YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Thursday 18 September 2014

POLISI WAIMALISHA ULINZI MANISPAA YA DODOMA BAADA YA KUZUIA MAANDAMANO YA CHADEMA


 Jeshi la polisi limeimalisha ulinzi katika maeneo yote ambayo yalitajwa na chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa ndiyo watapitia wakiandamana kwenda kwenda Bungeni kuanzia saa 4 asubuhi ya leo.(Picha na John Banda wa Pamoja Blog)
Polisi wakiwa wamefunga kamba kati barabara ya mzunguko ya stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani na chuo cha biashara CBE  kwaajili ya kuwazuia waandamanaji hao waliopanga kwenda Bungeni
 Polisi wapanda farasi wakiimalisha ulinzi katika viwanja vya nyerere Squere ambapo Chadema wamepanga kuanzia maandamano kuelekea bungeni.
 Askali polisi wakiwafanya mawasiliano kwenye gari lao ambalo lilikuwa limepakia mbwa kwa ajili ya kuimalisha ulinzi katika viwanja vya Nyerere Dodoma kwa ajili ya kuwazuia waandamanaji wa Chadema walipanga kuandamana kwenda Bungeni.
Kwa Hisani ya Pamoja Pure Blog

SHUHUDIA MSHIKEMSHIKE WA POLISI NA WAFUASI WA CHADEMA DAR MUDA HUU


Jeshi la polisi jijini Dar es Salaam limetumia mbwa na virungu kuwatanyama mamia ya wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Manendeleo Chadema ambao walifurika Makao Makuu ya Jeshi hilo kwa lengo la kumsindikiza Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, ambaye aliitwa kwa mahojiano.

Name:  c2.jpg
Views: 0
Size:  44.7 KB




Name:  c1.jpg
Views: 0
Size:  44.2 KB

MTOTO ALIYEZAMIA KWEYE NDEGE, ATOWEKA TENA NYUMBANI! SOMA ZAIDI HAPA!


Mtoto Happiness Rioba(10) aliyedaiwa kuzamia kwenye ndege kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar bila kugundulika, ametoweka tena nyumbani kwao baada ya kukutanishwa na mama yake mzazi Sara Zefhania. 
Happiness ambaye ni mkazi wa eneo la Mkokozi, Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani inadaiwa ametoweka katika mazingira ya kutatanisha. 
Akizungumza na Mwananchi jana, Sara alisema mwanawe alitoweka jana saa sita mchana na kutokomea kusikojulikana.


Alisema asubuhi mtoto wake aliamka salama bila tatizo lolote na muda wote walikuwa pamoja kwa kuwa alikuwa na wageni kutoka kituo cha televisheni cha ITV, waliomuahadi kumtembelea nyumbani kwa lengo la kumuona Happines
“Aliamka vizuri tu na muda wote alikuwapo nyumbani, lakini ilipofika saa sita mchana, nilipigiwa simu na waandishi wa habari wa ITV kuwa nikawachukue katika kituo cha daladala... kabla sijaondoka nilimwambia mwanangu nakwenda kupokea wageni, lakini niporejea nyumbani na wageni hatukumkuta,” 

alisema Sara.
Alisema baada ya kumkosa alianza kumtafuta akishirikiana na waandishi hao pamoja na majirani, lakini hawakufanikiwa kumpata ndipo alipotoa taarifa kwa mjumbe wa Serikali za Mitaa na kuwataarifu ndugu, jamaa na marafiki.

Aidha, aliongeza mwanawe alipokuwa Zanzibar alifanya mambo ya ajabu likiwamo kuongea na paka, kula chakula kwa kutumia mkono wa kushoto, kutokuongea na watu pamoja na kutoweka katika mazingira ya kutatanisha.

UNAAMBIWA JAJI ALIYETOA MAAMUZI KATIKA KESI YA MWANARIADHA OSCAR PISTORIUS ATISHIWA KUUWAWA



Mashirika ya kisheria nchini Afrika Kusini, yameelezea wasiwasi kuhusu vitisho dhidi ya jaji aliyetoa uamuzi katika kesi inayomkabili mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius.

