YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Thursday 20 March 2014

MAGAZETI YA LEO MARCH 20, 2014


.
.
Ni utaratibu wa millardayo.com kila siku kukupa nafasi ya kusoma kurasa za mwanzo na mwisho za magazeti mbalimbali ya Tanzania.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

SIKILIZA NYIMBO MPYA YA YOUNG KILLER "My Power"

s

killerHuu ni wimbo mpya wa Young Killer ambao ameutoa leo rasmi leo March 20 unaitwa My Power ni single ya nne  baada ya Dear Gambe,Jana na leo,Mrs.Super Star na hii My Power ambayo zote zimefanywa Classic Sound chini ya Producer Mona Gangstar.
Bonyeza play kusikiliza.


NJEMBA MOJA YAKAMATWA LIVE IKILA URODA NA MWANAFUNZI KWENYE GARI LAKE





Jamani haya Magari yetu yamegeuka kuwa Gesti House siku hizi, Maana haka kamchezo kameshamiri hapa jijini Dar ...Hiki ndicho kilichomkuta njemba huyu Baada ya kunaswa akila Uroda na mwanafunzi kwenye gari yake.

UPDATES OF MISSING MALYSIA AIRLINE: MABAKI YANAYODHANIWA KUWA NI YA NDEGE YA MALYSIA YAONEKANA NCHINI AUSTRALIA



"The Malaysian prime minister has confirmed that there is a new lead in the investigation into the missing Malaysia Airlines flight MH370.
Australian search aircraft are investigating two objects spotted by satellite floating in the southern Indian Ocean that could be debris from a Malaysian jetliner missing with 239 people on board, Prime Minister Tony Abbott said on Thursday.

"I can confirm we have a new lead," Malaysian Transport Minister Hishammuddin Hussein told reporters in Kuala Lumpur, where the investigation into the missing airliner is based.

"I am meeting the Australian delegation now," he added. we are waiting for some information."

Another official in Malaysia said investigators were "hopeful but cautious" about the Australian discovery. The satellite images were being reviewed and they were awaiting visual confirmation, the source said.

No confirmed wreckage from Malaysia Airlines Flight MH370 has been found since it vanished from air traffic control screens off Malaysia's east coast early on March 8, less than an hour after taking off from Kuala Lumpur for Beijing.

"New and credible information has come to light in relation to the search for Malaysia Airlines Flight MH370 in the southern Indian Ocean," Abbott told the Australian parliament.

"The Australian Maritime Safety Authority (AMSA) has received information based on satellite imagery of objects possibly related to the search."

"Following specialist analysis of this satellite imagery, two possible objects related to the search have been identified," he said.

Abbott said he had already spoken with his Malaysian counterpart Najib Razak and cautioned that the objects had yet to be identified.

"The task of locating these objects will be extremely difficult and it may turn out they are not related to the search for MH370," Abbott said"

NEW! CHUO CHA MADINI, MWANZA KINATANGAZA NAFASI ZA MASOMO.

Chuo cha madini ndani ya Jiji la mwanza kinakuletea kozi za madini ma mafunzo ya Hoteli na Utalii sasa kinatangaza nafasi za masomo katika kozi za madi na mafunzo ya hotel na utalii.


Ada ni nafuu na huduma ya Hostel pia na mafunzo kwa vitendo hutolewa na chuo. Karibuni nyote nafasi  ni chache.

NEW EVENTS.

