YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday 16 September 2014

BREAKING NEWZZ: WALIOKUFA KWENYE KANISA LA TB JOSHUA LILILOPOROMOKA WAFIKIA 50..!

Idadi ya watu waliokufa kwenye ghorofa la makao makuu ya Kanisa la SCOAN (Synagogue Church of All Nations) la Nabii TB Joshua wamefikia 50.
Jengo hilo la ghorofa tano ambalo ni makao makuu ya kanisa na nyumba ya kulala wageni liliporomoka Jumamosi  wakati ujenzi ukiendelea.Hadi kufikia jana Jumapili jumla ya watu 41 walikuwa wameripotiwa kufa, lakini maiti nyingine tisa zimeongezeka leo hii.Inaelezwa kwamba, mhubiri huyo wa kimataifa alipewa kibali cha kujenga ghorofa mbili, lakini mwenyewe akaamua kujenga ghorofa tano.Uokoaji bado unaendelea na watu wengine 124 walikuwa wameokolewa wakiwa hai hadi kufikia jana Jumapili.
A photo taken and released by Nigeria's National Emergency Management Agency (NEMA) on September 12, 2014 shows emergency workers transporting a man after he was pulled out from the rubble of The Synagogue Church of All Nations
Mmoja wa majeruhi waliookolewa kwenye kanisa hilo akiwa hajitambui.
Jengo hilo liko katika eneo la Ikotun magharibi mwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Lagos. 
 

RASMI: SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU UHALALI WA BUNGE LA KATIBA KUENDELEA!


Serikali ya Tanzania imetoa tamko juu ya kuendelea kwa bunge maalumu la katiba na kusema kuwa lipo kwa mujibu wa sheria hivyo wananchi wasidanganyike na maneno ya wanasiasa juu ya uhalali wa Bunge hilo katika kuunda rasimu ya Katiba.
Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Dkt. Asha-rose Migiro.
Akizungumza Bungeni jana Mjini Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria nchini Mh, Dkt. Asha-rose Migiro amesema Serikali haitavumilia upotoshaji wa wanasiasa na kuwataka wananchi wasishawishiwe kufanya vurugu na kuandamana na kusema pindipo atakaefanya hivyo basi Sheria itakuachukua mkondo wake.
 JE, UMEPTITIA MAGAZETI YA LEO J4?!
Dkt, Migiro amesema kuwa Mahakama imeridhia kuendelea na mchakato huo kama ulivyopangwa na kuwataka wananchi wasubiri Katiba itakayopendekezwa na kuongeza kuwa Vyama vya siasa vitakaa tena chini ya kituo cha Demokrasia Tanzania ili kupata maridhiano juu ya katiba hiyo.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta ametangaza kuwa zoezi la kuipigia kura rasimu ya Katiba litafanyika kuanzia tarehe 29 mwezi huu hadi Oktoba 2 ama 3 ili kupata Katiba iliyopendekezwa.

Akihairisha kikao cha Bunge hilo jana usiku Sitta amesema kabla ya zoezi hilo la kupiga kura itafanyika kazi ya wajumbe kupitia na kuidhinisha Ibara zote karibu 300 kwa utaratibu utakaopangwa.

Amesema kwa hali ilivyo itachukua siku 300 kupitia na kuridhia Ibara zote kwa kumhoji mjumbe mmoja mmoja kwa wajumbe wote 460 wakati wamepewa siku 60 tu hivyo kamati ya uongozi itabidi ije na utaratibu utakaokoa muda.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA TATU WA AFRIKA KUHUSU MASUALA YA USIMAMIZI WA KODI.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi mkutano mkuu wa tatu wa Afrika kuhusu masuala ya usimamizi wakodi uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam, leo Septemba 16, 2014.
 Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufungua rasmi mkutano mkuu wa tatu wa Afrika kuhusu masuala ya usimamizi wakodi uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (wa pili kulia) wakiwa meza kuu na baadhi ya viongozi wa TRA wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa tatu wa Afrika kuhusu masuala ya usimamizi wakodi uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam, leo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, waliohudhuria mkutano huo, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam, leo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, waliohudhuria mkutano huo, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam, leo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, waliohudhuria mkutano huo, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa TRA, baada ya kufungua mkutano mkuu wa wa tatu wa Afrika kuhusu masuala ya usimamizi wakodi uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam, leo. 