Jaji Thokozile Masipa alimpata Pistorius na hatia ya kuua bila kukusudia wala sio mauaji ya kusudi.

Jaji huyo amekuwa akikosolewa tangu kutoa uamuzi wake kuwa Pistorius alimuua mpenzi wake kwa bahati mbaya.

Baadhi ya matamshi yaliyotolewa ni ya chuki , kumlimbikizia lawama na hata kwenda kinyume na mahakama.

Bi Masipa amewekewa ulinzi tangu kutoa uamuzi wake, kwa mujibu wa jarida la City Press.

Maafisa wa polisi wamekuwa wakishika doria nje ya nyumba yake na pia wamekuwa wakimsindikiza kila anapokwenda.

Pistorius alikana kosa la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa kukusudia.

Wataalamu wa maswala ya kisheria wamekosoa uamuzi wa jaji Masipa ambaye alichukua wadhifa wake mwaka 1998 na kuwa mwanamke wa pili mweusi kuwahi kushikilia wadhifa huo.

Taarifa ya wanasheria hao ilisema kuwa uamuzi wa jaji Masipa ilikuwa sawa kuambatana na sheria na pia kulingana na ushahidi uliotolewa Masipa.

Viongozi wa mashitaka walilaani uamuzi wa jaji Masipa wakisema kuwa Pistorius alipaswa kupataikana na hatia ya kumuua mpenzi wake kwa kukusudia.

EXCLUSIVE: CHRIS BROWN KUTUA BONGO KWENYE SERENGET FIESTA


Habari zilizopo chini ya kapeti ambazo bado hazidhibitishwa ni kwamba yale nyota wa R&B anayedwa na kukubalika na wengi ambapo umaarufu wake umeweza kuongezeka mara dufu kutokana na kutoka kimapenzi na Rihanna ... Ambapo wabongo wameweza kufananisha mapenzi ya Diamond na Wema Sepetu ni kama Chris na Rihanna.. Sasa unaambiwa Mazungumzo ya mwisho ya kukubaliana ndio yanafanyika na pia kama watakubaliana vizuri Chris Brown kutua Bongo bila utata hiyo .. Na kiingilio kikiwa sh elfu 50 wala msishangae

BASI LA SHAKILA LATUMBUKIA MTO PANGANI MKOANI TANGA


 
Basi la Shakila likiwa limetumbukia katika Mto Pangani wakati likiwa kwenye kivuko cha MV Pangani. 

CHADEMA WATANGAZA KUMSINDIKIZA MBOWE KESHO HADI MAKAO MAKUU YA POLISI ,WANACHAMA NAO WATAKIWA KUJITOKEZA


MWANASHERIA MKUU WA CHADEMA AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI MUDA HUU

 Chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA leo kimetangaza kuwa mwenyekiti wao keshoi ataenda polisi makao makuu kuitikia wito wa jeshi hilo ambao ulikuja kwa barua ukimhitaji mwenyekiti huyo kufika makao makuu ya jeshi hilo.

Kauli hiyo imetangazwa muda huu makao makuu ya chama hicho na  wanasheria mkuu wa chama hicho mbunge TUNDU LISSU wakati akizungumzia wito wa jeshi la polisi kumhitaji mwenyekiti wao kwa kile ambacho ameadi kuwa hakijawekwa wazi wanamwitia nini.

"Tumepokea barua ya jeshi la polisi makao makuu wakimtaka mwenyekiti wetu kufika makao makuu ya polisi kwa maelezo,kamati kuu ya chama imeridhia mwenyekiti aende ila hawezi kwenda mwenyewe hivyo wanasheria wote wa chama walioko mkoani Dar es salaam watamsindikiza kwa ajili ya kujua mwenyekiti wetu ameitiwa nini.hivyo tunaomba wanasheria wote wa chama kesho tukutane polisi makao makuu saa tano kwa ajili ya kumsindikiza. 
Naibu katibu mkuu wa chama  JOHN MNYIKA akizungumza 
Aidha naibu katibu mkuu wa chama  hicho mh JOHN MNYIKA NAYE naye amewataka wananchi na wapenzi wa chama hicho kujitokeza kesho kumsindikiza mwenyekiti wao kwa ajili ya kusikiliza kile ambacho mwenyekiti wao ameitiwa nini na jeshi la polisi.

