YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday 21 June 2016

MAMBO MUHIMU KATIKA KUTUMA MAOMBI YA CERTIFICATE NA DIPLOMA



TETESI ZA USAJIRI BARANI ULAYA.


Mabingwa wa Ulaya Real Madrid wameanza mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Ufaransa, Paul Pogba, 23, kutoka Juventus, kwa mujibu wa wakala wake (Marca), mabingwa wa EPL Leicester wako tayari kulipa pauni milioni 30 kumsajili mshambuliaji wa Watford Troy Deeney, 27, baada ya dau lao kukataliwa mara mbili (Mirror), kocha msaidizi wa Manchester United Ryan Giggs ambaye anatarajiwa kuondoka Old Trafford, huenda akawania kazi ya kuifundisha Nottingham Forest (Mirror), hata hivyo taarifa nyingine zinasema Giggs hana mpango wa kwenda Forest ambayo wamiliki wake wanamtaka meneja wa zamani wa Olympiakos Michel (Nottingham Post), meneja mpya wa Chelsea Antonio Conte anapanga kumsajili winga wa Lazio Antonio Candreva, 29, pamoja na beki wa Juventus Leonardo Bonucci, 29 (Sun), meneja wa Pari St-Germain Laurent Blanc ataondoka wiki hii (Europe 1), Liverpool wanapanga kupanda dau kumtaka winga wa England na Newcastle Andros Townsend, 24 (Mirror), Manchester City pia wanamtaka Townsend ambaye ada yake ni takriban pauni milioni 10.5 (Telegraph), Everton wameanza mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji kutoka Cameroon, Vincent Aboubakar, 24, kwa pauni milioni 16 kutoka Porto (Daily Mail), West Brom wanataka kumsajili kiungo Moussa Sissoko, 26, kutoka Newcastle (Birmingham Mail), meneja wa zamani wa Manchester United Louis van Gaal, meneja wa zamani wa Ajax, Frank de Boer na Andre Villas-Boas wanawania kazi ya kuifundisha AC Milan (La Gazzetta dello Sport), mshambuliaji wa AC Milan Fernando Torres, 32, anatarajiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja Atletico Madrid (Marca), Crystal Palace, Aston Villa na Norwich wanataka kumsajili kiungo wa Reading Aaron Tshibola, 21 (GetReading), Swansea wako tayari kuwapa mikataba mipya Leon Britton na Angel Rangel (South Wales Evening Post), meneja wa Sheffield Wednesday Carlos Carvalhal hawanii nafasi ya umeneja Southampton (Sheffield Star), mshambuliaji wa Manchester City Kelechi Iheanacho, 19, huenda akakosa mwanzo wa msimu baada ya kuitwa na timu ya taifa ya Nigeria kushiriki michuano ya Olimpiki mjini Rio (Manchester Evening News). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.

UJUMBE WA RAISI KWA WABUNGE.

Rais John Magufuli ametuma ujumbe bungeni kuwa yeye ni mbunge namba moja na anataka mapato yake yote yakatwe kodi stahiki, hatua inayofuata ni kutoachwa kwa mtu yeyote katika suala la kodi ya mapato.Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alitangaza ujumbe huo wa Dk Magufuli kwamba alipewa mapema alipopeleka pendekezo la kukata kodi ya mapato katika kiinua mgongo cha wabunge. Kwa mujibu wa Dk Mpango, kabla hata ya kuwasilisha mapendekezo ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017, alipeleka mapendekezo hayo ya kwa Rais Magufuli.“Nataka niwaambie, nilipopeleka hili (kukata kodi kiinua mgongo cha wabunge) kwa Rais, alinishangaa na kisha akasema yeye ni Mtanzania na ni lazima Watanzania wote walipe kodi kwa ajili ya kuendeleza nchi yao. “Rais alisema yeye ni mbunge wa kwanza wa Tanzania mpya na anapenda awe wa kwanza kukatwa kodi stahiki katika mapato yake, hivyo sasa kiinua mgongo cha Rais kitakatwa kodi,” Dk Mpango aliwaambia wabunge wenzake jana wakati akifanya majumuisho ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2016/17.Kutokana na kauli hiyo ya Rais, Dk Mpango alisema hata Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa viinua mgongo vyao lazima vikatwe kodi. Alimgeukia Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, akamwambia kuwa na yeye lazima akatwe kodi kisha akawageukia mawaziri, akawakumbusha kuwa wao ni wabunge na kwa dhamana waliyopewa kuwa mawaziri, wanapaswa kuongoza kwa mfano katika kukatwa kodi ya mapato katika mapato yao.Hatua hiyo, kwa mujibu wa Dk Mpango, inashuka katika ngazo zote za uongozi, kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya, ambao nao pia kiinua mgongo chao, lazima kikatwe kodi. Akifafanua hatua hiyo ya serikali kukata kodi ya mapato kwa kila mtu, waziri alisema sheria inataka vyanzo vyote vya mapato vikatwe kodi na kiinua mgongo ni moja ya vyanzo vya mapato vinavyotambulika na sheria hiyo.Alisema kila Mtanzania amekuwa akikatwa kodi hiyo isipokuwa wachache na hatua hiyo ya serikali inalenga kutoa haki sawa katika utozaji kodi kwa jamii yote. Baada ya muda, Naibu Spika, Dk Tulia alitania mbona Mwanasheria Mkuu George Masaju na Spika Job Ndugai hawajatajwa au wao wamesamehewa; na katika jibu la ishara, Dk Mpango alionesha kutikisa kichwa kueleza kuwa hawajasamehewa, bali nao watakatwa kodi hiyo.