MFUKO WA PENSHENI WA PSPF WATIMIZA MIAKA 15 TOKEA KUANZISHWA KWAKE.


 Mkurugenzi wa Idara ya Habari- Maelezo, Bw Assah Mwambene akizungumza jambo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari na Viongozi wa Mfuko wa Hifadhi wa Pensheni wa PSPF mapema leo katika Ukumbi wa JB Belmonte, Jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa pensheni wa PSPF, Bw Adam Mayingu akizungumzia mafanikio ya mfuko wa PSPF katika kipindi cha Miaka 15 tokea kuanzishwa kwake katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo katika Ukumbi wa JB Belmonte Jijini Dar.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mh Adam Mayingu (kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo, Mh Assah Mwambene leo katika Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo wakati Mkurugenzi mkuu wa PSPF alipokuwa akizungumzia mafanikio ya PSPF ndani ya miaka 15 tokea kuanzishwa Kwake.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF na wanahabari waliohudhuria mkutano kati ya Waandishi wa habari na Mfuko wa Pensheni wa PSPF uliolenga kuelezea mafanikio ya mfuko huo ndani ya Miaka 15 tokea kuanzishwa kwake.
Mmoja wa Waandishi wa Habari akiuliza swali wakati wa Mkutano kati ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF na waandishi wa habari uliofanyika leo Katika ukumbi wa JB Belmonte, Jijini Dar Es salaam, Mkutano huo ulilenga kueleza mafanikio yaliyopatikana kwa Kipindi cha Miaka 15 tokea kuanzishwa kwa mfuko huo wa PSPF.

NEWS # MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI DAR ACHINJWA NA KUTUPWA KICHAKANI:


Mwili wa Melasi Lutebula Ndabi ukiwa umetupwa baada ya kuchinjwa.

 Mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina la Melasi Lutebula Ndabi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa  Kamati ya Ulinzi  na Usalama Mtaa wa Muhimbili 2, Kata ya Pemba, Wilaya ya Temeke jijini Dar, ameuawa kwa kuchinjwa na watu  wanaodaiwa kufika kwake kwa ajili ya kukodi shamba la kulima matikiti.Habari zinadai kuwa, marehemu mbali na kuwa mfanyabishara na kiongozi katika eneo hilo, pia alikuwa akijishughulisha kwa kilimo na ufugaji, kazi ambazo amekuwa akizifanya tangu afike  katika eneo  hilo mwaka 2005.

Akizungumzamke wa marehemu aitwaye Rehema Shaban (pichani),  alisema siku za nyuma kuna watu watatu walifika nyumbani hapo wakihitaji kukodi shamba kwa ajili ya kulima matikiti.

Watu hao ambao inadaiwa si wakazi wa eneo  hilo na wala hawajulikani walisema wanatokea Kijiji cha Lisu wilayani  Nzega, Mkoa wa  Tabora  walielekezwa  kwa  marehemu huyo.

Ilielezwa kuwa, kwa mara ya kwanza watu hao walifika  nyumbani kwa marehemu Septemba 5, mwaka huu baada ya mazungumzo ya kina, marehemu aliwaonesha eneo la ekari tatu

.

                 Mke na watoto wa Lutebula Ndabi wakiwa na uzuni.

 Mke huyo alisema hata yeye tukio hilo limemchanganya kwani aliamini wale vijana walikuwa ni watafutaji na ndiyo maana mumewe aliwapa shamba, kumbe walikuja kutafuta roho ya mume wake.

Alisema tangu watu hao wafike, siku tatu mbele ndipo walipogundua mumewe amechinjwa na vijana hao watatu hawajaonekana tena. Alisema siku ya tukio, mume wake aliondoka na vijana hao kwa madai wanakwenda kumtolea pesa kwenye mtandao wa simu ili wamlipe kwa ajili ya shamba hilo.

Kwa mujibu wa Rehema, watoto wake wawili (mmoja miaka 7, mwingine 4) ndiyo waliogundua mwili wa marehemu baba yao akiwa amechinjwa walipokwenda kuchunga ng’ombe.

 
Jeneza la marehemu, Lutebula Ndabi.