KAZI IMEANZA: JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA LAZUIA MAANDAMANO YALIYOPANGWA NA CHADEMA



Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) EMMANUEL G. LUKULA

Na Sylvester Onesmo wa Jeshi l
a Polisi Mkoa wa Dodoma.Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limetoa tamko la kuzuia maandamano ya Chama cha CHADEMA hapo tarehe 18/09/2014 na kuwataka wananchi kuyapuuza.
Akiongea na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi wa Polisi EMMANUEL G. LUKULA (ACP) alisema kuwa; Kufuatia Viongozi wa CHADEMA kutaka kufanya maandamano kuelekea viwanja vya Ofisi za Bunge Mkoani Dodoma kwa ajili ya kupinga Bunge la Katiba siku ya tarehe 18/09/2014 linaloendelea, kuwa maandamano hayo ni batili na akiwataka wananchi wakazi wa Dodoma kuyapuuza kwa kuwa yanakiuka Sheria iliyoliweka Bunge hilo.

Kamanda LUKULA  alitaja sababu za msingi za kuzuia maandamano hayo kuwa ni:-
1. Siku ya maandamano ya tarehe 18/09/2014 ni siku ya kazi ikiwa ni pamoja na muda wa maandamano hayo ni masaa ya kazi saa 04:00 asubuhi hadi saa 06:00 mchana yataathili ufanisi wa watu waliopo makazini/maofisini.
2. Bunge maalumu la Katiba linaloendelea kwa sasa lipo Kisheria na hakuna tamko lolote lililotolewa na Mahakama yoyote kulisitisha, hivyo moja ya kazi ya Jeshi la Polisi ni kulinda Sheria na wale wanaofuata sheria. Hivyo kufanya maandamano yanayopinga Bunge la Katiba ni kukiuka Sheria iliyoliweka Bunge hilo.
3. Kuna kesi Mahakamani ya kupinga Bunge hilo kuendelea, hadi sasa shauri hilo linaendelea Mahakamani. Hivyo kwa CHADEMA kuandamana ni kuingilia Uhuru wa Mahakama.
4. Baadhi ya Wilaya barua za kufanya maandamano zimechelewa kufika kwa Wakuu wa Polisi Wilaya kabla ya saa 24 kisheria.

Aidha Kamanda Lukula  alitoa wito kwa wananchi wa Dodoma kupuuza maandamano yoyote ya kupinga uwepo wa Bunge la Katiba kwani ni batili. Aidha aliwashauri viongozi wa CHADEMA Mkoa na Wilaya za Dodoma wayasitishe maandamano hayo na wasipo ridhika, wakate rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa maelekezo zaidi.

Tuesday 16 September 2014

BREAKING NEWZZ: WALIOKUFA KWENYE KANISA LA TB JOSHUA LILILOPOROMOKA WAFIKIA 50..!

Idadi ya watu waliokufa kwenye ghorofa la makao makuu ya Kanisa la SCOAN (Synagogue Church of All Nations) la Nabii TB Joshua wamefikia 50.
Jengo hilo la ghorofa tano ambalo ni makao makuu ya kanisa na nyumba ya kulala wageni liliporomoka Jumamosi  wakati ujenzi ukiendelea.Hadi kufikia jana Jumapili jumla ya watu 41 walikuwa wameripotiwa kufa, lakini maiti nyingine tisa zimeongezeka leo hii.Inaelezwa kwamba, mhubiri huyo wa kimataifa alipewa kibali cha kujenga ghorofa mbili, lakini mwenyewe akaamua kujenga ghorofa tano.Uokoaji bado unaendelea na watu wengine 124 walikuwa wameokolewa wakiwa hai hadi kufikia jana Jumapili.
A photo taken and released by Nigeria's National Emergency Management Agency (NEMA) on September 12, 2014 shows emergency workers transporting a man after he was pulled out from the rubble of The Synagogue Church of All Nations
Mmoja wa majeruhi waliookolewa kwenye kanisa hilo akiwa hajitambui.
Jengo hilo liko katika eneo la Ikotun magharibi mwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Lagos. 
 

