YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday 25 November 2014

MASKINI MSICHANA HUYU AFANYIWA KITU MBAYA KATIKA UCHOCHORO HADI KUPOTEZA FAHAMU



Huyu ni msichana ambaye alikutwa katika uchocholo wa club za bar usiku kati ya galax majira ya asubuhi saa 12 akiwa hajitabuhi 

Baadhi ya wanachi wakijaribu kumuongalia bint huyo akiwa ana fahamu huku akiwa katika kichocholo huku nguo zake zikiwa zimechanwa na watu wasifamika mjini kahama.

Askari polisi wa kituo cha polis kahama thomas munyongo akijaribu kumtabua msichana huyo na bila mafanikio na kuomba msanda katika kituo cha polisi .

Baadhi ya watu wakijaribu kumtambua msichana huyo .
kwa picha zaidi bofya soma zaidi


Baadhi ya wanachi wakimchukuwa binti huyo kwenda kwenye gari ya polisi na kupelekwa hospital ya wilaya ya kahama .

Hakiwa katika gari la polisi huku akiwa hana fahamu

Msichana akiwa hospital ya wilaya kahama daktali akijaribu kumkangua kama yuko hai .

Hivi ndivyo msichana alipochukuliwa kupelekwa hospital ya wilaya kahama kwa uchunguzi zaidi

Baadhi ya askari polisi wamtoa msichana ndani ya gari ya polisi baada ya kumfikisha hospital ya wilaya kahama
.

Hivi karibuni mkuu wa wilaya ya kahama Benson Mpesya alipinga marufuku biashara ya ngono katika wilaya yake. kutokana wasichana wengi kufanya biashara hiyo haramu .
Aidha wilaya kahama imekuwa ni sehemu kubwa kwa wasichana kuingia katika biashara ya ukahaba jambo ambalo linafanya wasichana wengi kubakwa na kutupwa katika mitalo ya maji au manyumba yasio kwisha 

MTOTO ALIYEPEWA KIPIGO CHA KUFA MTU KUTOKA KWA HOUSE GIRL HUKO UGANDA, AFYA YAKE INAENDELEA VIZURI.


Mtoto akiwa hospitali anaendelea na matibabu Habari iliyo 'make' headlines kwa siku ya jana mpaka leo na imetokea kuisisimua jamii na kuiamsha kutoka katika usingizi fulani, habari juu ya mtoto aliyepata kipigo cha kufa mtu kutoka kwa house girl, kwa sababu kesi ipo mahakamani, hatuwezi kujaji sana ila tusubiri mahakama itoe tamko lake japo jamii imeshatoa hukumu kali kwa binti huyo hata tukiwa tunasubiri majibu ya mahakama.

Kutokana na kipigo hicho, mitandao mingi iliripoti kuwa mtoto huyo kapoteza maisha kwa sababu ya kipigo kuwa "heavy" sana. Mtoto yupo salama na anaendelea na matibu.

SAHAU KUHUSU YULE BEKI TATU ALIEMPIGA MTOTO>>>JIONEE JINSI DAWA YA KUDHIBITI MA BEKI TATU ILIVYOPATIKANA



No comments:

AISEE HII HATARI SANA ...UNAAMBIWA HUYU MTOTO ATUMIWA KUMWIBA MTOTO MWENZAKE, AKAMATWA... MTAA WAFUNGWA KWA TIMBWILI LA MTOT



Mtoto mwenye umri wa miaka 8 anayedaiwa kutumika kumwiba mtoto mwenzake. Tukio hilo la kushangaza lililonaswa na Ijumaa Wikienda lilijiri wiki iliyopita mishale ya saa 8:00 mchana maeneo ya Majengo Mapya, Kata ya Kihonda jirani na nyumbani kwa aliyekuwa staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, marehemu Alberth Keneth Mangweha ‘Ngwea’.Hatari! Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 8 (jina linahifadhiwa kimaadili), mkazi wa Kihonda mjini hapa anayesoma darasa la kwanza kwenye Shule ya Msingi Noto Sosario, anadaiwa kutumika kumwiba mtoto mwenzake kisha kukamatwa na kunusurika kuuawa na wananchi wenye hasira zaidi ya 300.

