YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Wednesday 3 September 2014

NI SHEEEEEDAH, NDOA YA SHABIKI WA MAN UTD





Tazama hii ndo ilikua keki







UMEONA GARI 50 CENT ALIYOMNUNULIA MWANAE WA MIAKA MIWILI????


Written By Bongo Admin on Wednesday, September 3, 2014 | 9/03/2014 01:31:00 AM

50 Cent Buys Son Miniature Car For His Birthday | PHOTO:






Rapper, 50 cent recently bought a miniature Mercedes benz

 ML 450 SUV for his 2 year old son, Sire as a birthday gift. 


50 surprised the little man with the gift in Los Angeles last 

weekend. Benefits of having a rich ass father! See another 

photo below…..   




MAWAKALA WA MAKOMANDOO WA NEPAL WALIOTUA NCHINI KINYEMELA NA KUJIFANYA 'WALINZI' WAPANDISHWA KORTINI


MKURUGENZI wa Kampuni ya Ulinzi ya Advanced Limited, Juma Ntinginya (47) na wenzake wawili, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuwahifadhi raia wa Nepal.
 Washtakiwa hao walipanda kizimbani jana mbele ya Hakimu Mkazi, Devotha Kisoka na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali kutoka Idara ya Uhamiaji, Patrick Ngayomela.Ngayomela alidai washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Meneja uendeshaji wa kampuni hiyo, Henry Mwakipunda (34) na dereva Hamza Sefu (30).Akiwasomea mashtaka yao, Ngayomela alidai kuwa Agosti 29 mwaka huu, maeneo ya Kijitonyama, wilayani Kinondoni, kinyume na sheria, washtakiwa waliwahifadhi raia wa Nepal huku wakijua kufanya hivyo ni kosa.
 
Washtakiwa wote walikiri kutenda makosa hayo na kwamba waliwaingiza raia hao kwa nia ya kufanya kazi katika kampuni yao. 
 
Inadaiwa viza walizokuwa nazo zilikuwa kwa ajili ya kutembea nchini na si kufanya kazi.
 
Hakimu Kisoka aliwahukumu washtakiwa kwenda jela mwaka mmoja au kulipa faini ya Sh 100,000 kila mmoja. Wote walilipa faini na kuachiwa huru. 
 
Wakati huo huo, mshtakiwa Halit Gurbuz (33) ambaye ni raia wa Uturuki, alipandishwa kizimbani katika mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru, kwa makosa mawili ya kuishi nchini na kufanya kazi bila kibali.
 
Ngayomela akimsomea mashtaka, alidai Agosti 30 mwaka huu maeneo ya Mikocheni, mshtakiwa akiwa raia wa Uturuki, alikutwa akiishi nchini bila kibali. 
 
Katika shtaka la pili, anadaiwa huku akijua hana kibali cha kuishi nchini, alikuwa anafanya kazi Kampuni ya Techno Plus bila kibali cha kumruhusu kufanya hivyo.
 
Mshtakiwa alikiri kosa na Hakimu Mchauru aliahirisha kesi hiyo hadi leo kwa ajili ya kumsomea hukumu. Hata hivyo, mshtakiwa alikwenda mahabusu Keko.
 Komandoo Sidhee Bahadurkatuwal (kulia) kutoka Nepal akionesha nyumba ya Mrwanda aliyokuwa akiilinda kupitia kampuni ya Ulinzi ya Advanced Security karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, akiwa na makomandoo wenzake kutoka Nepal.

SHOCKING: KICHENI PATI YA LUCY KOMBA WA BONGO MOVIES YAWADUWAZA WATU WENGI!


NI mshangao! Sherehe ya kicheni pati ya staa wa filamu Bongo, Lucy Komba imewashangaza waalikwa wengi baada ya kutawaliwa na vitu vingi vya kiasili tofauti na matarajio ya wengi.
Staa wa filamu Bongo, Lucy Komba.
 Sherehe hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo mbali na watu wa kawaida, wake wa viongozi mbalimbali nchini pamoja na baadhi ya wasanii wa Bongo Movies walihudhuria. 