RASMI: SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU UHALALI WA BUNGE LA KATIBA KUENDELEA!


Serikali ya Tanzania imetoa tamko juu ya kuendelea kwa bunge maalumu la katiba na kusema kuwa lipo kwa mujibu wa sheria hivyo wananchi wasidanganyike na maneno ya wanasiasa juu ya uhalali wa Bunge hilo katika kuunda rasimu ya Katiba.
Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Dkt. Asha-rose Migiro.
Akizungumza Bungeni jana Mjini Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria nchini Mh, Dkt. Asha-rose Migiro amesema Serikali haitavumilia upotoshaji wa wanasiasa na kuwataka wananchi wasishawishiwe kufanya vurugu na kuandamana na kusema pindipo atakaefanya hivyo basi Sheria itakuachukua mkondo wake.
 JE, UMEPTITIA MAGAZETI YA LEO J4?!
Dkt, Migiro amesema kuwa Mahakama imeridhia kuendelea na mchakato huo kama ulivyopangwa na kuwataka wananchi wasubiri Katiba itakayopendekezwa na kuongeza kuwa Vyama vya siasa vitakaa tena chini ya kituo cha Demokrasia Tanzania ili kupata maridhiano juu ya katiba hiyo.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta ametangaza kuwa zoezi la kuipigia kura rasimu ya Katiba litafanyika kuanzia tarehe 29 mwezi huu hadi Oktoba 2 ama 3 ili kupata Katiba iliyopendekezwa.

Akihairisha kikao cha Bunge hilo jana usiku Sitta amesema kabla ya zoezi hilo la kupiga kura itafanyika kazi ya wajumbe kupitia na kuidhinisha Ibara zote karibu 300 kwa utaratibu utakaopangwa.

Amesema kwa hali ilivyo itachukua siku 300 kupitia na kuridhia Ibara zote kwa kumhoji mjumbe mmoja mmoja kwa wajumbe wote 460 wakati wamepewa siku 60 tu hivyo kamati ya uongozi itabidi ije na utaratibu utakaokoa muda.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA TATU WA AFRIKA KUHUSU MASUALA YA USIMAMIZI WA KODI.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi mkutano mkuu wa tatu wa Afrika kuhusu masuala ya usimamizi wakodi uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam, leo Septemba 16, 2014.
 Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufungua rasmi mkutano mkuu wa tatu wa Afrika kuhusu masuala ya usimamizi wakodi uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (wa pili kulia) wakiwa meza kuu na baadhi ya viongozi wa TRA wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa tatu wa Afrika kuhusu masuala ya usimamizi wakodi uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam, leo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, waliohudhuria mkutano huo, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam, leo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, waliohudhuria mkutano huo, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam, leo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, waliohudhuria mkutano huo, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa TRA, baada ya kufungua mkutano mkuu wa wa tatu wa Afrika kuhusu masuala ya usimamizi wakodi uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam, leo. 

MFUKO WA PENSHENI WA PSPF WATIMIZA MIAKA 15 TOKEA KUANZISHWA KWAKE.


