YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Thursday 13 March 2014

DALADALA ZINAZOELEKEA CHUO KIKUU CHA UDOM ZAGOMA KWA SAA NNE(4)


 Wakazi wa maeneo ya Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiwa wamejazana katika kituo cha Daladala cha Jamatini mjini hapa wasijue cha kufanya baada ya Madereva wa Magari hayo kugoma kwenda njia hiyo wakishinikiza kusimamisha abiria wanapopakia.
 Wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiwaza jinsi ya kusafiri
mpaka maeneo ya Makulu, Chimwaga na Ng'ong'onha baada ya wenye Daladala
kugoma kutokana na kile walichodai ni kukamatwa mara kwa mara na polisi
wa usalama barabarani wakitakiwa kutojaza kupita kiasi.


Magari yanayosafirisha abiria yakiwa yameegeshwa pembezoni ya Bohari ya mkoa baada  ya madereva wa magari hayo kugoma  kutoa huduma ya usafiri kwa njia ya UDOM kwa madai ya kuonewa na Askari wa barabarani mara kwa mara katika njia hiyo japo Kamanda wa Polisi Usalma Barabarani  Boniventura Nsokolo kudai polisi hawatashindwa kuwakamata kama watawaona wakivunja sheria.
 Wanafunzi hao wakaamua kutumia usafiri wa pikipiki baada ya kuona mambo ni magumu huku wakishikiza kuwavaa wahusika.

 Na John Banda, Dodoma

MADEREVA wa Daladala zinazoenda Chuo Kikuu cha Dodoma [UDOM] manispaa ya Dodoma leo wamegoma kutoa huduma hiyo kwa zaidi ya saa 4 hali iliyosababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi wa maeneo hayo.

Mgomo huo ulioanza majira ya saa 7 mchana ulianza kama mdhaha tu mara baada ya abiria waliokuwa katika kituo hicho kujiuliza maswali yasiyo na majibu baada ya kuona makonda wa Daladala hizo wakikufunga milango na kuwakataza wasiingie na kama haitoshi wakaamuru madereva wao wayaondoe kituoni hapo.


Madereva hao ambao walipoyaondoa magari waliyapeleka kuyaegesha maaneo ya Bohari walisema waliamua kufanya hivyo kutokana na kusumbuliwa mara kwa mara na polisi wa usarama barabarani kutokana na kusimamisha abiria.

Walisema wanashangazwa na kitendo hicho kinachofanyika na polisi wa Dodoma pekee kinyume na mikoa kama ya Mwanza, Arusha, Mbeya na hata Dar es laam ambako wanapakia watakavyo na hakuna wa kuwauliza.

Waliongeza kuwa vitendo hivyo wanavyofanyiwa vya kuzuiliwa kusimamisha abiria ni kuwatia hasara kutokana na kukosa abiria pindi wanapokuwa wakitokea UDOM ilihali sehemu yenyewe ni mbali huku mafuta yakiwa juu.

Kwa upande wake Mkuu wa polisi wa usalama Barabarani Wilaya Boniventura Nsokolo alisema kila Dereva aangalie leseni yake inamruhusu kupakikia kiasi gani, na wao kama polisi hawawezikuona Dereva akivunja sheria harafu wakamuacha bila kumchukulia hatua.

''Lazima tuwakamate kama wakivunja sheria za Barabarani kwani kila mtu ana leseni na inamuongoza apakie abiria wanagapi na kwenye kila mkoa kuna utaratibu kutokana na kitengo husika kinachosimamia na kutoa leseni hivyo ni vizuri kufuata utaratibu'', alisema Nsokolo

Tuesday 11 March 2014

YALIOANDIKWA KATIKA MAGAZETI YA LEO TAREHE 12/3/2014

.
.
Ni utaratibu wa millardayo.com kila siku kukupa nafasi ya kusoma kurasa za mwanzo na mwisho za magazeti mbalimbali ya Tanzania.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
mg28-w480-h580
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

NMB WAAMUA KUSAIDIA VIJANA KWA KUFANYA HAYA,

three wheeler 1Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni tatu yaani Fair Deal Auto Private Ltd inayosambaza pikipiki za miguu miwili na mitatu aina ya Bajaji,kampuniyaCar & General Limited Ltd inayosambaza pikipiki za miguu mitatu aina ya TV’S King pamoja na kampuni ya Quality Motors inayosambaza pikipiki za miguu miwili aina ya Honda wameingia ubia ili kuwawezesha wananchi kupata mikopo nafuu ya kumiliki pikipiki za miguu miwili na mitatu.
NAGU 4Hii yote ni katika kuendeleza azma ya NMB inayolenga kubuni huduma na bidhaa mbalimbali za kibenki zinazogusa kwa karibu mahitaji ya wateja na watanzania kwaujumla.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mikopo hii jijini Mwanza,Waziri waUwezeshaji naUwekezaji kutoka ofisi ya Waziri Mkuu,Mhe.Dkt.Mary Nagu amesema>>’Mikopo hii ya pikipiki itawasaidia sana vijana na wananchi kwa ujumla kuweza kumiliki pikipiki zitakazowawezesha kuendesha maisha yao ya kila siku. Binafsi natambua ajira kwa vijana imekua ni changamoto maeneo mengi nchini hivyo basi ningependa kuwasisitiza vijana wachukue fursa hii inayotolewa na NMB kuweza kumiliki biashara zao wenyewe na kujikimu kiuchumi‘.
Vile vile kutoka NMB Mkuu wa Kitengo cha Biashara za kibenki Bw.Filbert Mponzi amesema kuwa bidhaa hii mpya inalenga kupunguza changamoto za ajira kwa vijana hapa nchini.
Marejesho ya mkopo huu wa pikipiki ya miguu miwili na mitatu yanatolewa ndani ya muda wa miezi 24 ambapo kwa kipindi hiki chote, mteja ataendelea kurejesha makato yake ya kila mwezi kwa kuzingatia taratibu za makubaliano yatakayofanyika baina ya mteja na benkiya NMB.
Mikopo hii pia inawekewa bima kwa ajili ya ulemavu au kifo kitakachomtokea mmliki wa pikipiki iliyochukuliwa mkopo,bima hii ni kwaajili ya kumpa unafuu mkopaji endapo atapata matatizo ya kiafya ambayo yatamfanya apate ulemavu au kupoteza maisha.
NAGU 6Kwa maelezo zaidi tembelea matawi ishirini na moja tu ya NMB nchi nzima yanayotoa mikopo hii,matawi hayo kwa Mwanza-Buzuruga na Kenyata Road,Dar es Salaam-Tegeta,Magomeni,Mwenge,Mbezi Beach, Temeke, Ilala,Mlimani City,Msasani na Airport,Arusha-Clock Tower na Arusha Market,Manyara-Babati naKatesh,Dodoma,Mbeya-Mwanjelwa,Mbalizi Road naUsongwe,Moshi-Nelson Mandela na Tanga-Madaraka

TAZAMA PICHA NYINGINE ZA AJALI YA BASI LA HOOD ILIYOTOKEA LEO ASUBUHI HUKO MKOANI KILIMANJARO WILAYA YA SAME




KATIKA AJALI ILIYOTOKEA LEO ASUBUHI MAENEO YA SAME KATIKA KIJIJI KATI YA MGAGAO NA NJARO AMBAPO UNAAMBIWA
HAKUNA MTU ALIYEPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI HIYO ILA WAPO WALIOUMIA VIBAYA AMBAPO MAJERUHI WAPO KATIKA HOSPITAL YA WILAYA YA SAME



MATUKIO KATIKA PICHA 

Monday 10 March 2014