YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Wednesday 2 April 2014

MAGOLI YOTE YA MECHI ZA UEFA JANA USIKU.


article-2594421-1CBF5C8300000578-254_634x345

Manchester United jana walitoka sare na mabingwa watetezi wa kombe la ulaya FC Bayern Munich katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Old Trafford. Unaweza kutazama video ya magoli ya mchezo huo hapa……



Tuesday 1 April 2014

DARAJA LA RUVU LAFUNGWA, MKUU WA WILAYA YA BAGAMOYO AWAPIGA 'STOP' WAKAZI WA KIWANGWA KWENDA BAGAMOYO


 Wakazi wa Kiwangwa, wa Kiwangwa, wakivushwa na vijana waliojitolea kujipatia ajila katika Daraja la Ruvu kwa kuwavusha wananchi kwa kuwabea ama kuwaongoza njia ili kuvuka eneo hilo la daraja lililojaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini. Kamera ya Sufianimafoto iliwashuhudia viajana hao wakiwavuja raia katika eneo hilo kwa ujila wa Sh. 2000 kwa kila aliyebebwa mgongoni asiyetaka kuvua viatu ama kugusa maji hayo, na Sh. 500 kwa kushikwa mkono kuongozwa njia kutoka mwanzo wa maji hayo hadi kuyavuka, na kuyaongoza magari kuvuka eneo hilo ni Sh. 3000 hadi 5000.

Kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jana, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi, alifika eneo hilo na kujionea wananchi wakitaabika kuvuka ene hilo na huku magari ya abiria yaliyokuwa yakitokea Bagamoyo kwenda Kiwangwa, yakibeba abiria na kuishia eneo hilo na kubeba wengine walioshushwa upande wa pili na kugeuza kwa kila abiria kulipa Sh. 1000. Na kisha abiria hao wakipata usafiri mwingine wa kubebwa na Vijana waliopo eneo hilo kwa Sh. 2000 kwa aliyependa ama 500 kwa kuongozwa njia.
 Vijana hao wakiliongoza moja ya gari lililokuwa likivuka eneo hilo ambapo dereva anafuata njia wanayopita vijana hao wa kulia na kushoto hadi kuvuka ili kuoepuka kupita eneo hatarishi na kutumbukia ama kusukumwa na maji hayo yaliyokuwa yakionekana kuwa na nguvu kubwa.
 Mkuu wa Wilaya ya bagamoyo, Ahmed Kipozi, akizungumza na watendaji wake aliowaagiza kusimamia zoezi la kuwazuia wananchi kuvuka eneo hilo, ambapo watendaji hao walimueleza Mkuu huyo wa Wilaya kuwa wananchi wamekuwa wakaidi na kuamua kukataa kutii amri na kuvuka, jambo lililomfanya Mkuu wa wilaya kuamua kuagiza askari Polisi wenye silaha ili kulinda eneo hilo kuwazuia waanchi kuvuka ili kuepuka maafa.

''WA HUKU WA HUKU NA WA HUKO WA HUKO''
Baada ya hapo Mkuu huyo wa Wilaya aliwatoa tamko na kuwataka wakazi wa Kiwangwa kutokwenda Bagamoyo na waBagamoyo kutokwenda Kiwangwa, kwa kipindi chote cha mvua ili kuepuka maafa yanayoweza kutokea kwa kutumbukia na kusombwa na maji, ama daraja hilo la Jeshi kukatika kutokana na maji kuanza kupita juu ya daraja hilo jana.
 Mkuu wa Wilaya, akizungumza na madereva wa magari waliokuwa wakisubiri kuvuka eneo hilo pamoja na vijana waliokuwa wakitoa huduma ya kuwavusha watu.
 Vijana wakifanya kazi yao ya kuwavusha watu eneo hilo.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI»

 Baadhi ya magari yaliyokaidi amri yakivuka eneo hilo.
 Vijana hao waliwavusha hadi wagonjwa katika eneo hilo kama anavyoonekana pichani akiwa amembeba mtu mzima anayeonekana kuwa ni mgonjwa.
 Baadhi ya vijana walijiona kama wapo Beach, walikuwa wakipiga mbizi na kuogelea eneo hilo kwa furaha.
 Magari yakiwa katika foleni kusubiri kuvuka eneo hilo.
 Baadhi ya abiria walioshushwa upande wa pili wakiwania usafiri wa kuelekea Bagamoyo baada ya kufaulishwa na gari jingine la uapnde wa pili.
 Hawa nao ni wa upande wa pili 
 Gari la Abbas Tarimba likivuka eneo hilo.
 Vijana wakijipigia debe kwa dereva ili akibali kuvushwa, bila kujua kuwa ndani yake alikuwapo Mkuu wa Wilaya hiyo.
 Katapila lililoletwa ili kuziba eneo hilo kuzuia magari kuvuka....
 Haya ni baadhi ya madaraja ya barabara mpya inayojengwa yakiwa yamejaa maji.
 Dereva wa pikipiki akipakia gunia la mkaa vizuri ili awapakie na abiria wake wawili baada ya kuvuka darajani hapo.
 Haya ni baadhi ya maeneo hayo yaliyojaa maji, ambapo mmoja wa vijana hao anaonekana akipiga mbizi kwa furaha.
 'Bonge' la Mgahawa likiwa limejaa maji
Pembeni (kulia) ni mtumbwi unaotumiwa na wakazi wa eneo hili kuvuka kuelekea upande wa pili.Chanzo Sufiani Mafoto.com