 “Nikiwa bado najiuliza aliko mume wangu, mara mtoto wangu Ashura (mkubwa) akaja anakimbia huku ana wasiwasi, akasema, mama nimeona shati la baba, ndala na mguu wake. Ndipo tukaenda huko na watu lakini Ashura  alikataa kufika kwa awamu nyingine.

“Tulipofika tuliukuta mwili wa mume wangu. Niliona amekatwa kichwani na pembeni kulikuwa na panga. Baada ya hapo nilihisi mwili ukiishiwa nguvu, sikujua nini kilichoendelea,” alisema mwanamke huyo.

Mpaka sasa Jeshi la Polisi Wilaya ya Temeke linawashikilia  watu watatu, wawili wakiwa ni wale waliowakaribisha wale vijana huku mmoja wao akiwa mwenyeji wa kijiji cha jirani, alikamatwa kutokana na maelezo ya bahasha iliyokutwa kando ya mwili wa marehemu ikisema ‘kumbuka yaliyotokea mwaka 2013’ ambapo baadhi ya watu walisema mtuhumiwa huyo aliwahi kutofautiana na marehemu.

NEWS # MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI KESI YA KUPINGA BUNGE MAALUMU LA KATIBA


MAHAKAMA Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam jana imetupilia mbali maombi ya pingamizi la awali la kusimamisha  Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma, iliyofunguliwa na  Mwandishi wa Habari Said Kubenea, kwa kuwa wametumia kifungu cha sheria kisicho sahihi.

Kadhalika, mahakama hiyo imetupilia mbali pingamizi hilo la awali, kwa kuwa mlalamikaji ametumia kifungu cha sheria namba 2 kidogo cha (2) (JALA) ambacho hakina mamlaka ya kufungua maombi hayo mahakamani.

Uamuzi huo ulitolewa chini ya jopo lililoketi la majaji watatu, wakiongozwa na Mwenyekiti Mh.Jaji Augustino Mwarija, Dr. Fauz Twaib na Aloyisius Mujuluzi.

Jopo hilo lilisema mahakama imetupilia mbali pingamizi hilo la awali kwa sababu halina mashiko ya kisheria.
Upande wa mlalamikiwa uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Gabriel Malata na mlalamikaji Peter Kibatala.

Awali,  Mwanasehria Mkuu (AG) kupitia Naibu Mwanasheria Mkuu, George Masaju kuiomba mahakama hiyo kutupilia mbali pingamizi hilo kwa kuwa maombi yake ni batili kisheria na hayawezi kuthibitishwa mahakamani, hivyo yatupiliwe mbali.

Katika pingamizi hilo lililoambatana na hati ya kiapo, AG kupitia naibu wake, amedai kuwa maombi hayo ya mlalamikaji yana dosari ambayo haiwezi kurekebishika kwa kuwa zinahitaji kifungu maalum cha sheria kinachoipa nguvu mahakama ya kuridhia maombi hayo.
Mapema mahakamani hapo, Kubenea aliwasilisha maombi ya pingamizi la awali ya kusimamisha Bunge hilo kwa muda yaliyopewa usajili wa namba 29 ya mwaka 2014, pamoja na maombi ya msingi ya tafsiri ya mamlaka ya Bunge yote yalifunguliwa mahakamani hapo jana chini ya Hati ya Dharura.

Katika kesi ya msingi iliyopewa usajili  namba 28 ya mwaka 2014, Kubenea anaiomba mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya Mamlaka ya Bunge la Katiba chini ya  vifungu vya 25 (1) na 25 (2) vya Sheria ya Marekebisho ya Katiba namba Namba 83 ya mwaka  2011.

Pamoja na mambo mengine katika kesi hiyo ya kuomba tafsiri ya mamlaka ya Bunge  hilo, pia Kubenea amewasilisha maombi mahakamani hapo akiiomba mahakama itoe zuio la muda la kusimamisha Bunge hilo ili kusubiri uamuzi wa maombi ya tafsiri hiyo.

FREEMAN MBOWE ASHINDA NAFASI YA UENYEKITI CHADEMA


Freeman Mbowe akiwasalimia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema.
Freeman Mbowe ameshinda tena nafasi ya Uenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa baada ya kupata jumla ya kura 789 huku mpinzani wake Ngambaranyela Mongatero akipata kura 20.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema wakifuatilia mkutano huo.
Mbowe ameshinda nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara imechukuliwa na Prof. Abdallah Safari aliyepata kura 775 za ndiyo huku kura za hapana zikiwa 34 baada ya kuwa mgombea asiye na mpinzani.
Makamu Mwenyekiti Zanzibar ni Said Issa Mohamed aliyepata jumla ya kura 645 huku mpinzani wake Hamad Mussa Yusuph akiambulia kura 163.

