YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday 16 July 2013

WANAJESHI WENGINE WATATU WA TANZANIA WAFARIKI DUNIA HUKO SUDANI,




WINGU zito limetanda kwa askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), katika nchi za Sudani Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Wakati Watanzania wakiendelea kuomboleza vifo vya wanajeshi saba wa jeshi hilo waliopoteza maisha katika Jimbo la Darfur, Sudani kwa kushambuliwa na waasi, nchini DRC yamezuka mapigano makali baina ya waasi na majeshi ya Serikali. 

Mapigano hayo yameripotiwa kuibuka kati ya Wanajeshi wa Serikali na waasi karibu na mji wa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Msemaji wa wapiganaji wa waasi wa M23, ameliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa ndege za kivita za Serikali zimefanya mashambulio ya anga katika maeneo yao usiku wa kuamkia jana.

Umoja wa mataifa kwa upande wake umesema uko tayari kutumia nguvu, kuwalinda raia ikiwa wapiganaji hao wa M23 wataingia katika mji wa Goma.

Raia wakimbia mapigano 

Wakati huo huo, mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu, yamesema kuwa zaidi ya wakimbizi elfu sabini raia wa Congo wamekimbilia nchi jirani ya Uganda, kukwepa mapigano hayo.

Wapiganaji wa waasi wa Uganda nchini Congo, Allied Democratic Forces walishambulia mji wa Kamango na kusababisha mapigano makali kati yao na jeshi la serikali.

JWTZ: Askari wetu DRC wapo salama
Kwa upande wake, Msemaji wa Jeshi la Tanzania (JWTZ), Kanali Mgawe, alipoulizwa kuhusu mapigano hayo aliwataka wananchi kutokuwa na wasi wasi kuhusu usalama wa wanajeshi wa Tanzania.

“Wanajeshi wa Tanzania wapo salama hakijatokea kitu chochote tofauti na kama kuna tatizo lolote tutatoa taarifa, wanajeshi wetu nchini Kongo DRC wapo salama,” alisema. 

Wanajeshi wengine wadaiwa kufa Darfur 
WAKATI Watanzania wakiendelea kuomboleza vifo vya wanajeshi saba wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), waliokufa katika Jimbo la Darfur nchini Sudani, askari wengine watatu wa jeshi hilo wamedaiwa kupoteza maisha.

Idadi hiyo imedaiwa kuongezeka, baada ya wanajeshi hao watatu ambao ni kati ya 14 waliokuwa wamejeruhiwa vibaya, nao kupoteza maisha katika shambulizi la kushtukiza.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya JWTZ, kimesema kuwaaskari hao wamefariki dunia baada ya jitihada za madaktari kuokoa maisha yao kushindikana.

Askari hao walifariki baada ya kushambuliwa na kikundi cha waasi wa Sudani, walipokuwa katika msafara wa kusindikiza waangalizi wa amani kutoka Khor Abeche kwenda Nyara, katika Jimbo la Darfur.

MTANZANIA ilipomtafuta msemaji wa jeshi hilo, Kanali Kapambala Mgawe kuzungumzia taarifa hizo, alisema hakuna taarifa zozote zinazoonesha kuwapo na ongezeko la idadi ya vifo vya Darfur, Sudani.

Kuhusu usafirishwaji wa miili ya askari hao kuja nchini, Kanali Mgawe alisema suala hilo la usafirishwaji wa miili ya askari hao, linaratibiwa na Umoja wa Mataifa (UN), ingawa JWTZ inafuatilia kwa karibu.

“Ninapenda kukuambia kuwa hadi sasa hakuna mwanajeshi aliyeongezeka, ila hizo ni taarifa ambazo si sahihi na zimekuwa zikienezwa katika mitandao ya kijamii. Sisi kama jeshi hatuna taarifa kama hizo,” alisema Kanali Mgawe.

Alipoulizwa kuhusu kutajwa kwa majina ya marehemu waliokufa katika tukio hilo la kushtukiza, Kanali Mgawe alisema jeshi haliwezi kutaja majina hayo kwa sasa, ila kinachofanyika ni kuwasiliana na ndugu wa marehemu hao.

“Safari hii asilimia kubwa ya askari wetu waliokwenda Sudan, wametoka katika mikoa ya mipakani, kwa hiyo tunachokifanya sasa tumeshawasiliana na makamanda wa kambi zote za jeshi ambazo wametoka marehemu hawa, ili waweze kuwasiliana na ndugu wa marehemu.

“Hivi ndugu utajisikiaje unasoma gazeti au unaangalia TV na kusikiliza redio halafu ukasikia kuwa ndugu yako amefariki utajisikiaje, ni lazima katika hili tuweze kufuata taratibu nzuri zinazokubalika kwa kuwasiliana nao moja kwa moja.

“Ninachotaka kuwahakikishia Watanzania kuwa JWTZ lipo imara na kama kuna taarifa yoyote tutaitoa mbele ya umma,” alisema.