 Mkurugenzi wa Idara ya Habari- Maelezo, Bw Assah Mwambene akizungumza jambo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari na Viongozi wa Mfuko wa Hifadhi wa Pensheni wa PSPF mapema leo katika Ukumbi wa JB Belmonte, Jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa pensheni wa PSPF, Bw Adam Mayingu akizungumzia mafanikio ya mfuko wa PSPF katika kipindi cha Miaka 15 tokea kuanzishwa kwake katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo katika Ukumbi wa JB Belmonte Jijini Dar.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mh Adam Mayingu (kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo, Mh Assah Mwambene leo katika Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo wakati Mkurugenzi mkuu wa PSPF alipokuwa akizungumzia mafanikio ya PSPF ndani ya miaka 15 tokea kuanzishwa Kwake.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF na wanahabari waliohudhuria mkutano kati ya Waandishi wa habari na Mfuko wa Pensheni wa PSPF uliolenga kuelezea mafanikio ya mfuko huo ndani ya Miaka 15 tokea kuanzishwa kwake.
Mmoja wa Waandishi wa Habari akiuliza swali wakati wa Mkutano kati ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF na waandishi wa habari uliofanyika leo Katika ukumbi wa JB Belmonte, Jijini Dar Es salaam, Mkutano huo ulilenga kueleza mafanikio yaliyopatikana kwa Kipindi cha Miaka 15 tokea kuanzishwa kwa mfuko huo wa PSPF.

NEWS # MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI DAR ACHINJWA NA KUTUPWA KICHAKANI:


Mwili wa Melasi Lutebula Ndabi ukiwa umetupwa baada ya kuchinjwa.

 Mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina la Melasi Lutebula Ndabi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa  Kamati ya Ulinzi  na Usalama Mtaa wa Muhimbili 2, Kata ya Pemba, Wilaya ya Temeke jijini Dar, ameuawa kwa kuchinjwa na watu  wanaodaiwa kufika kwake kwa ajili ya kukodi shamba la kulima matikiti.Habari zinadai kuwa, marehemu mbali na kuwa mfanyabishara na kiongozi katika eneo hilo, pia alikuwa akijishughulisha kwa kilimo na ufugaji, kazi ambazo amekuwa akizifanya tangu afike  katika eneo  hilo mwaka 2005.

Akizungumzamke wa marehemu aitwaye Rehema Shaban (pichani),  alisema siku za nyuma kuna watu watatu walifika nyumbani hapo wakihitaji kukodi shamba kwa ajili ya kulima matikiti.

Watu hao ambao inadaiwa si wakazi wa eneo  hilo na wala hawajulikani walisema wanatokea Kijiji cha Lisu wilayani  Nzega, Mkoa wa  Tabora  walielekezwa  kwa  marehemu huyo.

Ilielezwa kuwa, kwa mara ya kwanza watu hao walifika  nyumbani kwa marehemu Septemba 5, mwaka huu baada ya mazungumzo ya kina, marehemu aliwaonesha eneo la ekari tatu

.

                 Mke na watoto wa Lutebula Ndabi wakiwa na uzuni.

 Mke huyo alisema hata yeye tukio hilo limemchanganya kwani aliamini wale vijana walikuwa ni watafutaji na ndiyo maana mumewe aliwapa shamba, kumbe walikuja kutafuta roho ya mume wake.

Alisema tangu watu hao wafike, siku tatu mbele ndipo walipogundua mumewe amechinjwa na vijana hao watatu hawajaonekana tena. Alisema siku ya tukio, mume wake aliondoka na vijana hao kwa madai wanakwenda kumtolea pesa kwenye mtandao wa simu ili wamlipe kwa ajili ya shamba hilo.

Kwa mujibu wa Rehema, watoto wake wawili (mmoja miaka 7, mwingine 4) ndiyo waliogundua mwili wa marehemu baba yao akiwa amechinjwa walipokwenda kuchunga ng’ombe.

 
Jeneza la marehemu, Lutebula Ndabi.

 “Nikiwa bado najiuliza aliko mume wangu, mara mtoto wangu Ashura (mkubwa) akaja anakimbia huku ana wasiwasi, akasema, mama nimeona shati la baba, ndala na mguu wake. Ndipo tukaenda huko na watu lakini Ashura  alikataa kufika kwa awamu nyingine.

“Tulipofika tuliukuta mwili wa mume wangu. Niliona amekatwa kichwani na pembeni kulikuwa na panga. Baada ya hapo nilihisi mwili ukiishiwa nguvu, sikujua nini kilichoendelea,” alisema mwanamke huyo.