Hallow people...file:///C:/Users/user/Desktop/DDDDDDD.htm

Wednesday 19 March 2014

ASIA DARWESH DADA MPIGA KINANDA AMBAYE KAACHA REKODI YA PEKEE TOKA ALIPOFARIKI 1995



Asia Darwesh kwenye kinanda pembeni yake ni Johnny Rocks kwenye drums. Haba wakiwa Bandari Grill- New Africa Hotel-enzi za Ngoma za magorofani
MAKALA HII IMEANDIKWA NA MWANDISHI  FRED MOSHA
Jina Asia Daruwesh, sio jina geni kwa mashabiki wa muziki Tanzania na pengine Afrika mashariki kwa ujumla. Huyu Dada anaweza kutajwa kama mpiga kinanda wa kwanza kabisa mwanamke kuwahi kutokea kwenye rhumba letu la kitanzania ingawa siku za nyuma kuliwahi kuwa na bendi ya akinamama watupu ikiitwa Women Jazz ambayo kuanzia magitaa, masaxphones na kuimba walikuwa akinamama watupu. Asia Daruwesh alizaliwa mwaka 1964. Ingawa alikuwa na asili ya Zanzibar, maisha yake kwa kiasi kikubwa yalikuwa Zambia kuanzia utotoni hadi anakua na huko ndiko alikopata inspiration ya kuwa mwanamuziki. Kwa hapa kwetu Tanzania, jina la Asia Daruwesh lilisikika kwenye safu ya mwanzo kabisa ya King Kikii mwaka 1984 akiwa na Kikii mwenyewe, Mumba Kisi, Kapelembe Coco, Samba Wa Mikalay, Zahoro Bangwe, Mohamed Idd Control, Matei Joseph na wengine. Alishiriki kupiga kinanda kwenye nyimbo kadhaa za bendi hii iliyokuwa ikitumia mtindo wa Embalasasa Shika Break kama Kinyume, Dodoma Capital, Njimina, Mimi na we, Kibwanange, Malalamiko na nyingine kadhaa huku nyimbo kama Lamanda na Kitoto chaanza tambaa akimuachia Ally Hemed Star huyuhuyu ambaye leo anajulikana kama muimbaji na mtunzi mzuri wa Taarab. Hata hivyo mwaka 1986 mwishoni aliihama bendi hiyo na kujiunga kwenye safu ya mwanzoni ya MK Group wakati huo. Nyimbo karibu zote za kuanzia toleo la kwanza hadi la tatu la MK Group amepiga kinanda yeye. Hassan Rehani sijui anakumbuka nini ukimtajia MK Group!! Mwaka 1989 alikuwa miongoni mwa wanamuziki wanne walioihama MK Group na kwenda kuasisi Bicco Stars. Angekuwemo na Joseph Mulenga katika group hii lakini alirudi nyuma. Akiwa Bicco aliungana na akina Kinguti System, Fresh Jumbe, Athuman Cholilo Mashida, Seif Rengwe, Sid Morris, Mafumu Bilal, Andy Swebe Ambassadeur na wengine Katika bendi hii ndiko alikotunga wimbo wake wa kwanza wa Bwana Kingo na pia akashiriki kuimba na ameimbisha wimbo huo. Mwaka 1992 alianzisha bendi yake mwenyewe akiita Zanzibar Sound ikitumia mtindo wa Wesaka Dance akiwa na akina Bob Gad William, Hezron Ludala ama Bob Ludala, Fariala Mbutu, na baadaye akina Mohamed Idd Control na Shaban Lendi. Wimbo Banana ambao baadaye Bob Gad alikuja kuurudia akiwa na Twanga Pepeta ulirekodiwa kwa mara ya kwanza na bendi hii. Aidha wimbo Hadija ambao Fariala alikuja kuurudia na Kilimanjaro Connections ulirekodiwa nao huku Ludala akiwa muimbaji Kiongozi. Kufariki dunia kwa Asia Daruwesh ama kwa jina la utani Super Mama mwaka 1995 ndiko kulikohitimisha safari ya bendi hii. Ni hayo tu

URAFIKI JAZZ BAND 1




                                                                  
Pichani toka kushoto waliosimama-Hamis Nguru-mwimbaji, Marifa Ramadhani-Tumba, Juma Saidi- Maracas, Abas Lulela-Bass, Abasi Said -Saxophone, Fida Said-Saxophone, Mohamed Bakari (Churchill)-rythm, Juma Mrisho(Ngulimba wa Ngulimba)-Mwimbaji na Kiongozi wa Bendi.Waliokaa Michael Vicent-Solo gitaa, Ezekiel Mazando-Rythm, Juma Ramadhani Lidenge-second solo na Ayub Iddi- Bass
Bendi ya Urafiki (Urafiki Jazz Band), ilianzishwa mwaka 1970 na kiwanda cha nguo cha Urafiki kilichopo Ubungo. Jina rasmi la kiwanda lilikuwa ni FRIENDSHIP TEXTILE MILL. Kiwanda kilijengwa kwa msaada wa watu wa Jamhuri ya China na kwa urafiki huo kilipewa jina la Friendship Textile. Bendi ilianzishwa ili kutangaza bidhaa hasa Khanga na Vitenge za kiwanda hiki kwani wakati huo kulikuwa na viwanda vingine kadhaa vya nguo nchini kama vile Mwatex, Mutex, Kilitex, na kadhalika


Meneja Mkuu wa kiwanda cha Urafiki Bw. Joseph Rwegasira aliubariki mpango huo wa kuanzishwa bendi ya dansi ya kiwanda na hivyo aliidhinisha malipo ya hundi ya Shs. 50,000/= kununulia seti ya vyombo vya muziki kutoka katika duka la Dar Es Salaam Music House ambalo mpaka leo lipo katika mtaa wa Samora Avenue – Dar Es Salaam.

Ili kupata kundi lililo bora, Menejimenti ya kiwanda cha Nguo cha Urafiki ilimuajiri Juma Mrisho Feruzi maarufu kwa jina la Ngulimba wa Ngulimba na kumuagiza atafute wapigaji kutoka popote ili kuunda kundi imara.. Katika kuhakikisha bendi hiyo mpya inasimama, Ngulimba alichukua wapigaji watano kutoka Orchestre African Qwillado, bendi ambayo aliipigia kabla ya kuanza Urafiki. Na hii ndio maana nyimbo za mwanzoni za Urafiki Jazz Band zilionekana kama zina mahadhi ya Orch. Qwillado.

Wanamuziki aliowachukua Ngulimba kutoka Orch. Qwillado walikuwa ni Michael Vincent Semgumi, mpiga gitaa la Solo, Ayoub Iddi Dhahabu – Besi, Abassi Saidi Nyanga – Tenor Saxophone na Fida Saidi, Alto Saxophone. Ngulimba yeye akawa Muimbaji na pia Kiongozi wa Bendi.