AZAM FC YAKUBALI KICHAPO CHA GOLI 3 KWA 0 DHIDI YA YANGA


Mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngasa, kushoto akimtoka  beki wa Azam FC, Erasto Nyoni katika mchezo wa Ngao ya Hisani uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanya imeshinda 3-0.
 
Kikosi kamili cha Yanga kilichoifunga Azam FC 3-0 katika mchezo wa Ngao ya Hisani 

NSSF YADHAMINI MPAMBANO W SIMBA FC NA NDANDA FC


Timu zikiingia uwanjaniTimu zikiingia uwanjani
washabiki
Baadhi ya mashabiki wakishudia mchezo huo.Kaimu Meneja wa NSSF Mkoa Mtwara, Bw. Daniel Lyimo akizungumza na waandishi wa habari juu ya shirika la NSSF kuandikisha Wakulima ili waweze kupata mafao ya NSSF yakiwemo, matibabu bure kwa mwanachama na wategemezi, mikopo ya pembejeo na vifaa vya kilimo, mafao ya kuumia kazini na pension ya uzeeni. Kaimu Meneja wa NSSF Mkoa Mtwara, Bw. Daniel Lyimo akizungumza na waandishi wa habari juu ya shirika la NSSF kuandikisha Wakulima ili waweze kupata mafao ya NSSF yakiwemo, matibabu bure kwa mwanachama na wategemezi, mikopo ya pembejeo na vifaa vya kilimo, mafao ya kuumia kazini na pension ya uzeeni
.Kikosi cha Ndanda FC katika picha ya pamoja kabla ya kufanyika mchezo wa kirafiki uliodhaminiwa na NSSF kupitia kampeni yake ya wakulima scheme.  
Kikosi cha Ndanda FC katika picha ya pamoja kabla ya kufanyika mchezo wa kirafiki uliodhaminiwa na NSSF kupitia kampeni yake ya wakulima scheme.Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali mstaafu, Joseph Simbakalia akikagua timu ya Simba wakati wa mchezo wa kirafiki na timu ya Ndanda FC uliofanyika kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali mstaafu, Joseph Simbakalia akikagua timu ya Simba wakati wa mchezo wa kirafiki na timu ya Ndanda FC uliofanyika kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini MtwaraKikosi cha Simba FC katika picha ya pamoja kabla ya kufanyika mchezo wa kirafiki uliodhaminiwa na NSSF kupitia kampeni yake ya wakulima scheme. Kikosi cha Simba FC katika picha ya pamoja kabla ya kufanyika mchezo wa kirafiki uliodhaminiwa na NSSF kupitia kampeni yake ya wakulima scheme

21
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kupitia mpango wake wa wakulima Scheme imedhamini mechi kati ya Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam na Timu ya Ndanda FC ya Mtwara. Akizungumzia mchezo huo uliofanyika jana mkoani Mtwara, Meneja Kiongozi, Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume alisema mpango huo umelenga kuwasaidia wakulima mkoani humo.

Alisema kupitia mpango huo NSSF imejikita kuandikisha Wakulima ili waweze kupata mafao yakiwemo, matibabu bure kwa mwanachama na wategemezi, mikopo ya pembejeo na vifaa vya kilimo. Aliongeza kuwa mpango huo unatoa mafao ya kuumia kazini, pamoja na pension ya uzeenipindi watakapofikisha umri wa miaka 55.
"..Hii ni kuisaidia serikali kujinasua na mzigo wa kulea wazee kwa kuwaingiza mapema kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF ili waanze kujiwekea kwa maisha yao ya baadae," alisema Bi. Chiume.

Mpango huo unamwezesha mkulima kupitia chama cha wakulima AMCOS kuweza kupata mkopo na taarifa muhimu kuhusu wakulima,wakulima wanachama wa nssf wanajiunga bure na kuchangia kuazia shilingi 20,000 na kuendelea. Akifafanua zaidi alisema wakulima mbalimbali mkoani Kigoma na wilayani Mbinga tayari wamenufaika kwa kupata mikopo zaidi ya bilioni 3.7 tangu mpango huu wa Wakulima Scheme uanzishwe.