 
Raia wenye hasira kali wakimsubiri kwa hamu mtoto huyo nje ya nyumba aliyohifadhiwa. 
Akizungumza na mwanahabari wetu, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Mama Seleman alisema: “Mtoto huyu alikamatwa kwa jirani yangu, Asha Tembo akidaiwa kutaka kuiba mtoto wa mama huyo kwa njia za kichawi hivyo mama huyo aliamua kupiga kelele na kumuitia mwizi. 

Kamanda akimbana mtoto huyo kwa maswali. “Mtoto alikuwa amevaa nguo nyeusi ndipo umati ukajitokeza na kuanza kumshambulia kwa maneno makali huku wengine wakimpiga vibaya na kutishia kumuua.
Makamanda wa Polisi wakimchukua mtoto huyo kwa usalama zaidi. “Baada ya kuona watu wanazidi, nikaamua kumwokoa na kumficha ndani kwangu.“Nikiwa ndani umati wa watu ulitishia kuchoma nyumba yangu lakini nilifunga milango kisha nikawaita polisi wakaja kumuokoa mtoto huyo.”
Mtoto huyo akichukuliwa kwenye 'Defender' kuelekea kituo cha Polisi.Kwa upande wake, mtoto huyo alisema: “Bibi ndiye huwa ananituma. Kwa sasa niko kwenye ulimwengu wa giza na mateso makubwa.
Naye mama mzazi wa mtoto huyo, Maria Vicent alisema: “Mwanangu nilimzaa akiwa salama lakini tangu atoke Moshi (Kilimanjaro) kwa bibi yake amekuwa wa ajabu hivyo nimepanga kumpeleka kwenye maombi.”

Thursday 20 November 2014

HIVI NDIVYO MWAKYEMBE ALIVYOSULUBIWA


Dodoma. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, jana ilimsulubu Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ikieleza kuwa wizara yake iliingia mkataba wa mradi wa treni za kisasa kutoka Stesheni ya Dar es Salaam hadi Pugu kupitia Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) bila kufuata taratibu.
Kambi hiyo ililieleza Bunge kuwa mkataba huo ulisainiwa baina ya mmiliki wa Kampuni ya M/s Shumoja, Robert Shumake na Shirika la Reli Tanzania huku Waziri Mwakyembe akishuhudia.
Msemaji Mkuu wa kambi hiyo, Ofisi ya Waziri Mkuu,  Uwekezaji na Uwezeshaji, Pauline Gekul alitoa madai hayo wakati akiwasilisha maoni ya kambi hiyo kuhusu muswada wa marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP).
Gekul alisema taratibu hazikufuatwa kwa kuwa haieleweki ni lini Serikali, wakala au Wizara ya Uchukuzi ilitangaza zabuni ya mradi wa treni kutoka Stesheni hadi Pugu kupitia JNIA.
“Pia haijulikani ni lini Serikali ilifanya upembuzi yakinifu kuhusu mradi huo wa reli kwa kufuata taratibu kama zinavyoainishwa na Sheria ya PPP ya mwaka 2010 ambayo inafanyiwa marekebisho hivi sasa,” alisema Gekul na kuongeza: “Haijulikani ni kampuni ngapi ambazo ziliomba tenda ya ukandarasi wa treni na kwamba M/s Shumoja ilishinda tenda hiyo kwa vigezo gani.”
Alisema kwa kifupi ni wazi kuwa Dk Mwakyembe na wizara yake walikiuka vifungu vya Sheria ya PPP. Alivitaja vifungu hivyo kuwa ni 4(1) na (2) vinavyomtaka waziri kutangaza katika Gazeti la Serikali miradi mbalimbali inayotegemewa kufanywa na sekta ya umma kwa ubia na sekta binafsi.
Gekul alisema pia kifungu cha 5(1) kilikiukwa ambacho kinaitaka mamlaka inayohusika kufanya upembuzi yakinifu baada ya kupembua mradi ambao utafanywa kwa ubia.
“Pia kifungu cha 9 kinachotaka mzabuni kutoa nyaraka mbalimbali za miradi ikiwamo jina, mahesabu yaliyofanyiwa ukaguzi pamoja na vielelezo vya uwezo wa kifedha,” alisema Gekul.
Alihoji kulikuwa na uharaka gani wa utekelezaji wa mradi huo ambao umekiuka Sheria ya PPP bila kuwahusisha wadau wengine ambao wangeweza pia kushindana na Shumoja?
“Ingekuwa ni vyema kama Serikali ingeweka bayana undani wa mkataba wa mradi huo ambao kama Watanzania hatujawahi kusikia ukitangazwa ili kutoa fursa kwa wazabuni wenye uwezo kushindania zabuni hiyo zaidi ya kuona na kuusikia mradi siku ya utiaji saini,” alisema.
Alisema Serikali ikishabanwa kutoa majibu juu ya uvunjwaji wa sheria, huja na majibu ya kejeli, hivyo Watanzania waelewe kuwa sheria zimekuwa zikipindishwa ili kupitisha miradi ambayo baadaye hugeuka kuwa mzigo kwao kama ilivyokuwa IPTL na Escrow.
Alisema pamoja na adha ya usafiri jijini Dar es Salaam, ukweli utabaki palepale kwamba, Dk Mwakyembe alisimamia mchakato wa mradi uliokiuka sheria ambao ikiwa utashindikana katika utekelezaji na mzigo wa uvunjwaji ama usitishwaji wa mkataba, gharama zitarudi kwa Watanzania.MWANANCHI