Hata hivyo Kanali Mgawe alisema jeshi hilo limetuma ujumbe maalumu kwenda Darfur kuchunguza kiini cha tukio hilo, ingawa hakuweza kueleza kikosi hicho kinaundwa na wataalamu wa fani gani.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 16/7/2013 YA HABARI NA MICHEZO


DSC 0019 00396DSC 0018 6db76DSC 0017 4f3cbDSC 0016 efb81DSC 0011 16ad0DSC 0012 6cefcDSC 0013 5a4ce

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 16/7/2013 YA HABARI NA MICHEZO


DSC 0019 00396DSC 0018 6db76DSC 0017 4f3cbDSC 0016 efb81DSC 0011 16ad0DSC 0012 6cefcDSC 0013 5a4ce

SAMAHANI KWA PICHA MTOTO ABAKWA NA KUWEKWA MIWA SEHEMU ZA ZILI MPAKA KUFA...!!! (+18)



Vanusia Silva Pereila mdada mwenye miaka 9 mkazi wa kijiji kimoja nchini brazil,mapema wiki hii amebakwa karibu na shamba la miwa na watu wanaoaminika kuwa ni watumiaji wa madawa ya kulevya.



 
MAELEZO ZAIDI KUTOKA CHANZO CHA HABARI HII HAYA HAPA. 
The horrific crime happened in Arataca, state of Bahia, Brazil. Vanusia Silva Pereira was taken to a vacant lot, punched in the face, raped and then had a sugar cane forced up her snatch.
 
The victim’s father, identified as Mr. Wilson, an agricultural laborer told police that Vanusia chose bad company to hang out with lately and that was her demise. Police do not suspect that her murder was a crime of passion, however coroner who examined the body said the woman had been subjected to exceptional violence before death which brought the possibility of this being the crime of passion back into question.

TAZAMA PICHA ZA P-FUNK NA KAJALA WALIPOAMUA KWENDA KUMTEMBELEA BINTI YAO KATIKA SIKU YAKE YA KUZALIWA


aaccaa4ced0611e29f4822000aeb1254_7
Jana ilikua ni siku ya kuzaliwa ya mtoto wa kwanza wa producer Paul Matthysse aka P-Funk Majani aliyezaa na aliyekuwa mchumba wake Kajala Masanja. 

Wazazi hao wamemtembelea mtoto wao shuleni na kupiga naye picha

.
bb598fd6ed3011e2978e22000a1fb9d3_7

Kupitia Instagram, Kajala ameshare picha kadhaa zinamuonesha akiwa na Majani, binti yao Paula na Wema Sepetu.
fb926974ed3011e2af3c22000aa80233_7



Kajala amemwandikia ujumbe mtamu binti yake akisema:
  HAPPY BIRTHDAY my darling, my heartbeat, da reasonto whythez always a smile abt…ur my right hand, my sweetheart, my number one, my beautiful daughter…..mummy loves u sooo much sweet angel….and I pray to god to keep u for a long long tym… u will live to blow a hundred candles my precious….
Happy Birthday, Paula.

MTANGAZAJI WA KIKE WA REDIO AKUTWA AKIFANYA MAPENZI NDANI YA GARI:




The act of making love has led to the disgrace and downfall of a number of personalities. Last Saturday, a seasoned radio presenter of one of the radio stations was caught making out with a younger musician in her car. 

The duo who were busted by the female presenter collegues later drove off in the said presenters car. Their action attracted the attention of two workers who saw the car bouncing and when they got closer, lo and behold the presenter was seen half naked and doing God knows what.

TAZAMA PICHA ZA KILICHOJIRI KATIKA MAZISHI YA MWANAFUNZI WA IFM, ALIYEZAMA BAHARINI.




CONTINUE READING:

















Makamu Mkuu wa Chuo cha Tumaini Makumira, Prof. Parsalaw akiongea nenoa.


Askofu Mkuu wa KKKT. Ask.Dr. Alex Malasusa akitoa salamu za Kanisa.









Ni vilio tu kwa waombolezaji



Rachel Fute na Vaileth Lwendo ambao ni Dada wa Marehemu wakipita
Mama wa Marehemu akisaidiwa kutoa heshima kwa Binti yake.

Baba wa Marehemu, Mchungaji Habakuki Lwendo akimuaga Binti yake.





Vilio vilitawala kanisani


Sanduku lililouhifadhi mwili wa Marehemu Wende likiwa tayari kushushwa kaburini.



Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam leo wameungana na Familia ya Mchungaji, Habakuki Lwendo na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) katika mazishi ya Binti yao Wende Lwendo aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Uhandisi Kompyuta katika mazishi yaliyofanyika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Wende alifariki Ijumaa ya Julai 12, 2013 wakati akijumuika na rafiki zake kuogelea Bahari ya Hindi eneo la Ufukwe wa Kipepeo Kigamboni kilometa chache kutoka eneo alilokuwa akishi.
Mazishi hayo mbali na wanafamilia na wanafunzi wa IFM kuhudhuria pia yalihudhuriwa na Askofu Mkuu wa KKKT Tanzania, Askofu, Dk Alex Malasusa, Makamu Mkuu wa Chuo cha Tumaini Makumira, Prof. Parsalaw pamoja na wachungaji mbalimbali na Wafanyakazi wa Chuo cha Makumira anakofanyia kazi Mchungaji, Habakuki Lwendo ambaye ni baba wa Marehemu Wende.
Picha na Jestina George