Miongoni mwa matukio ambayo yaliibua mshangao kwa waalikwa ni bibi harusi mtarajiwa (Lucy) kutinga ukumbini hapo akiwa ndani ya baiskeli yenye magurudumu matatu (guta) akiwa na wapambe wake ambao walikuwa peku miguuni. Kwenye guta hilo lililotengenezewa kibanda cha asili kilichowekwa nyasi juu, Lucy alikaa ndani yake huku wapambe wake wakiwa wameshika nyungo ndogo kuashiria asili ya Mtanzania.
Akiwa kwenye usafiri wa baiskeri ya matairi matatu maarufu kama 'Guta'.
 Kama hiyo haitoshi, Lucy aliwaacha hoi waalikwa kutokana na vazi lake ambalo ni tofauti na wanavyovaa wengine katika sherehe kama hiyo kwani alitinga kipensi kifupi kwa ndani chenye rangi ya bendera ya Tanzania huku kwa nje kikifunikwa na kitambaa chepesi. 

“Ama kweli hii ni ya aina yake, hebu angalia nguo yake alivyoitengeneza kwa kweli inavutia sana, full utamaduni,” alisikika mmoja wa watu walioudhuria sherehe hiyo.  Ulipofika wakati wa kufungua shampeni, nayo ilikuwa ya aina yake. Aliandaliwa pombe ya kienyeji ya mkoani Ruvuma ijulikanayo kama Kangara ambayo aliiweka ndani ya kibuyu kidogo huku akipita kugongesha na wageni waalikwa.
Akiingia ukumbini kwa mbwembwe.
 Baadhi ya marafiki zake waliotoka nchi mbalimbali akiwemo muigizaji kutoka nchini Italia, Angela Howell, alidondosha chozi la furaha alipoona waalikwa wanakula ndafu badala ya keki kama ilivyozoeleka na wengi. 

Lucy Komba anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni na mchumba wake aitwaye Stanley, raia wa Denmark. Watafanya sherehe kubwa Bongo na baadaye kuangusha nyingine Denmark.

JUMBA LA BIG BROTHER AFRICA LATEKETEZWA NA MOTO! SHOW IMEAHIRISHWA


big brother africa house jumba nyumba imeungua moto Jumba la Big Brother Africa lateketezwa na moto! Show imeahirishwa

Msimu huu wa Big Brother Africa, “Hotshots” ambao umekuwa na mkosi kukumbwa na skendo, umekumbwa na balaa lingine baada ya jumba lililotarajiwa kufanyika show hiyo kuungua moto. Watayarishaji wa show hiyo, M-Net na Endemola wako katika hekaheka za kutafuta jumba lingine, lakini bado hawajafanikiwa. Janga hilo limepelekea waandaji hao kuahirisha uzinduzi wa bBA Hotshots kwa muda usiojulikana. Show hiyo ilikua imepangwa kuanza Jumapili September 9, kabla balaa hili halijatokea.

PICHA ZIKIONESHA JINSI SHOW YA DIAMOND ILIVYOVURUGWA NA KICHAPO NCHINI UJERUMANI









SINCE DIAMOND ALICHELEWA KUFIKA UKUMBUNI WATU WALIKASIRIKA SANA NA KUANZA KUFANYA FUJO KUHARIBU VENUE IKABIDI POLISI WAITWE NA AMBULANCE NA KWAVILE WATU WALIKUWA WANA HASIRA IKABIDI DIAMOND ATOLEWE PALE NA POLICE ESCORT SO NILIVYOELELEWA NIKWAMBA HATA SHOO HAKUWEZA KUFANYA TENA,,HII INASIKITISHA NINA MASWALI MENGI SANA JE PROMOTA NDIO ANA KAZI YA KUMLETA MSANII KWENYE VENUE INAKUWAJE WALIMCHELEWESHA KUJA UKUMBINI?NA HIVI MNAMHARIBIA MSANII REPUTATION YAKE NA BRAND YAKE NA NYIE WENYEWE PIA,,JAMANI ITS TIME FOR CHANGES INTHIS INDUSTRY,,NA SIKU NYENGINE DIAMOND USIKUBALI KABISAA KUCHELEWESHWA WEWE SIO MGENI BALI NDIO STAR WA SHOW AND PEOPLE CAME TO SEE YOU SO UNA POWER KUBWA SANA AU WEKA KWENYE MKATABA WAKO MIMI NAPANDA STAGE MDA HUU NA WAO WATANGAZE ILI WATU WAJUE,,,




Y

Tuesday 2 September 2014

SAKATA LA MKE WA KAMANDA BARLOW, MAPYA YAIBUKA!



