YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Saturday 26 July 2014

MFANYAKAZI WA NDANI ABAKWA HADI KUFA HUKO DODOMA,ALIPOTEA TANGU JUMAMOSI ILIYOPITA


Kinamama walio karibu na familia ya marehemu Isabela Andrew aliyebakwa hadi kufa wakiangua kilio baada ya kushuhudia mahali mwili wake ulipokutwa huko Area C mjini Dodoma jana. 
Mfanyakazi wa ndani, Isabella Andrew (18), amefariki dunia na kifo chake kikidaiwa kusababishwa na kubakwa na watu wasiojulikana.

Mwili wa msichana huyo ulikutwa ukiwa umeharibika katika moja ya pagale, lililopo Area C, Dodoma Mjini na mwandishi wetu alishuhudia ukitolewa hapo kwa machela huku polisi wakiwahoji mashuhuda wa tukio hilo.

Mkazi wa Mtaa wa Kiwanja cha Ndege, Jackson Coy aliyekuwa akiishi na binti huyo alisema msichana huyo alipotea tangu Jumamosi iliyopita.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime, alisema mwili huo uliokotwa jana saa mbili asubuhi na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha kifo chake.

Mwili huo ulibainika baada ya mama mmoja, Rehema Msambile kufika katika pagale hilo alipokuwa akifuatilia nyendo za mtoto wake ambaye juzi alipigwa kwa tabia ya utoro shuleni.

“Niliamua leo (jana) kumfuatilia, nikaanza katika mapagale.Nilipofika hapa ndipo nikaona mwili wa marehemu ikabidi nimuite jirani hapo aje aone,” alisema.

Diwani wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Henry Kandenga alisema mazingira yanaonyesha kuwa binti huyo alibakwa kwa sababu walikuta nguo za ndani zikiwa pembeni.

“Hakuna yowe iliyosikika kwamba kuna mtu anauawa ukizingatia kwamba nyumba ziko jirani na hata nyumba aliyokuwa akiishi ni jirani na mahali alipokutwa,” alisema .

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma

HUSSEIN MACHOZI AFUMANIWA KENYA NA MKE WA MTU,

Hussein Machozi afumaniwa akizini na mke wa mwanasiasa maarufu Kenya

posted 3 hours ago by admin
Hit maker wa  ‘Kwa Ajili Yako’, Hussein Machozi aliyekuwa ameweka kambi na kukubalika sana nchini Kenya anadaiwa kuwa amefumaniwa na mke wa mwanasiasa wa nchini humo na kupewa masaa 24 kuvuka mpaka wa Kenya.
Kwa mujibu wa gazeti la The Star la Kenya, Hussein Machozi alikuwa anatembea na mwanamke wa mwanasiasa huyo wa Mombasa kwa muda mrefu kwa siri huku wakiwa na mipango mikubwa ikiwa ni pamoja na kununua nyumba.
Lakini mapenzi ni kikohozi, siri hiyo ilimfikia mwanasiasa huyo baada ya kushtukia pale alipoona ujumbe usio wa kawaida kwenye simu ya mkewe kwa njia ya WhatsApp.
Mwanasiasa huyo ambaye anadaiwa kuwa mtu anaesafiri mara kwa mara  kufanya biashara na kushughulikia mambo ya siasa aliamua kuweka mtego ambao ulimnasa mwizi wake na kumtia mikononi mwake.
Gazeti hilo linaeleza kuwa liliongea na rafiki wa karibu wa Hussein Machozi wa Mombasa anaefahamika kwa jina maarufu Notystee na alikiri kutokea kwa tukio hilo.
“Nilishtuka pale nilipopokea simu kutoka kwa Hussein Machozi akiniambia kuwa alikuwa katika tatizo. Aliniambia mapema kuwa anaenda kukutana na mwanamke ambaye alikuwa mpenzi wake lakini sikujua kitu ambacho kingetokea.”
Hata hivyo, Hussein Machozi anaonekana bado yuko nchini Kenya kwa mujibu wa chanzo chetu

MAUZAUZA NDANI YA KABURI LA ADAMU KUMBIANA...YALIYOTOKEA HAPA NI ZAIDI YA YALIYOKUTWA KWA RECHO


SIKU chache baada ya kukutwa mauzauza katika kaburi la mwigizaji Rachel Haule ‘Recho’, kaburi la mwigizaji Adam Kuambiana (pichani)limekutwa limetoboka kimaajabu.