Wanamuziki wengine wa mwanzo ambao waliungana na hao watano waliotoka Orch. Qwillado ambao tayari walikwisha ajiriwa kiwandani Urafiki, walikuwa – Juma Ramadhani Lidenge – Second Solo, Mohamed Bakari Churchil – gitaa la kati (rhythm), Ezekiel Mazanda – rhythm, Abassi Lulela – Besi, Hamisi Nguru – Muimbaji, Mussa Kitumbo – Muimbaji, Cleaver Ulanda – Muimbaji, Maarifa Ramadhani – Tumba, Juma Saidi – Manyanga (maraccass) na Hamisi Mashala – mpiga drums.

Mtindo walioanza nao Urafiki ulijulikana ‘Mchaka Mchaka’ na baadae ukabadilika na kuwa ‘Chaka Chua’ na hatimae mwisho mwisho bendi inaelekea ukingoni walipiga mtindo wa ‘Pasua’ na ‘Patashika’

Mwaka 1971 Gidion Banda, mwanamuziki kutoka bendi ya Morogoro Jazz alijiunga na kundi akiwa mpigaji wa Saxophone.

Aidha, Bendi ya Urafiki ilipitiwa na wanamuziki wengi baadhi wakiwemo Gideon Banda mpuliza saxophone kutoka Morogoro Jazz wengine wakiwemo Thobias Cosmas Chidumule na Frank Mahulu – Waimbaji waliotokea Western Jazz (Saboso) mwaka 1973 na kuongeza nguvu katika safu ya uimbaji. Waimbaji hao walishiriki nyimbo nyingi baadhi zikiwa Tausi Karuka, Jembe na Panga (Geza Ulole), Kosa la Nani, Mauaji ya Soweto, Rukia Hukusikia, Maonyesho ya Mtu Mweusi n.k.

Pia waliongezeka Mkali na Hidaya kutoka Morogoro wakipuliza matarumbeta, hao walikuja 1973 na Ali Saidi alietokea Cuban Marimba akipiga gitaa la kati (rhythm) na baadae mwaka 1975, Mganga Hemedi kutoka Tanga, akitokea Atomic Jazz, nae alijiunga na kuwa upande wa solo na rhythm.

Urafiki Jazz imetunga nyimbo nyingi, zaidi ya mia tatu zinazoelekeza kwenye siasa, mapenzi, nasaha na mafundisho na pia kukosoa. Baadhi ya nyimbo zake za siasa zilizopata umaarufu ni kama zile Mwenyekiti Nyerere, Mauaji ya Soweto, Jembe na Panga n.k..

Mwaka 1975 Bendi ilishiriki katika mashindano ya bendi za muziki wa dansi yaliyofanyika Mnazi Mmoja – D’Salaam na kushika nafasi ya tatu na Mzee Ngulimba, kama Kiongozi wa Urafiki aliiwakilisha Tanzania pamoja na bendi ya Afro 70 iliyopata nafasi ya kwanza na baadhi ya vikundi vya utamaduni kutoka Tanzania Bara na Zanzibar nchini Nigeria katika maonyesho ya mtu mweusi yaliyofanyika huko.

UNAWAKUMBUKA HAWA, URAFIKI JAZZ BAND 2


Urafiki Jazz Band
Bendi ya Urafiki ikiwa katika hali yake ya uchanga mwaka 1970 ilipata ajali ya gari, wakati kundi zima likitoka katika onyesho huko Chang’ombe, gari lao aina ya Volkswagon Kombi liligonga mti maeneo kona ya Kigogo na Msimbazi Mission.
Baadhi ya wanamuziki waliumia sana na gari lao, likawa halifai kabisa.
Wapigaji walioumia walikuwa ni Hamisi Mashala – Drummer Boy - alivunjika mguu, Mohamed Bakari Churchil aliumia kichwani na kushonwa nyuzi kadhaa, na pia Ayoub Iddi Dhahabu na Maarifa Ramadhani walipata maumivu makali kwa ndani mwilini.

Bendi ilisimamisha maonyesho yake kwa muda hadi wanamuziki wake walipopata nafuu na kuanza maonyesho tena. Hali ya ajali ile ilileta fikra mbaya kwa wanamuziki hao na wapenzi wao na ilionekana kana kwamba kulikuwa na mkono wa mtu katika ajali ile. Juma Mrisho ‘Ngulimba’ alitunga wimbo ‘Nimekosa Nini Jama’, wimbo ulioelezea kadhia hiyo. Katika kipindi hiki dhana ya ushirikina ilitawala sana katika bendi mbalimbali. Vifo vya wanamuziki mara nyingi vilihusishwa na upinzani katika bendi. 
Kufikia miaka ya ‘80’ kati bendi ya Urafiki ikawa inasua sua kutokana na uchakavu wa vyombo na Menejimenti iliyokuwepo wakati huo haikuwa tayari kutoa pesa kununulia vyombo vipya. Bendi ya Urafiki ilifikia tamati katika miaka ya ‘80’ kati kati na bendi hiyo ikatoweka katika anga za muziki na kubaki historia.