Sakata la madai kuwa mke wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, Stella Barlow (pichani)alitimuliwa ukweni kwa mapanga limechukua sura mpya baada ya ndugu wa mumewe kuibuka na kutoa ufafanuzi.
Mjane Stell Barlow wakati wa mazishi ya aliyekuwa mume wake, Kamanda Liberatus Barlow.
 Akizungumza kwa njia ya simu mwishoni mwa wiki iliyopita, ndugu wa marehemu Kamanda Barlow, aliyejitambulisha kwa jina moja la Lyimo alisema si kweli hata kidogo kuwa walimkimbiza kwa mapanga shemeji yao huyo. 
“Kilichotokea ni kwamba tulimuambia huyo mama kuwa hawezi kufanya chochote kwenye kaburi la mumewe mpaka akamuone kiongozi wa ukoo. Kimila tangu wakati kaburi linachimbwa, linakuwa chini ya uangalizi wa wanaume na hata baada ya kuzika haliwezi kuwa chini ya mwanamke, hilo tulimjulisha,” alisema Lyimo.
Kamanda Barlow enzi za uhai wake.
 Alifafanua kuwa wamewahi kufanya misa ya kumuombea marehemu Barlow na ndugu wengine na mama huyo aliarifiwa lakini hakuja. “Ujumbe wetu ni kwamba muambieni huyo mama  kuwa siyo vizuri kuchafua ukoo kwa sababu hatuna ugomvi naye na hakika kama ni wa kulaumiwa ni yeye siyo sisi wana ukoo,” alisema Lyimo.

NGOMA MPYA KALI: USHAWAHI MSIKIA DIAMOND AKICHANA?! HUYU HAPA AKIWA AKIWA NA GODZILLA!



BONYEZA DOWLOAD AU PLAY HAPA CHINI..
U

WARAKA WA MAKANISA KUHUSU KATIBA MPYA WAZAGAA MITAANI




Iringa. Waraka uliotolewa juzi na Jukwaa la Wakristo Tanzania wakitaka mchakato wa Katiba Mpya usitishwe, jana ulisomwa katika baadhi ya makanisa na sasa utasambazwa katika jumuiya ndogo za Kanisa Katoliki.
Akizungumzia waraka huo katika Ibada ya Jumapili, Paroko wa Parokia ya Mkwawa ya Kanisa Katoliki Jimbo la Iringa, Padri Oscar Rutechura alisema amechukua uamuzi huo ili kuwawezesha waumini kuelewa vizuri tamko la viongozi wao wa dini kuhusu mchakato wa katiba unaoendelea.
“Katika ibada hii ya leo nitatoa mahubiri kwa muda mfupi, nitafanya hivyo ili niweze kufanya mambo mengi yaliyoko mbele yangu,” alisema Padri Rutechura kabla ya kusoma waraka huo.
Waraka huo ulitolewa kwa pamoja na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (FPCT) na Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA).
Padri Rutechura alitaja mapendekezo sita yaliyomo kwenye waraka huo ambayo ni: Kuitaka Serikali irudishe tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kulitaka Bunge kuboresha maoni ya wananchi yaliyomo kwenye rasimu ya Katiba na kuacha kuyadharau na kuyapuuza.
Mengine ni kutaka mchakato wa Katiba usitishwe, Bunge la Katiba liendeshwe kwa mujibu wa kanuni, wananchi waendelee kusoma na kufuatilia mchakato na Tume ya Mabadiliko ya Katiba ihusishwe na kupewa mamlaka ya kujibu maswali yanayojitokeza.
Padri Rutechura alisisitiza kuwa ametumiwa waraka huo na Askofu wa Jimbo la Iringa, Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa ambaye kwa sasa ndiye Rais TEC kwa ajili ya kuusoma kwa waumini wote.
Alisema baada ya kuusoma angetoa nakala na kuzigawa kwa viongozi wa jumuiya ndogondogo ili waumini wote wa parokia hiyo wapate fursa ya kuusoma na kuuelewa na watoe uamuzi sahihi.
Padri Rutechura aliwataka waumini kuhakikisha wanajiandikisha kwa wingi kwenye daftari la kudumu la wapigakura pindi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) itakapotangaza kuanza kuandikisha upya wapigakura.
Alisema hatua hiyo itawasaidia waumini hao kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kupiga kura ya maoni kupata Katiba Mpya au kuipinga, kuchagua viongozi wanaofaa katika uchaguzi wa serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu wa mwakani.
Wakati huohuo, polisi wilaya mpya ya kipolisi, Mbalizi mkoani Mbeya wamewakamata waumini 16 wa Kanisa la Katoliki, Parokia ya Songwe kwa madai ya kutaka kufanya vurugu kwenye kanisa lao.
Paroko wa Parokia hiyo, Ernest Mwashiuya alisema waumini hao walikamatwa jana na kwamba taarifa zaidi zitatolewa na polisi.
Baadhi ya waliokamatwa walisema tukio hilo lilitokea Jumamosi saa 12 jioni wakati wanajadili sehemu ya kusalia ibada ya Jumapili baada ya kutokuwa na imani na paroko wao. Walisema hatua hiyo ilichukuliwa baada ya Paroko Mwashiuya, Jumapili ya Agosti 24 kutamka kwamba waumini wasio na imani naye wasifike kanisani hapo tena.
“Polisi walifika nyumbani kwa Emmanuel Kalomba tulikokuwa tukisali na kutukamata,” alisema mmoja wa waumini waliokamatwa na kuachiwa kwa dhamana.