Gazeti la Risasi Jumamosi toleo la Julai 19, mwaka huu lilikuwa na babari yenye kichwa cha habari kisemacho: ‘Uchawi kaburini kwa Recho.’ Kwenye habari hiyo, ilielezwa kuwa katika kaburi la Recho kulikutwa tunguri iliyoviringishwa shanga, kitambaa cha kanga chakavu, manyoya ya kuku, yai moja na vitu vingine ambavyo havikujulikana ni nini.

Baada ya habari hiyo, siku mbili baadaye, chanzo kingine kiliwapigia simu waandishi wetu na kuwaeleza kuwa mbali na tukio la Recho, kaburi la Kuambiana limetoboka kimaajabu na kuzua mtafaruku miongoni mwa watu walioshuhudia kwa mara ya kwanza tukio hilo.

“Jamani haya ni mambo ya kishirikina, huwezi amini kaburi hili limetoboka ghafla kimaajabu maana juzi tu nilikuja kutembelea makaburi haya, lilikuwa halijatoboka,” kilisema chanzo hicho.

Mapaparazi wetu walifika katika makaburi hayo na kujionea kaburi hilo likiwa limetoboka huku watu wengi waliokuwepo eneo hilo walidai kuwa tukio hilo si la kawaida kwani limetokea wakati ambao mvua hazijanyesha.

Walisema kama tukio hilo lingetokea wakati ambao mvua zinanyesha basi wasingekuwa na mashaka lakini kwa jinsi ambavyo limetoboka wakati wa jua kali ni dhahiri kutakuwa na ‘mkono wa mtu’.
“Hapa bwana tusidanganyane kuna mkono wa mtu, haiwezekani kaburi lisitoboke kipindi kile cha mwanzomwanzo lije kutoboka sasa wakati kuna jua kali namna hii, lazima kuna mkono wa mtu tu,” alisema shuhuda mmoja.

Wengine walikwenda mbali zaidi kwa kuhoji kulikoni matukio hayo yawe kwa mastaa pekee na si kwa watu wengine?“Hii si bure hapa wachawi watakuwa na shida yao binafsi, haiwezekani iwe kwa mastaa tu ndiyo kunakuwa na mauzauza,” alisikika shuhuda mwingine.
Alipoulizwa mmoja wa walinzi wa eneo hilo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema hata yeye hajui kwa nini inatokea katika makaburi ya mastaa.“Mimi hata sijui kwa nini lakini yamefululiza, juzi tumeona kwa Recho na leo kwa Kuambiana, tumuombe sana Mungu atuepushe na mabaya,” alisema mlinzi huyo.

Hata hivyo, licha ya watu wengi walioshuhudia kaburi hilo kuamini katika uchawi, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye alionekana ni mcha Mungu alisema hakuna uchawi wowote zaidi ya ardhi kutitia na kusababisha mmomonyoko wa udongo.

“Jamani siyo uchawi, hivi vitu vinatokea. Hapa itakuwa wakati wa kuzika, kulikuwa na uwazi umeachwa hivyo ardhi iliposhuka kuziba uwazi huo ndipo iliposababisha tobo,” alisema shuhuda huyo mcha Mungu.
Kuambiana alikutwa na umauti Mei 17, mwaka huu alipokuwa akipelekwa katika Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge, Dar baada ya kuugua ghafla akiwa hotelini alipokuwa amepanga kwa ajili ya kuandaa filamu.

PICHA; AJARI YA FUSO HUKO SHINYANGA

25

  • Jul2014


Miili ya marehemu ikiwa katika eneo la dharura katika hospitali ya mkoa wa shinyanga
Hapa ni katika eneo la dharura katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga ambapo majeruhi 29 hadi sasa wamepokelewa kufuatia ajali ya gari aina ya fuso iliyokuwa imebeba watu wengi pamoja na mizigo kuelekea katika mnada wa Mhunze uliopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.Ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo Alhamis.Pichani majeruhi waliendelea kuhudumiwa na wataalam wa afya katika hospotali ya mkoa wa Shinyanga
Kwa mujibu wa kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja Daniel ameiambia malunde1 blog kuwa mpaka sasa wamepokea miili miwili ya marehemu na majeruhi 29
Huduma inaendelea kutolewa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga
Baadhi ya majeruhi wameiambia malunde1 blog kuwa gari aina ya fuso waliyokuwa wamepanda tena kwa kujazana ilikuwa inafukuzana na fuso nyingine na ghafla walijikuta wakiwa wameshapinduka
Kulia ni kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja Daniel akichukua maelezo kutoka kwa askari wa usalama barabarani
Majeruhi akipelekwa wodini
Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja Daniel akizungumza na waandishi wa habari hivi punde-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

