YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday 19 August 2014

HUU HAPA NDIO UJUMBE ALIOTOA HASHEEM THABEET KWENDA KWA MASHABIKI WAKE WOTE


http://larrybway91.files.wordpress.com/2014/07/hasheem-thabeet.jpg
NINGEPENDA KUANZA KWA KUSEMA ASANTENI SANA KWA KUSHOW LOVE KWENYE HILI PAGE LANGU. BINADAMU WOTE TUMEUMBWA TOFAUTI, NA TUMEBARIKIWA TOFAUTI. 

SOTE TUNA MAPUNGUFU NA SOTE TUNA MAMBO AMBAYO NDIYO YANAYOTUFANYA TUWE WATU AMBAO TULIVYO SASA. KWA HIYO KAMA ULISHAWAHI KUONGEA NA MIMI UTANIJUA NI MTU WA AINA GANI.

NA KAMA TULISHAWAHI KUKUTANA NA LABDA HATUKUELEWANA KAULI ZETU NAOMBA UNISAMEHE MIMI NI BINADAMU NA NAKOSEA KAMA WATU WENGINE TU. NA NINA MAMBO MENGI YANAENDELEA NIKIWA KAMA BINADAMU NA SIO KUWA NARINGA KWA AJILI YA USTAA AU KITU GANI.

MWISHO WA SIKU SOTE TUNAPITA TU HAPA, JANA ILIKUWA WAO, LEO MIMI, KESHO KUNA WENGINE WANAKUJA. HILO MUNGU NDIO ANAJUA.

NA KAMA HAUJAPATA HIYO NAFASI SIKU MOJA TUTAKUTANA. INSHALLAH

Monday 18 August 2014

MAGAZETI YA LEO TAREHE 19/8/2014

.
.
Kama kawaida millardayo.com inakupa vichwa vya habari vya magazeti yote ya kila siku. Leo pia kuna headline mpya kwenye magazeti mbalimbali. Chukua muda wako kupitia kila kilichoandikwa kwenye kurasa za mbele za magazeti ya leo.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
,
,
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Ni

TRAFIKI ALIEGONGWA NA GARI BAMAGA HUYU HAPA

Askari mmoja wa kikosi cha usalama barabara ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, amenusurika kufa baada ya kupata ajali akiwa
anaendesha pikipiki ya polisi,ambayo ilikosa mwelekeo na kugongana uso kwa uso na gari dogo lenye namba za usajili T 681 CUX eneo la Bamaga Mikocheni jijini Dar es salaam

MWANAUME ALIEJIFANYA HOUSE GIRL ATIWA MBALONI





Mwanaume mmoja huko nchini Uganda Amekamatwa baada ya Kujifanya ni Mwanamke ili apate kazi ya House Girl, Zoezi lake hilo lilifanikiwa na kuweza kupata hiyo kazi lakini siku zilivyozidi kwenda Boss wake ambae ni Mama Mwenye Nyumba alishtukia mchezo na kugundua ni Mwanaume, Baada ya kugundulika jamaa alichukua kipigo kutoka kwa Majirani , alipoulizwa kwanini ameamua kufanya hivyo alijitetea akasema Maisha ni magumu na kupata kazi kama mwanaume ni ngumu...

WAANGUKIWA NA JIWE WAKIWA WAMELALA

Watu 4 Wafariki Kwa Kuangukiwa na Jiwe Wakiwa Wamelala


Watu wanne wa familia mbiili tofauti wakazi wa mtaa wa Nyerere A, eneo la Mabatini jijini Mwanza wamefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuangukiwa na mawe wakiwa wamelala.

Tukio hilo limetokea majira ya saa Nane usiku wakati mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali pamoja na radi ilipokuwa ikinyesha.

EATV imefika katika eneo la tukio na kushuhudia wananchi wakishirikiana na jeshi la uokoaji na zimamoto pamoja na askari polisi wakiendelea na kazi ya kufukua miili iliyonasa chini ya jiwe kubwa.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Nyerere A, mabatini jijini Mwanza Hassan Maulid amewataja waliofariki dunia kuwa ni Sayi Otieno na Kwinta Kweko ambao ni mume na mke huku watoto wawili Kelfine Masalu na Emanuel Joseph wa familia ya Bw.Joseph William nao pia wakipoteza maisha baada ya chumba walichokuwa wamelala kuangukiwa na jiwe lililoporomoka kutoka juu mlimani.