INASIKITISHA LAKINI INAFUNDISHA PIA, KUTANA NA MTU HUYU ALIYEZALIWA KICHWA CHAKE KIKIWA MGONGONI


A man born with physical disabilities so severe his head is Upside-down has defied the odds to become an inspirational public speaker.

Claudio Vieira de Oliveira, 37, was born with his neck folded back on itself, as well as badly deformed legs and almost no use of his arms and hands. Doctors told his mother to stop feeding him as a newborn as they believed he had no chance of survival. But Claudio from Monte Santo, Brazil, has overcome his extreme disadvantages to graduate as an accountant and become a public speaker. 
"Since I was a child I've always liked to keep myself busy and work - I don't like to depend totally on other people. I do a bit of accounting, research for clients and consulting. I have learned to turn on the TV, pick up my cell phone, turn on the radio, use the internet, my computer - I do it all by myself." he said.
Claudio types with a pen held in his mouth, operates phones and a computer mouse with his lips and has specially made shoes that allow him to move around town. His determined independence saw him succeeding at school and qualifying as an accountant from the State University of Feira de Santana.

When Claudio was born, doctors told his mother Maria Jose he would not be able to survive. Maria Jose said:
"People started saying 'the baby is going to die' because he could barely breathe when he was born. Some people would say: 'Don't feed him, he is already dying'. But there's only happiness now. Claudio is just like any other person - that's how he was raised in this house. We never tried to fix him and always wanted him to do the normal things everyone else does. That's why he is so confident. He is not ashamed of walking around in the street - he sings and he dances."
At eight years old, Claudio, who had previously been carried everywhere, began to walk on his knees.

His family had to change the floor of the house so he could walk around without injuring himself.
Claudio's bed, plugs and lights had to be made lower so that he could do things for himself without asking for help.

He cannot use a wheelchair because of his unusual shape, making it hard for him to be independent outside the home - but he begged his mother to be allowed to go to school and learn with the other children. Doctors have recently diagnosed him with a rare condition called congenital arthrogryposis.

They believe he has multiple joint contractions in his legs and arms which mean they cannot extend properly. Claudio said:
"Throughout my life I was able to adapt my body to the world. Right now, I don't see myself as being different. I am a normal person. I don't see things upside-down. This is one of the things I always talk about in my interventions as a public speaker.
"Nowadays it's much easier to deal with the public, I'm not afraid of it anymore and I can say that I am a professional, international public speaker and that I receive invitations from all over the world."

AJALI: [PICHAZ] MWANAMKE AGONGWA NA DALADALA UBUNGO MAJI



Raia wakijaribu kuokoa maisha ya dada aliyegongwa na gari (daladala) maeneo ya Ubungo maji wakati akivuka bara bara.
 
Majeruhi (dada huyo) akichukuliwa kwenye gari na wasamaria wema.
 
HiIi ndilo gari aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili T454 BBV lililomgonga dada huyo.
 

 
Mwanamke mmoja (jina halijafahamika) aliyekuwa anavuka barabara ya Morogoro maeneo ya Ubungo maji kutoka ng'ambo ya tank na kuelekea upande wa Tanesco amegongwa na gari ya daladala aina ya Toyota Coaster lililodaiwa kuvunja sheria likiwa  linapita kwenye barabara ya magari ya mwendo kasi.
 
Katika ajali hiyo dereva wa basi(daladala) hakupatikana kwani alikimbia baada ya ajali.