ANGALIA PICHA ZA MAKAHABA WA KICHINA WAKIKIMBIZWA NA ASKARI DAR





Tag : AIBULAANAMAJANGA

MAMBO ANAYOYAFANYA SHILOLE NA WENZIE






 

















AFUMWA NA KUTEMBEZEWA KICHAPO LAIVU

TIMBWILI la aina yake lilifumuka ndani ya gesti moja iliyopo Mbezi Afrikana jijini Dar es Salaam (jina kapuni), kufuatia kijana aliyefahamika kwa jina moja la Kelvin kumkuta chumbani mtu aliyedai ni mjomba wake, Joseph akiwa na mkewe wa ndoa, Emiliani.
Mjomba wa Kelvin(Joseph) akimsihi Mpwa wake amsamehe mara baada ya kukutwa gesti na mke wa Kelvin.
Mkasa huo wa ajabu ulijiri usiku wa Jumamosi iliyopita kwenye gesti hiyo iliyopo Mbezi ya Afrikana jijini Dar es Salaam.
MPISHI WA FUTARI AUZA ISHU OFM
Mama mmoja aliyedai ni mpishi wa futari maeneo hayo, alipiga simu kwa makamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) na kusema:
Kelvin (kulia)'akidili' kisawasawa na mjomba wake. 
“Mimi ni mpishi wa futari hapa Mbezi Afrikana kuna baba mmoja na ndugu zake wanachakazana, kisa wamefumaniana kwenye gesti ya (akaitaja jina). Ipo hapahapa jirani njooni muwahi.”
Mlinzi wa gesti akijaribu kumzuia Kelvin asizidi kumjeruhi mjomba wake.
OFM KAZINI, AIBU!
Kufuatia taarifa hiyo, mkuu wa zamu wa OFM aliwaagiza mapaparazi wake wanaotumia pikipiki ziendazo kasi ambao walitumia muda usiozidi robo saa kutoka walipokuwa kufika eneo la tukio ambapo walimkuta Kelvin amemvaa mjomba ‘ake chumbani ambapo timbwili zito lilitifuka. Walikuwa wakigaragazana huku mjomba mtu huyo akiwa kama alivyozaliwa na damu chapachapa jambo lililomtia aibu!
Mjomba akiwa chumba cha gesti mara baada ya mkong'oto 'hevi' kutoka kwa mpwa wake.
PICHA ZA TUKIO
Mapaparazi wetu bila kuzubaa nao walianza kuchukua picha za tukio  hatua kwa hatua. Wakati Timbwili likiendelea, Joseph alikuwa akipiga mayowe kumuomba mpwa wake huyo amsamehe ili wayamalize kimyakimya na kumsihi asisambaze habari hizo zikafika mpaka nyumbani kwa mke wake.
MKE ATIMKA KINYEMELA
Katika hali ya kushangza, wakati wawili hao wakiendelea kuangushana chumbani, mke huyo alipata upenyo na kuchoropoka, akatimua mbio kwa kuhofia kipigo na kukwepa kamera za OFM.
...Mjomba taratiiibu 'akirejesha' mavazi mwilini mwake.
MLINZI WA GESTI
Timbwili la wajomba hao lilitulizwa na mlinzi wa gesti hiyo (jina halikujulikana)  ambaye alitumia mabavu na kufanikiwa kuwadhibiti na kuwaweka kitako.
MJOMBA MTU AGOMA KWENDA POLISI
Baada ya kutulizwa, Kelvin aling’ang’ania waende polisi lakini mjomba mtu alikataa katakata akimbembeleza mpwa wake kwamba wayamalize na kuahidi kutorudia tena mchezo huo huku akisema mwanamke huyo alimuwekea mtego wa makusudi.
Mjomba akiomba msamaha kwa mpwa wake.
CHONDECHONDE KELVIN
Baadhi ya waungwana waliofika kushuhudia tukio hilo walimsihi Kelvin kumsikiliza mjomba ‘ake na kupokea fidia kidogo kwani kuyasongesha mbele mambo hayo ni aibu kwa familia yao na kumtia matatani mjomba huyo kwa mkewe.
MJOMBA ‘AJIKOMITI’ KIMAANDISHI
Kufuatia maombi ya watu, akiwemo mlinzi wa gesti hiyo, Kelvin alikubali kumsamehe mjomba wake ambaye naye ‘alijikomiti’ kimaandishi (kopi tunayo) kumlipa Kelvin fidia ya shilingi laki tano (500,000) na kuahidi kutorudia kummendea mke wake.
Sehemu ya nyaraka ikionyesha mjomba 'akijikomiti' kimaandishi.
Katika barua hiyo aliyoaindika Joseph kwa mkono, alikiri kukutwa na mke wa Kelvin na kusema anatoa shilingi laki tatu (300,000) siku hiyo kisha kiasi kinachobaki atatoa siku inayofuata.
MGONI AGEUKA NA KWENDA KUFUNGUA KESI
Hata hivyo, taarifa zilizotufikia wakati tunakwenda mitamboni zinadai kuwa, Joseph alikwenda kituo cha polisi (jina halijajulikana) kumfungulia kesi mpwa wake Kelvin na mkewe Emiliani akidai walipanga kumfanyia fumanizi.
KUTOKA KWA MHARIRI
Kwa sababu kisa hiki kinadaiwa kufikishwa polisi na Joseph, magazeti pendwa ya Global yataendelea kukifuatilia ili kujua mwisho wake. Endelea kusoma.

