YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Sunday 15 February 2015

Waliowajeruhi polisi TZ wasakwa



Polisi nchini Tanzania
Polisi nchini Tanzania wamesema wanawasaka watuhumiwa waliowajeruhi askari sita kwa risasi mkoani Tanga.
Askari hao walijeruhiwa wakati wakifanya kazi ya kuwatafuta watuhumiwa wa uhalifu wa kutumia silaha wanaodaiwa kuwa walijificha eneo moja nje ya mji wa Tanga wakiwa na silaha.
Awali kulizagaa taarifa na hofu kuwa wahusika walikuwa na itikadi za kigaidi, lakini taarifa ya maandishi iliyotolewa na polisi imewaita watu hao kuwa ni majambazi na kwamba msako wa kuwatafuta unaendelea.
Hata hivyo taarifa haikuleleza wanaotafutwa ni watu wangapi, ingawa imetaja kuhusika kwa jeshi lenye silaha jambo linaloashiria mapambano yalikuwa makali.

UKWELI WA MAPAMBANO YA POLISI NA WAHALIFU KATIKA MAPANGO YA AMBONI TANGA




Kamishna Chagonja alisema chanzo cha mapambano hayo, ni tukio la Januari 26 mwaka huu, wakati askari wawili walipovamiwa na watu wasiojulikana na kunyang’anywa bunduki mbili aina ya SMG, zilizokuwa na risasi 60.
“Upelelezi wetu uliendelea baada ya tukio hilo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola kuwasaka na tukafanikiwa kupata wahalifu…jana asubuhi tuliarifiwa kwamba silaha hizo zimefichwa kwenye moja ya mapango ya Amboni na ndipo wakapeleka askari huko ili kuzitafuta,” alisema.
“Wakati askari hao wakiendelea kutafuta, ghafla walivamiwa kwa kupigwa risasi na watu waliokuwa wamejificha kwenye eneo lingine la pango hilo …ikalazimika wajibu mapigo,” alisema.
Kamishna Chagonja alisema baada ya kuzima mapigano, waliamua kuingia ndani ya mapango hayo na kukuta vifaa mbalimbali vya kutengenezea milipuko, pikipiki moja, baiskeli tatu, silaha mbalimbali za jadi ikiwemo mishale, pinde, visu na mapanga lakini hawakufanikiwa kukuta mtu.
*Ni Al Shabaab?
Akizungumzia kuhusu watu hao kwamba ni kikundi cha wahalifu wa Al shabaab au la, alisema mpaka sasa Polisi haijabaini kutokana na ukweli kwamba katika operesheni hiyo hawajafanikiwa kukamata mtu ambaye wanaweza kumfananisha na magaidi hao.
“Msako wetu unaendelea, tunaomba wananchi watoe ushirikiano… kwa kweli ni mapema sana kuthibitisha kwamba hao wahalifu ni wa kikundi cha Al-Shabaab kama inavyodaiwa mitaani, kwa sababu mpaka sasa hatujatambua sura zao na kubaini ni watu wa aina gani,” alisema.
Alisema askari waliojeruhiwa, wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga ya Bombo na hali ya afya zao inaendelea vizuri.
Hata hivyo taarifa kutoka kwa chanzo cha kuaminika ndani ya Hospitali ya Bombo, imeeleza kwamba askari mmoja wa JWTZ amefariki dunia jana saa 8.30 mchana ingawa Chagonja amekataa kuthibitisha kifo hicho.
Hali shwari
Licha ya kudai kwamba hali imerejea kuwa shwari, lakini mpaka sasa wako kazini na ulinzi umeimarishwa kuanzia katika eneo la Utofu lililoko umbali wa kilometa 5 kutoka mjini, ambapo askari wanaonekana kutaka kupata taarifa za kila mtu na magari yanayoendelea kutumia njia hiyo.
*Mitaani
Mitaani hali ya ulinzi na usalama miongoni mwa wananchi katika halmashauri ya Jiji la Tanga, iliendelea kugubikwa na hofu kubwa na mashaka kutokana na mapigano yaliyokuwa yakisikika baina ya askari na kikundi cha wahalifu hao.
Mapigano hayo yalikuwa katika kitongoji cha Mikocheni kilichopo kata ya Kiomoni kwenye machimbo ya mawe ambayo yameambatana na eneo la mapango ya Amboni.
Kwa mujibu wa baadhi ya wakazi wa kata hiyo iliyoko umbali wa kilometa 10 kutoka katikati ya Jiji la Tanga, walianza kuona vurugu za magari ya askari wa kutuliza ghasia pamoja na JWTZ wakikatiza katika maeneo hayo huku ikisikika milio ya risasi na vishindo vikubwa.
Agata Juma, mkazi wa Kiomoni Majimoto, alisema vurugu hizo zilisababisha wapate hofu na kukumbuka tukio la hivi karibuni la mlipuko wa bomu la kurushwa kwa mkono, uliotokea wiki tatu zilizopita kwenye eneo hilo.
“Yani hatuelewi kinachoendelea, maana askari hawazungumzi kitu na wananchi bali tunasikia sauti za ving’ora pamoja na mishindo ya vitu kama mizinga mikubwa ikilia … mambo hayo yanafanyika huko jirani na mampango ya Amboni,” alidai.
Naye Jumaane Amboni, alidai usiku kucha hawakupata usingizi kutokana na hofu, hasa baada ya kupata taarifa ambazo hata hivyo hazijathibitishwa na Polisi, kwamba eneo hilo limevamiwa na kikundi cha Waislamu wenye itikadi kali wa Al-shabaab.
“Usiku wa kuamkia leo (jana) mambo yalikuwa magumu sana maana tumesikia risasi zikirindima na vishindo kama vya mizinga vikilia mara kadhaa pasipo kuelewa cha kufanya…. tumeamua kukaa ndani na kujifungua. “Tunachofanya hapa ni kujaribu kukusanya mahitaji ya muhimu kama chakula na vitu vingine, kwa sababu hatuelewi hayo mapigano yataisha lini hasa ikizingatiwa kwamba eneo walilojificha ni ndani ya sehemu ya mapango ya mawe ambayo hayatumiki kabisa,” alisema.
Hata hivyo, baadhi ya wakazi katika maeneo ya katikati ya Jiji la Tanga, ingawa shughuli zinaendelea kama kawaida lakini wamekuwa katika hali ya wasiwasi.
HABARI LEO