DEREVA WA HALIMASHAURI AGEUKA MUHASIBU.

Upungufu wa watumishi katika kituo cha afya cha Likombe manispaa ya Mtwara Mikindani, kimepelekea dereva wa kituo hicho Ally Mchanyambi kutumika kukusanya mapato ya kituo,hali iliyowashangaza madiwani wa halmashauri hiyo na kutoa agizo kwa mkurugenzi  wa manispaa hiyo kumuondoa kwenye nafasi hiyo mara moja  na nafasi ijazwe na mtumishi mwenye sifa za uhasibu .

MANENO YA ABDUL JUMA MCHEZA WA YANGA MARA BAADA YA KUPOTEZA MECHI.


" Wachezaji tumeumia sana kwa matokeo ya kufungwa dhidi ya MO Bejaia, goli tulilofungwa lilitokana na walinzi kukosa mawasiliano kuukabili mpira uliopigwa kuelekea lango letu ___ Timu yangu ilicheza vizuri sana sema tu tukashindwa kutumia nafasi za kufunga tulizokuwa tumezipata

"Siwezi sema tumefungwa kwa sababu mimi sikuwepo hapana, pengo langu kwa kiasi fulani lilionekana maana washambuliaji akina Ngoma na Tambwe walikosa zile krosi walizozoea ambazo huwa nawalisha, mchezo ujao ni dhidi ya TP Mazembe ambayo ni timu kubwa barani Afrika wao pia wanatambua Yanga ni timu kubwa kwa sasa hivyo utakuwa ni mchezo mgumu na lazima tupambane tupate matokeo na naamini tutafuzu hatua inayofuata

"Bado sijaanza mazoezi mepesi nataraji kuanza kesho au Alhamisi itategemea na ushauri wa daktari, hapa naelekea kuonana naye ili anipe maendeleo ya jeraha" Alimalizia Juma Abdul,mlinzi wa Yanga aliyeko majeruhi.

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI ATOA TAMKO KWA WALIMU.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Salum Hapi, amesema walimu wote ambao hawaridhiki na mishahara yao ni bora watafute shughuli nyingine za kufanya.

Kwa mtazamo wako kauli hii unadhani ni sawa?

KUNDI LA ALSHABAAB LADAI KUFANYA MASHAMBULIZI


WABUBGE WANAPOTOKA NJE YA UKUMBE WA BUNGE

HUWAKILISHI WA WANANCHI UPO WAPI?  HASWA PALE WABUNGE TULIOWACHAGUA WANAPOAMUA KUTOKA NJE YA UKUMBI WA BUNGE.  HATA HIVYO HAKI IK9 WAPI PALE BUNGENI?  KWA SABABU MALALAMIKO MENGI YAMEKUWA YAKITOLEWA NA KAMBI RASMI YA UPINZANI KUHUSU MWENDENDO MZIMA WA VIKAO VYA BUNGE.  TAFAKARI Na chukua hatua



UTATA WA MATUMIZI YA KADI ZA MABASI YA MWENDO KASI


Utata katika matumizi ya kadi za kupandia mabasi ya DART.  Haya ni baadhi ya mambo ambayo bado wananchi wangepende kuelekezwa haswa katika matumizi ya kadi za kupandia magari ya DART.  Mtumiaji wa card anapaswa kuelezwa ni wakati gani haswa ambapo ataweza kuswap kadi yake je ni akiwa anaingia kwenye basi au anatika kwenye basi?  Na vipi kuhusu makato na salio la kiasi kilichobakia kwenye card yake atawrza kutambuaje?  Maswali mengine muhimu unaweza kushare na sisi katika comment..... 

WABUNGE KUHAIDI KUFANYA MIKUTANO YA SIASA NCHI NZIMA.


Monday 20 June 2016