SHILOLE ANATAFUTA KIKI KUPITIA JINA LANGU, KWANZA SI HADHI YANGU. SIWEZI KUJIBISHANA NA MSANII WA VIGODORO,

 


MTIFUANO mzito umeibuka kati ya mastaa wa Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na Baby Madaha baada ya kurushiana vijembe.Awali katika gazeti la Amani toleo la wiki iliyopita, Baby Madaha alinukuliwa akisema kuwa Mwezi wa Ramadhani unambana kiuchumi, kwa vile kumbi nyingi za starehe zimefungwa, hivyo anakosa shoo.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Shilole alisema anamshangaa Madaha kwa kukosa hofu ya Mungu, huku akimchana kuwa, haweki akiba, anaishi maisha ya kutegemea shoo ndiyo maana anaulalamikia mwezi huu.
Madaha alivyoelezwa kuhusu maoni ya Shilole, alikuja juu na kutema cheche: “Shilole anatafuta kiki kupitia jina langu, kwanza si hadhi yangu. Siwezi kujibishana na msanii anayetegemea shoo za kwenye vigodoro, akatafute pa kutokea

# 10 SIRI YATOBOLEWA CHANZO CHA BIFU KUBWA KATI YA DIAMOND PLATNUMZ NA ALLI KIBA.. SHUKA NAYO HII HAPA



Leo ilikuwa ni siku ya Ya mkali wa zamni wa Bongo fleva, Ali kuba akiachia ngoma zake mbili katika kipindi cha XXL cha CLOUDs FM, Kama umefuatilia katika wiki hii kumekuwa na vuguvugu kali linaloendelea kati ya Mahasimu hawa wawili, sasa wengi wakiwa hawajui nini chanzo cha Bifu kubwa linaloendelea kati ya Diamond Platnumz na Ali Kiba.
Katika ali ya kutaka kujua ukweli mtangazaji wa kipindi hicho alimtandika swali la kizushi Ali Kiba kuhusu Bifu hilo linaloendelea mapka sasa huku akitaka kujua chanzo kikubwa cha yeye na Diamond na yeye kuhitiliafiana. Ali aligoma kabisa kuelezea chanzo cha ugomvi ama bifu lililo kati yao. Bila ajizi Dj FETTY aliamua kuweka wazi chanzo cha vuguvugu hilo. kuwa katika wimbo wa LALA SALAMA wa Diamond kulikuwa kuna mistari ama verse ambazo alitakiwa kuimba Ali Kiba, lakini kwa mshangao Diamond alifuata mistari ambayo Ali Kiba ilibidi aimbe, na kwa upande wa pili Alikiba katika wimbo wake wa Single boy pia kulikuwa kuna verse ambazo Diamond ilibidi aimbe lakini Alikiba akaamua Kumtolea nje na kumshirikissha Lady Jay dee.
Kwa hiyo Hiyo no sababu kuu kati yanyingi zinazopelekea Bifu kubwa kati ya wasanii hawa wawili wa Bongo Fleva. ni mengi yamezungunzwa ndani ya kipindi hicho cha XXL,