.. MAJANGA...!!!! KWELI MWISHO WA DUNIA UMEKARIBIA..EMBU ONA HUYU MCHUNGAJI ANAVYOMWOMBEA HUYU MAMA!


Wanawake MUNGU awasaidie sana Mjue kujenga Mahusiano binafsi ya karibu na MUNGU mwenyewe kuliko kutegemea sana kuombewa hovyo hovyo,Kisa tu Umeambiwa na Rafiki yako kwamba yuko Apostle flani ana Upako sana.
Ndio ni kweli mna Matatizo mengi yamewasonga yakiwemo Ndoa zenu Watoto wenu,Biashara zenu,na Kadharika,Na mara nyingi nia yenu ni kufunguliwa kwenye hivyo vifungo vinavyowasumbua.Na shetani yuko karibu sana nanyi kwasababu anajua Nguvu iliyomo ndani yenu, ila wengi wenu hamjielewi.Ndio maana Mnafanyiwa vitu vingi sana kwa jina la kukombolewa na baadhi ya Watumishi kwa imani kwamba Mtapona.Na ndio maana kila huduma maombezi Mmejaa nyie na Ndio maana inakuwa rahisi sana kwenu kudhurumiwa mambo mengi kwa kujenga imani kubwa sana kwa watu kuliko BABA yenu.

Hebu tazama picha kama hii,Mumeo akikukuta unafanyiwa Maombi ya Staili hii "Atakuelewa kweli!?
 
Jifunzeni kumlilia MUNGU vyumbani mwenu na Mkumbusheni ahadi zake juu ya Maisha yenu na vizazi vyenu.

Tuesday 10 February 2015