Mpaka sasa Jeshi la Polisi Wilaya ya Temeke linawashikilia  watu watatu, wawili wakiwa ni wale waliowakaribisha wale vijana huku mmoja wao akiwa mwenyeji wa kijiji cha jirani, alikamatwa kutokana na maelezo ya bahasha iliyokutwa kando ya mwili wa marehemu ikisema ‘kumbuka yaliyotokea mwaka 2013’ ambapo baadhi ya watu walisema mtuhumiwa huyo aliwahi kutofautiana na marehemu.

NEWS # MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI KESI YA KUPINGA BUNGE MAALUMU LA KATIBA


MAHAKAMA Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam jana imetupilia mbali maombi ya pingamizi la awali la kusimamisha  Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma, iliyofunguliwa na  Mwandishi wa Habari Said Kubenea, kwa kuwa wametumia kifungu cha sheria kisicho sahihi.

Kadhalika, mahakama hiyo imetupilia mbali pingamizi hilo la awali, kwa kuwa mlalamikaji ametumia kifungu cha sheria namba 2 kidogo cha (2) (JALA) ambacho hakina mamlaka ya kufungua maombi hayo mahakamani.

Uamuzi huo ulitolewa chini ya jopo lililoketi la majaji watatu, wakiongozwa na Mwenyekiti Mh.Jaji Augustino Mwarija, Dr. Fauz Twaib na Aloyisius Mujuluzi.

Jopo hilo lilisema mahakama imetupilia mbali pingamizi hilo la awali kwa sababu halina mashiko ya kisheria.
Upande wa mlalamikiwa uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Gabriel Malata na mlalamikaji Peter Kibatala.

Awali,  Mwanasehria Mkuu (AG) kupitia Naibu Mwanasheria Mkuu, George Masaju kuiomba mahakama hiyo kutupilia mbali pingamizi hilo kwa kuwa maombi yake ni batili kisheria na hayawezi kuthibitishwa mahakamani, hivyo yatupiliwe mbali.

Katika pingamizi hilo lililoambatana na hati ya kiapo, AG kupitia naibu wake, amedai kuwa maombi hayo ya mlalamikaji yana dosari ambayo haiwezi kurekebishika kwa kuwa zinahitaji kifungu maalum cha sheria kinachoipa nguvu mahakama ya kuridhia maombi hayo.
Mapema mahakamani hapo, Kubenea aliwasilisha maombi ya pingamizi la awali ya kusimamisha Bunge hilo kwa muda yaliyopewa usajili wa namba 29 ya mwaka 2014, pamoja na maombi ya msingi ya tafsiri ya mamlaka ya Bunge yote yalifunguliwa mahakamani hapo jana chini ya Hati ya Dharura.

Katika kesi ya msingi iliyopewa usajili  namba 28 ya mwaka 2014, Kubenea anaiomba mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya Mamlaka ya Bunge la Katiba chini ya  vifungu vya 25 (1) na 25 (2) vya Sheria ya Marekebisho ya Katiba namba Namba 83 ya mwaka  2011.

Pamoja na mambo mengine katika kesi hiyo ya kuomba tafsiri ya mamlaka ya Bunge  hilo, pia Kubenea amewasilisha maombi mahakamani hapo akiiomba mahakama itoe zuio la muda la kusimamisha Bunge hilo ili kusubiri uamuzi wa maombi ya tafsiri hiyo.

FREEMAN MBOWE ASHINDA NAFASI YA UENYEKITI CHADEMA


Freeman Mbowe akiwasalimia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema.
Freeman Mbowe ameshinda tena nafasi ya Uenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa baada ya kupata jumla ya kura 789 huku mpinzani wake Ngambaranyela Mongatero akipata kura 20.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema wakifuatilia mkutano huo.
Mbowe ameshinda nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara imechukuliwa na Prof. Abdallah Safari aliyepata kura 775 za ndiyo huku kura za hapana zikiwa 34 baada ya kuwa mgombea asiye na mpinzani.
Makamu Mwenyekiti Zanzibar ni Said Issa Mohamed aliyepata jumla ya kura 645 huku mpinzani wake Hamad Mussa Yusuph akiambulia kura 163.