Kaimu kamanda wa jeshi la uokoaji na zimamoto mkoa wa Mwanza inspekta Augustino Magere amewashauri wakazi wa jiji la Mwanza waishio maeneo ya milimani kuchukua tahadhari ili kuepusha maafa kama yaliyojitokeza.

Wakisimulia tukio hilo katika hali ya majonzi na simanzi, baadhi ya wakazi wa mtaa huo wa Nyerere A, wanaeleza namna walivyoupokea msiba huo mkubwa.

Huyu ndiye mtoto pekee aliyenusurika kifo baada ya wazazi wake kufariki dunia kufuatia nyumba yao kuangukiwa na jiwe kubwa

KAULI KUTOKA KWA MACHANGUDOA

MACHANGU: HATUTAACHA KUJIUZA NG’O, HATA WAKIKAMATWA WANARUDI TU



Wadada hao waliyasema hayo, juzi Jumatano baada ya kunaswa na paparazi wetu maeneo ya Sinza Afrikasana pembeni ya Corner Bar ikiwa ni siku chache baada ya baadhi yao kukamatwa na polisi ambapo walisema biashara hiyo ndiyo maisha yao.
Walisema, hawapendi kuifanya lakini wanalazimika kutokana na maisha duni waliyonayo. 
“Nani asiyependa kulala usiku na familia yake? Ukituona barabarani ujue hali ni mbaya. Hata kama polisi wanatukamata lakini wanatuachia na tunarudi sokoni kama kawaida,” alisema changu mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Zuena na kuongeza:
“Wateja wetu wenyewe wanajua kuwa hii nguvu ya polisi ni ya soda tu, wakiona tumepigwa ambushi kidogo wanasubiri zipite siku chache kisha tunaendeleza harakati zetu, sisi bila kuja kujiuza hatuwezi kuwasomesha watoto wetu wala kuwalisha.” 
Katika hali ya kushangaza wakati changudoa huyo akizungumza hayo, wapo waliokuwa wakimshawishi paparazi wetu anunue ngono kwa maelezo kuwa, hali ni mbaya kwani polisi wamekuwa wakifanya doria mara kwa mara.
“Sasa, achana na mambo ya kutuhoji bwana, tutoe basi kama vipi tukuuzie mambo kwa bei ya ofa. Cheki nilivyojaaliwa,” alisema binti mmoja ambaye ukikutana naye mchana unaweza kusema, ‘mke si ndiyo huyu’.
Hata hivyo, katika pitapita ya mwandishi wetu maeneo mengi kama vile Kinondoni, Sinza Mapambano, Mwenge Bamaga na Buguruni, madadapoa hao wameonekana wakiendelea kujiuza kwa kuibia huku wakiwa makini na kila mteja anayewatokea. 
Aidha, gazeti hili linalipongeza Jeshi la Polisi jijini Dar kwa operesheni ambazo limekuwa likizifanya kwani kwa namna moja ama nyingine kasi ya biashara hiyo imepungua licha ya kwamba wanatakiwa kuongeza nguvu zaidi. Pia taasisi za ustawi wa jamii na serikali kwa jumla zinatakiwa kuangalia mbinu mbadala za kuweza kuwaondoa akinadada hao kwenye mazingira hayo hatarishi. 



MAONYESHO YA BIASHARA YA BIDHAA ZA KICHINA KUANZA TAREHE 21 HADI 24 MWEZI HUU DIAMOND JUBILEE


 Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na KilimoTanzania Bw. Daniel Machemba akiongea na waandishi habari (hawapo pichani) kwenye mkutano wa waandishi kuhusu maonyesho ya bidhaa za Kichina, kushoto kwake ni Mwakilishi wa Uchumi na Biashara kutoka Jamhuri ya Watu China nchini Tanzania Bi.Wang Fang, na kulia kwake ni Bi Rehema Mtingwa Afisa wa Mawasiliano kutoka TPSF.
 
 Baadhi wa washiriki waliohudhuria kwenye mkutano wa waandishi kuhusu maonyesho ya bidhaa mbalimbali  za Kichina yatakayoanza tarehe 21 hadi 24 mwezi huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam.

 Mwakilishi wa Uchumi na Biashara kutoka Jamhuri ya Watu China nchini Tanzania Bi.Wang Fang akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani).
 Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na KilimoTanzania Bw. Daniel Machemba akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa biashara kutoka Jamhuri ya Watu wa China mara baada ya mkutano na Waandishi.