Wednesday 19 November 2014

HUYU NDYE BINTI ALIYESABABISHA KIFO CHA MASHAKA! MFANYABIASHARA MKUBWA ALIYEFARIKI NDANI YA GARI LAKE HUKO BUKOBA!



Inasikitisha sana kifo cha huyu bwana Leonard Mtensa kilichotokea ndani ya gari lake, mpenzi wake anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi. Hapa chini ni picha ya huyo dada na picha ya marehemu.
 
Jackline Hassan mwenye umri wa miaka 25 aliyekuwa na marehemu.
Huyu ndiye marehemu bwana Leonard Mtensa aliyekutwa na mauti ndani ya gari lake aina ya IST akiwa na mpenzi wake!

HAYA NDIO MAISHA! MADAME WEMA SEPETU ATUPIAMO AKIWA NA USAFIRI WAKE MPYA NA KUACHA FUMBO KAMA KAWAIDA!


Binti Wa Miaka 5 Abadilisha Maisha Ya Familia Yake.


Binti Mdogo Abadilisha Maisha Ya Familia Yake Kutoka Katika Hali Ya Kawaida Na Kuwa Katika Maisha Ya Hali Ya Juu,Jina Lake Anaitwa Breanna.


 Nyota Ya Mtoto Huyu Iling"ara Pindi Mama Yake Alipopost Picha Zake Katika Mtandao ambapo Alipata MashabikiZaidi Ya Milioni Moja  Waliomfolo Kupitia Page Yake Ya Instagram.

Breanna Anatokea Korea Kusini Lakini Kwa Sasa Anaishi Dubai Na Familia Yake,Amepata Mialiko Mbali,Mbali Ya Kwenda Kufanya Dili Za Uwana mitindo Na Sehemu Ambazo Ameshatembelea Bahrain Na Indonesia.

Breanna anabeba Mikoba Ya Gharama Kubwa Ikiwemo Louis Vuitton,Channel Na Kuvaa Nguo Za Wabunifu Wakubwa Duniani,Wakati Mwingine Mama Yake Anapata Hofu Kubwa  Juu Ya Binti Yake Na Kuhofia Ukuwaji Wake Kulingana Na Umaarufu Aliokuwa Nao.

Inapotokea Anaumwa Basi  Hupata   E-Mail Nyingi Kutoka Nchi MbaliMbali Kutaka Kujua Breanna.
 Kwa Sasa Ni    Gumzo Kwa Breanna Na Familia Yake Pindi Wanapopita Mitaani Kila Anae Muona anamshangaa na Kutaka Kupiga Nae Picha .