MADAWA YA KULEVYA YAKAMATWA GEREZA LA KEKO,YAINGIZWA KWA NJIA TATA, HAKUNA ALIYEAMINI



PIPI 60 za madawa ya kulevya aina ya heroine yanayokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi milioni 60 yanadaiwa kukamatwa ndani ya Gereza la Keko jijni Dar es Salaam baada ya mtu mmoja kuingia nayo akiwa ameyameza.

Madawa ya kulevya.
Kwa mujibu wa chanzo, mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Mashujaa Udugu Matata, aliingia gerezani humo Machi 21, mwaka huu akitokea kusomewa shitaka la kukutwa na madawa ya kulevya katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Inadaiwa Matata alikamatwa na polisi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Machi 17, mwaka huu, saa 8.25 usiku akitokea nchini Brazil.
Baada ya kukamatwa alitoa pipi 102 za madawa hayo. Alipofikishwa gerezani hapo, inasemekana mtuhumiwa huyo hakuwa na hali nzuri kiafya, jambo lililofanya awekwe chumba cha mahabusu wagonjwa ili aweze kufuatiliwa kwa karibu na madaktari.

Mashujaa Udugu Matata aliyekuwa na madawa ya kulevya.
“Kesho yake asubuhi kuna mfungwa alikwenda kufanya usafi katika chumba hicho, wakati anachukua takataka, akaitwa na Matata na kumuomba achukue mzigo uliofungwa kwenye karatasi ambao ulikuwa unanuka kinyesi, akamweleza ampelekee mahabusu mwenzake anayeitwa Abbas Gede,” kilisema chanzo chetu.
Inasemekana Gede ni rafiki wa Matata ambaye naye ana kesi ya ‘unga’ na kwamba awali waliwahi kuishi pamoja Brazil.
Kutokana na sheria kutoruhusu mfungwa kuonana na mahabusu, alilazimika kumpatia mahabusu mwingine ili aufikishe mzigo huo, lakini badala ya kuufikisha, mahabusu huyo aliambiwa na rafiki zake kuwa unga huo ni wa mamilioni ya shilingi, hivyo asubiri awape ndugu zake wakija kumpelekea chakula.
Kamishina Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Minja.
Hata hivyo, akiwa katika harakati za kutaka kuwapa ndugu zake, askari wa magereza walimkamata na alipoulizwa alikoyatoa, alimtaja Matata na hivyo kufanikisha kukamatwa kwa wote waliohusika na mzigo huo.
Mkuu wa gereza hilo, Sena Shida amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa watu wote waliohusika wataadhibiwa. “Kwa upande wake, Matata ataadhibiwa mara atakapopata nafuu kulingana na sheria ya mwaka 1967, huo unga tumeuchoma moto,” alisema Shida.
Naye Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Godfrey Nzowa alipoulizwa alikiri kukamatwa kwa Matata na kwamba alitoa pipi 102.
Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Godfrey Nzowa.
Awali walijua kuwa zimeisha hata hivyo, Nzowa alisema alimwagiza mkuu huyo kuyapeleka madawa hayo ofisini kwake, akashangaa kusikia yalichomwa. Aidha, alisema aliwasiliana na mkuu huyo wa gareza ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo ingawa hakuweza kutoa ripoti kituo cha polisi kama ilivyo taratibu.
Taarifa zilizopatikana ndani ya jeshi la polisi zinadai kuwa, Matata aliwahi kukamatwa mwala 2007 kwa tuhuma ya kusafirisha madawa ya kulevya na kufikishwa mahakamani na alikuwa chini ya uangalizi wa jeshi hilo na wakati huo alikuwa hajabadili jina, aliitwa Abdallah Mauri Kaikai.
Kamishina Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Minja aliwahi kuufumua uongozi wa Gereza la Keko kutokana na tuhuma za kuwepo biashara ya madawa ya kulevya ndani ya gereza hilo

MAGAZETI YA LEO APRIL 1, 2014

i

.
.
Ni utaratibu wa millardayo.com kila siku kukupa nafasi ya kusoma kurasa za mwanzo na mwisho za magazeti mbalimbali ya Tanzania.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

.
.
.
.