"...Wakulima wote wanakaribishwa kutumia fursa hii kujiunga na NSSF."

Aidha mpangu huu unampa mkulima nafasi pekee ya kulipa kwa msimu wa mavuno yaani msimu wa mavuno anaweza nlipia kwa mwaka mzima,miezi anayoweza lipa .lakini pia wakulima wanaweza lipia baada miezi iliyopitilizia bila malipo msimu wa mavuno.
NSSF likiwa ni shirika pekee lenye kuwapa huduma ya afya bure wanachama na kuwawezesha wanachama kutoyumba kiuchumi kwa sababu za gharama za matibabu kwenye familia.

NSSF linawahudumia familia ya mwanachama kwa kuwapa matibabu bure watoto wanne na mke au mume. Alieleza kuwa matibabu haya wanapata pia wakulima wanaojiandikisha kwenye mpango huu kwa SHIB ya NSSF na kuwawezesha kuokoa vipato vyao ambavyo vingetumia kwenye matibabu. NSSF mkoa wa mtwara unampango wa kuandikisha wanachama zaidi ya 63,000 kutoka kwa wakulima wa vijiji na wilaya zote mkoani Mtwara na Lindi ambazo ni Tandahimba, Nanyumbu, Masasi, Nachingwea, Newala, Mtwara Vijijini ambao wengi ni wakulima wa zao korosho.

aidha wakuliwa wataweza kupata mikopo kupitia SACCOS zao na kuwawezesha kununua mbolea,madawa ya kuulia wadudu, pembejeo, zana mbali mbali za kilimo ili kujiinua kiuchumi kupitia NSSF SACCOS Loans, Ofisi ya NSSF Mkoa wa mtwara umeshatoa jumla ya shilingi Bilion 1.75 kwa SACCOS zilizokidhi vigezo na kuwainua kimaisha wajasilia mali, wakulima na wafanyakazikwenye mkoa huo. Mpango huu wa Wakulima Scheme ulizinduliwa rasmi na Rais Jakaya Kikwete Mwezi Mei mwaka huu.Mr Dalali akitoa shukran kwa waandalizi wa ndanda day na wadhamin wa mpambano ambao ni NSSF kwa kuwezesha timu hizo kupambana kwenye mechi ya kirafiki baina ya timu hizo.Kwa mara ya mwisho timu ya mtwara kucheza mpira ilikuwa ni miaka kumi iliyopitaBw. Dalali akitoa shukran kwa waandalizi wa ndanda day na wadhamin wa mpambano ambao ni NSSF kwa kuwezesha timu hizo kupambana kwenye mechi ya kirafiki baina ya timu hizo.Kwa mara ya mwisho timu ya Mtwara kucheza mpira ilikuwa ni miaka kumi iliyopita

DUNIA IMEKWISHA: MWANAMKE AWABAKA WATOTO WA KIUME WAWILI , AWALAZIMISHA WAMUINGILIE KIMWILI USIKU WA MANANE!

Vitendo vya ngono nchini Uganda vimesababisha maambukizi makubwa ya Ukimwi. Mwanamke wa miaka 37, aliyefahamika kwa jina moja la Adong anashikiliwa na Polisi huko mjini Gulu nchini Uganda kwa kosa la kuwaingilia watoto wawili wa kiume wenye umri wa miaka 14 na 15 ambao vilevile ni wenye undugu na yeye!
Aliwaingilia watoto hao alipokwenda kuwatembelea wazazi wao na ndipo usiku akanyata na kuingia chumbani mwao na kuwashawishi bila aibu wamle uroda! Ilitokea baba yao aliwasikia wanae wakijadili juu ya "utamu" na ndipo akaiarifu polis nao hawakuzubaa na kumtia ndani. Akitiwa hatiani anaweza kufungwa miaka 7 au maisha! Mambo hayo! Taarifa zaidi tutawaletea tukizipata...!

