl Nyerere alisema, 'huko nyuma baadhi ya viongozi wapinzani wa Muungano wameishawahi kusema tufanye referendum kwa Zanzibar kuhusu Muungano, tukakataa kwa sababu safi kabisa'.

Tundu Lissu anadai, Mwl. Nyerere hakukataa hoja ya Muungano kwa sababu safi kabisa, bali aliwaweka kizuizini wale waliohoji Muungano. Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uwongo na hakuweza kusema kweli.

Kitu muhimu kabisa cha kujiuliza na kufikiria. Kama kweli Mwl. Nyerere alikuwa anaishi kwa uwongo na udanganyifu, ina maana hata hati ya Muungano haipo na kama haipo, ina maana amewaingizwa 'mkenge' wananchi na hasa wanaCCM kwa kusimamia hoja ambayo kiuhalisia haipo. (Muungano wa serikali mbili).

Tukikubaliana na hoja ya Tundu Lissu, inabidi tujiulize, Kwa nini Baba wa Taifa alikuwa anaishi maisha ya uwongo na udanganyifu?. Alikuwa anafanya hivyo kwa manufaa ya nani?.

Kama hoja ya Tundu Lissu ni kweli basi hatuna budi kusema, kweli uwongo hupanda lifti wakati ukweli hutumia ngazi kuwafikia walengwa!.

Hoja hii inanipeleka kwenye angalizo la sababu ya baadhi ya wajumbe wakiongozwa na Leticia Nyerere kushauri bunge kwa nguvu zote liweke mipaka kwenye kanuni za bunge zikiwataka wabunge kutowadharirisha waasisi wa Muungano. Kumbe nyuma ya hoja zao walikuwa wanaogopa ukweli usijulikane!.

Mpaka katiba mpya ipatikane, tutaona na kusikia mengi!.

Kauli mbiu ni serikali moja au kila nchi ichukue fito zake kwa sababu watu tuliowatuma kwenda kumalizia mchakato wa katiba kwa sasa wanahoji uharali wa Muungano huku wakitaka mpaka makaratasi yenye sahihi za waasisi wa Muungano. Hawa wabunge wameshindwa kufanya kazi ya kumalizia mchakato wa Katiba badala yake wanaanza kuuliza kama Muungano ni halali au batili. Yaani baada ya Miaka karibia 50 ndiyo tunaanza kuuliza Muungano kama ni halali huku waasisi wa Muungano tukiwasema ni waongo na wadanganyifu.

Ninadhani kuna kitu hakiko sawa kwenye baadhi ya hoja za Wabunge!. ANGALIA VIDEO HAPA:
0 comments

MAGAZETI YA LEO TAREHE 16/4/2014

.
.
Ni utaratibu wa millardayo.com kila siku kukupa nafasi ya kusoma kurasa za mwanzo na mwisho za magazeti mbalimbali ya Tanzania.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.