YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Thursday 31 July 2014

AIBU KWA TAIFA: MSANII ANASWA CHINA NA MADAWA YA KULEVYA


HUKU modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’, akisota jela nchini China kwa skendo ya kukamatwa na madawa ya kulevya (unga), mrembo mwingine ambaye aliwahi kujaribu kuchomoka kisanii kwenye muziki wa Kizazi Kipya almaarufu kwa jina la Winnie Mandela, naye amenaswa na polisi nchini humo.
Mrembo almaarufu kwa jina la 'Winnie Mandela' katika muziki wa kizazi kipya akiwa amenaswa na polisi China.

Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kupitishwa kwa msako maalum wa kutokomeza biashara hiyo katika viunga vya Mji wa Hong Kong, China.
JUX, PETIT MAN WAPATA WAKATI MGUMU
Kwa mujibu wa chanzo chetu chenye maskani yake Hong Kong, Mbongo Fleva, Juma Khaleed ‘Jux Vuitton’ na meneja wa msanii wa Bongo Fleva aitwaye Mirrow, Petit Man nao walijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kunusurika kuunganishwa kwenye oparesheni hiyo ya ukamataji wa waingizaji wa madawa ya kulevya nchini China.

'Winnie Mandela' wa muziki wa kizazi kipya Bongo akiwa chini ya ulinzi mkali China.

MADAI YA KUBEBA UNGA
Ilidaiwa kwamba Winnie alijikuta mikononi mwa askari wa China akidaiwa kubeba mzigo wa unga tumboni hivyo kukamatwa na kutembezwa mitaani kuelekea kituo cha polisi.

APITA VIZUIZI, AKAMATWA
Ilisemekana kwamba Winnie ambaye ni msichana wa mjini Dar, alifanikiwa kupita vizuizi vyote lakini kwa hali ilivyo kwa sasa nchini humo ndipo akajikuta akikamatwa na kutembezwa mtaani kama mhalifu wa kivita.

“Unaambiwa ilikuwa kama vita kwani polisi wa China huwa wana silaha za kutisha sana. Unajua Winnie alikamatwa kwenye mitaa ambayo kuna Wabongo wengi hapa Hong Kong,” kilisema chanzo chetu kutoka Hong Kong.
Ilidaiwa kwamba askari hao walipokea agizo maalum kutoka kwenye kitengo cha kudhibititi madawa ya kulevya nchini humo kwani kwa sasa nchi hiyo imechafuka kwa uingizwaji wa madawa ya kulevya, jambo ambalo limeifanya serikali ya China ifanye oparesheni kubwa ya kuhakikisha wanatokomeza wimbi hilo.
KWA WABONGO CHINA
Chanzo chetu kilisema kwamba kwa sasa Wabongo wanaokwenda au wanaokaa China wanaishi kama digidigi kwani wamefikia hatua ya kutoonesha pasipoti  zao na hata wengine wanadiriki kukataa uraia wao kwa kuwa Wabongo ndiyo wanasakwa kwa wingi.

“Sasa hivi jamaa wakisikia huyo ni Mtanzania wanamfuatilia sana kwani ndiyo wenye sifa ya uingizaji wa dawa za kulevya nchini China,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
KAMA HUAMINI MUULIZE JUX AU PETIT MAN
“Hicho ndicho kilichomtokea Winnie. Nakwambia Wabongo wanazidi kukamatwa na madawa ya kulevya. Yaani ni aibu, huwezi kuamini.

“Wabongo wengi sana wamekamatwa Hong Kong na wengine familia zao Bongo hazijui.
“Kama Watanzania hawaamini wawaulize Jux na Petit Man ambao walishuhudia mtiti mwanzo mwisho.”

BALOZI WA TANZANIA CHINA
Ili kupata undani na idadi ya Watanzania wanaokamatwa kwa ishu za madawa ya kulevya nchini China, gazeti hili lilimtafuta Balozi wa Tanzania China, Luteni General Abraham Shimbo ambapo simu yake ya ofisini iliita bila kupokelewa.