TABORA WAPOKE ASKARI 75


 Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP - Suzan Kaganda amewapokea askari 75 wa awamu ya kwanza walioripoti mkoani Tabora wakitokea Chuo Cha Polisi Moshi baada ya kuhitimu  mafunzo ya awali ya Polisi. Kamanda aliwataka askari hao kufanya kazi kwa weledi katika utendaji kazi pamoja na Nidhamu ya hali ya juu.  
 Askari wapya wakimsikiliza Afande Suzan Kaganda alipowapokea  mkoani Tabora wakitokea Chuo Cha Polisi Moshi 
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP - Suzan Kaganda amewapokea askari 75 wa awamu ya kwanza walioripoti mkoani Tabora wakitokea Chuo Cha Polisi Moshi. Picha na  Fakih Abdul - mwandisi wa Polisi Tabora.



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 16/09/2014.

Ndugu waandishi wa habari katika mkoa wetu wa Tabora kumetokea matukio yafuatayo:-

KUPATIKANA NA MADAWA YADHANIWAYO KUWA YA KULEVYA NA
PIKIPIKI ZA WIZIHuko  wilaya ya Igunga wamekamatwa watuhumiwa watatu:-
1.  WILLY s/o MASHILINGI, 22 yrs, Msukuma, mkulima na mkazi wa Kahama.
2.  SITA

s/o JILUNGA, 38 yrs, msukuma, mkulima na mkazi wa Nzega.
3.  YUSUPH

s/o MIHAYO, 24yrs, msukuma, mkulima wa mtaa wa Stoo.
4.  GILALA

s/o BULEBA, 35yrs, msukuma, mkulima, mkazi wa Igunga mjini.

wakiwa na madawa ya
kulevya wanayoyatumiwa kulewesha watu kisha kuwapora pikipiki. Walipohojiwa
walikiri kuhusika na matukio mbali mbali ya wizi wa pikipiki na kuonesha
pikipiki mbili zenye namba T 892 CXB, T 522 CQZ, T.914 BUW na T.812 CGU
zote aina ya SANLG ambazo walizipora huko Puge wilaya

ya Nzega. Juhudi za kuwatafuta wamiliki halari wa pikipiki hizo zinaendelea.
Watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya

upelelezi kukamilika.
KUPATIKANA NA
BHANGI GUNIA MBILI:
Huko wilaya ya Nzega amekamatwa mtuhumiwa MABULA s/o
EZEKIEL, 23yrs, Msukuma, mkulima na mkazi wa Ibologero akiwa na bhangi gunia
mbili. Mtuhumiwa baada ya mahojiano amekiri kuwa ni muuzaji na mtumiaji wa

bhangi.upelelezi kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani
AJALI YA GARI KUGONGANA NA PIKIPIKI YA MATAIRI MATATU
NA KUSABABISHA VIFO:
Huko kijiji cha Ndono barabara ya Urambo
gari no. T607 BNV scania lorry iliyokuwa ikiendeshwa na FUMBA s/o JUMA, 45yrs,
Msambaa, mkazi wa DSM iligongana na pikipiki ya kubeba mizigo (Guta) REG no.
T153 CWJ SUNLG na kusababisha vifo vya watu watatu papo hapo ambao ni MAHONA
S/O MUSA WANDEZI, 30yrs, Msukuma, mkazi wa Intika dereva wa pikipiki, HIBHA S/O
LUCAS, 30yrs, msukuma, mkazi wa Ndono, MABULA S/O MATONGO, 35yrs, msukuma,

mkazi wa Intika chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa pikipiki.
AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA
KIFO:
Huko maeneo ya barabara kuu Nzega – Igunga katika kijiji cha Kitangili GARI
T.300 CWB Toyota Hiace ikiendeshwa na STANSLAUS S/O JOAKIM, 33yrs, Mchaga,
mkazi wa Nzega ilimgonga mtembea kwa miguu JOKU D/O MBEGESHEN, 32yrs, Msukuma, M/biashara,
mkazi wa Singida na kufa papo hapo. Chanzo cha ajali ni uzembe wa mtembea kwa

miguu kuvuka barabara bila tahadhali. Dereva amekamatwa kwa mahojiano zaidi.
Jeshi la Polisi linazidi kutoa wito kwa
wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi lao ili kukomesha na kutokomeza

vitendo vyote vya uhalifu na kuwafichua wahalifu, pia  watumiaji wa barabara wafuate  sheria za usalama barabarani.

SUZAN S. KAGANDA –ACP.


KAMANDA WA POLISI MKOA WA TABORA.