YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Friday 4 July 2014

STORY YA UGOMVI WATANGAZAJI WA CLOUDS FM


xxlJumatano July 02 kupitia kipindi cha XXL zilisikika kelele za ugomvi hewani ambazo asilimia kubwa tuliamini kuwa ni za kweli hasa kutokana na baadhi yao kusikika kama wamekabwa huku wengine wakitaja majina ya viongozi kuja studio kuamulia ugomvi huo.
kila mmoja kwa nafasi yake anatamani kujua chanzo hasa cha kugombana lakini kupitia kipindi cha XXL leo July 04,wameeleza ukweli juu ya kilichotokea na kusema hii wamefanya kwa ajili ya kampeni ambayo Clouds Media Group wanaiendesha kwa sasa waliyoipa jina la Paza Sauti.
xxl3Kampeni hii inalenga kuhamasisha utoaji wa taarifa ambazo unaziona mtaani kwako kama haziko sawa kutoa taarifa hasa kwa vyombo vya dola ikiwemo Polisi ili kwa pamoja tuidumishe amani tuliyonayo Tanzania,Paza Sauti,Ukimya Hausaidii..
dozen11Bonyeza play kusikiliza maana halisi ya Paza sauti.
MAONI
SHARE

BOT YATANGAZA KULETA SARAFU YA SHILINGI 500


noti
Baada ya kubainika noti ya shilingi 500 kuwa na mzunguko mkubwa wa matumizi, na kuchakaa kwa haraka huku kiwango chake kudumu kwenye mzunguko kwa miezi sita, Benki kuu ya Tanzania (BOT), inatarajia kubadili noti hiyo na kuwa sarafu.
Sarafu hiyo ya 500 inatarajia kutambulishwa na kuanza kutumika hivi karibuni ikienda sambamba na kipindi cha mwaka huu wa fedha.
Mabadiliko hayo yanatarajiwa kufanyika huku sarafu hiyo ikitarajiwa kudumu kwenye mzunguko kwa zaidi ya miaka 20 na kubaki na ubora
wake ule ule.
Afisa mkuu wa benki kitengo cha idara kurugenzi za kibenki, Patrick Fata, amenukuliwa akisema kuwa “Tunafanya hivi kwasababu noti ya 500 inachakaa haraka kulinganisha na mzunguko wake na kuwafikia watu wengi na kuchakaa haraka, utengenezaji wake ni ule ule ila inachaa kutokana na mzunguko inaweza kushikwa na watu milioni moja kwa siku kuliko noti ya elfu 10.”
“Inaanza kutumika mwaka huu wa fedha inategemea kutoka Julai mwaka huu.”- Fata
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta FB

DARAJA LABOMOKA NA KUUA WATU HUKO BRAZIL


darajaDaraja limebomoka na kuua watu wawili huku wengine zaidi ya 10 wakijeruhiwa katika mji ambako mechi za nusu fainali zikitarajia kuchezwa nchini Brazil.
daraja2
Tukio hilo limetokea katika mji wa Belo Horizonte wakati magari yakipita chini ya daraja ambapo moja ya malori lililokuwa limebeba gari na ujenzi na gari moja lilinasa kwa mujibu wa maafisa.
daraja3
daraja4
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta FB