Wakati Jack Patrick akisubiri kupandishwa kizimbani kwa mara nyingine mwezi ujao, ripoti zinaonesha kwamba wapo Watanzania wengi waliofungwa na wengine kunyongwa kwa msala wa madawa ya kulevya

DUNIANI KUNA MAMBO JAMANI, UNAAMBIWA MISUKULE YA GWAJIMA YATINGA POLIS... NDUGU WATHIBITISHA KUHUSU VIFO VYAO




msukule1

Baada  ya  hivi  karibuni  kutoa  waraka  mzito  unaowalenga  watumishi  wa  mungu  kwa  kile  alichodai  kuwa  ni  ukiukwaji  wa  sheria  za  mungu, Nabii Hosea  Chamungu  ametangaza  rasmi  kuiwasilisha  ripoti  ya  misukule  feki  mikononi  mwa  jeshi  la  polisi  ili  hatua  za  kisheria  zichukuliwe…
.
Akiongea  kwa  kujiamini, Nabii  Cha Mungu  alimuonyesha  mwandishi  baadhi  ya  picha  za  misukule  ikiwmo  iliyowahi  kuonyeshwa  ndani  ya  kanisa  la  ufufuo  na  uzima  linaloongozwa  na  mchungaji  Josephat  Gwajima…..
“Unapofanya  kazi  ya  mungu  hutakiwi  kuwa  mwoga  kwa  lolote  kwani  yeye  ndiye  anayetulinda  sisi  sote, kondoo  wa  bwana  wamekuwa  wakipotea  siku  hadi  siku  huku  wachungaji  tukiwaangalia  bila  kuwaokoa.Mimi  sikubaliani  na  hii  miujiza  ya  kutoa  misukule  inayotangazwa  kila  siku  wakati  hatujui  hao  misukule  walifia  wapi….
msukule1
“Baada  ya  kufunuliwa  na  mungu  juu  ya  jambo  hili, nimeanza  kukusanya  taarifa  kuhusiaa  na  hili  jambo  na  tayari  uelekeo umeshapatikana, watu  hawataamini  siku  nitakapoliweka  wazi  hili  suala  kwani  nitaliomba  jeshi  la  polisi  liwashitaki  wote  waliorubuniwa  na  kujifanya  misukule  pamoja  na  wale  walioinjinia  ishu  nzima.Kama  kuna  watu  wenye  uwezo  wa  kufufua  watu  kwa  nini  vifo  vinaendelea  kutokea  kila  siku?”,alisema  Cha Mungu
Cha  Mungu  alidai kuwa  zoezi  hilo  litafikia  hitimisho  mwishoni  mwa  mwezi  ujao.
Aidha, alitoa  wito  kwa  ndugu, jamaa  na  wazazi  ambao  kwa  namna  moja  au  nyingine  wamehusika  na  kuficha  siri  za  ndugu, jamaa  au  watoto  wao  waliojihusisha  na  zoezi  la  kumdhihaki  Mungu  la  kujifanya  wao  ni  misukule  wangali  wakijua  si  kweli  wajisalimishe  kabla  hajawaumbua….
msukule
“Nitakapokamilisha  details  nitawataja  kwa  majina, mahali  walipo  na  jinsi  walivyohusika, kwa  wale  ambao  wanaogopa  vitisho  waje  nitawaombea  na  roho  ya  woga  itaondoka  na  hakuna  atakayewadhuru,” alisema
Jitihada  za  kumpata  mchungaji  Gwajima  kuongelea  suala  hilo  ziligonga  mwamba  kutokana  na  simu  yake  kutopatikana.

AIBU KUBWA HII: MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI AFUMWA AKILIWA URODA GESTI MCHANA KWEUPE


Askari wa jeshi la polisi na wasamaria wema wakiwa wamemdhibti binti anayedaiwa kuwa ni mwanafunzi wa darasa la saba moja ya shule ya msingi Manispaa ya Morogoro,
binti huyo anadaiwa kukurupushwa katika moja ya nyumba ya kulala wageni eneo la Mawenzi wakati akipelekwa kituo kidogo cha polisi. Kwa kile kinachodaiwa kujihusisha na mapenzi na masomo.
Wasamalia wema wakiwa wamemdhibti binti anayedaiwa kuwa ni mwanafunzi wa darasa la saba Manispaa ya Morogoro baada ya kumnusuru na kipigo

Sunday 27 July 2014

RAIS KIKWETE ATUNUKU WAHITIMU WA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI KATIKA MAHAFALI YA KOZI YA PILI


 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Kanali
James Ruzibiza Stashahada ya Usalama na Stratejia (Diploma in Security
and Strategic Studies) katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa
cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai
26, 2014. Kanali Ruzibiza, ambaye anatokea Rwanda, ni mmoja wa washiriki
tisa wa kozi waliotoka nchi za nje. Washiriki wengine kutoka nje y nchi
walitoka Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Uganda, zambia na Zimbabwe.
Jumla ya wahitimu 30, wakiwemo maafisa wandamizi katika utumishi wa
umma, ambapo 11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine vya usalama na idara mbalimbali. 
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Luteni Jenerali
C.L. Makakala Shahada ya Uzamili ya Falsafa ya Usalama na Stratejia
katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC)
chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014. Luteni
jenerali Makakala, ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi wa
kwanza, amekuwa mtunukiwa wa kwanza wa Shahada hiyo hapo chuoni.
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia baada ya kutunuku shahada katika  mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi  (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014.Jumla ya wahitimu 30 wamehudhuria kozi hiyo wakiwemo maafisa wandamizi katika utumishi wa umma, ambapo 11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine  vya usalama na idara mbalimbali. Washiriki wengine tisa wametoka  nchi  za nje ambazo ni Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Rwanda Uganda, Zambia  na Zimbabwe.
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaambia kuwa sasa ni
zamu yao kupiga picha ya kumbukumbu bila yeye wahitimu wa Kozi ya Pili
ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es
salaam leo Julai 26, 2014.

NEWS ALERT : BASI LA HOOD LAPATA AJALI MBAYA ASUBUHI HII LIKITOKEA MBEYA


Muda mchache baada ajali kutokea 
 Askari wa usalama wa barabarani wakiwa wamefika eneo la tukio  na baadhi ya Mashuhuda wakishuhudia ajali hiyo
 Basi la Hood limepata ajali asubuhi hii likitoka Mbeya haijafahamika mara moja lilikuwa linaelekea wapi na haijafahamika kama kuna watu waliojeruhiwa, endelea kufutilia hapa kupata taarifa kamili hii ni taarifa ya awali. Picha na Mbeya yetu Blog

MWIMBAJI BAHATI BUKUKU APATA AJALI MBAYA YA GARI


Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba, mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili hapa nchini, Bahati Bukuku amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kupata ajali mbaya katika eneo la Kongwa, mkoani Dodoma usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, mwimbaji huyo alipata majeraha makubwa sehemu mbalimbali mwilini na kwamba chanzo cha ajali hiyo kinadhaniwa kuwa ni mwendokasi.
Chanzo hicho hakijaweza kueleza zaidi kwamba Bukuku alikuwa akielekea ama kutoka mkoani Dodoma na kama ndani ya gari hilo kulikuwamo na abiria wengine.
Pia haikuweza kufahamika mara moja kama mwimbaji huyo alikuwa akiendesha mwenyewe gari hilo, ingawa kilithibishwa ajali hiyo na kwamba Bukuku alijeruhiwa vibaya.
Endelea kuperuzi blogu hii kwa habari zaidi ya tukio hilo.

DUNIA HAIISHUI VITUKO:KUTANA NA BINTI ALIEOMBA KU-DATE NA UHURU KENYATA....WALINZI WAKAMBANIA...SOMA STORY NZIMA HAPA


Binti huyu ni rafiki wa Uhuru Kenyatta  huko Facebook..sasa alimuomba KU-DATE na kupitia hukohuko FB na kukubaliwa..SOMA  HAPO CHINI ISHU ILISHINDIKANA VIP...
SOMA HAPA