YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Thursday 4 December 2014

MAGAZETI YA LEO IJUMAA 5, December 2014

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC06590
.
.
.
.
.
.
.

Wednesday 3 December 2014

MAZISHI YA MRAKIBU WA POLISI CAPT.KIDAI SENZALA ALIYEFARIKI KATIKA AJALI YA HEKOPTA DAR ES SALAAM


Maafisa wa Polisi wakiwa wamebeba sanduku lililohifadhi mwili wa Marehemu Capt. Kidai Senzala Kalise aliyefariki Novemba 29 mwaka huu katika ajali ya Helkopta iliyotokea Kipunguni B-Moshi Bar Dar es Salaam wakielekea katika makaburi ya familia huko Gonja Maore Wilaya ya Same mkoa wa Kilimanjaro Desemba 1, 2014.

Marehemu Kidai alikuwa Mrakibu wa Polisi na alizikwa kwa heshima zote za Kipolisi ikiwa ni kupigiwa mizinga na saluti mbalimbali za kipolisi kabla na baada ya maziko yake. 

Helkopta aina ya Robertson R44 iliyo tolewa msaada kutoka kwa Taasisi ya Howard G. Foundation inayomilikiwa na mfanyabiashara mashuhuri nchini Marekani Bw. Warren Buffet  ililetwa nchini kwa lengo la kukabiliana na vitendo vya ujangili na kupokelewa nchini na Waziri wa Maliasili na Utalii June 14,  2014 jijini Dar es Salaam na kuikabidhi kwa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) ilipata ajali majira ya saa nne asubuhi baada ya 
kupata hitlafu katika injili yake na kupoteza maisha ya Mrakibu wa Polisi Capt. Kidai Senzala Kaluse, Mkaguzi wa Polisi Capt. Simba Musa  Simba,  Konstebo wa Polisi, Josso Selestine na Capt. Joseph Khalfan wa Malisasili aliyezikwa Arusha.SOURCE: Father Kidevu Blog

Maofisa wa Polisi wakijiandaa kulibeba jeneza la Marehemu Capt Kidai.
 Wanafamilia wakiwa katika gari lililobeba mwili wa mpendwa wao Capt. Kidai Senzala.
 Maofisa wa Polisi wakiwa wamebeba sanduku la Mrakibu wa Polisi-Capt. Kidai.
 Heshima za Kihjeshi zikitolewa kabla ya jeneza kushushwa kaburini na kupigiwa mizinga.
 Heshima zikiendelea...
Ndugu wa marehemu akiwepo mkewe, mama yake mzazi marehemu, dada zake na ndugu wengine wakitafakari kazi ya Mungu baada ya kufanyika kwa mazishi ya Capt. Kidai Senzala.

HABARI PICHAZ: MBUNGE ZITTO KABWE AMTAMBULISHA MCHUMBA WAKE!


 Mh. Zitto Kabwe anayemfuatia ndiye mchumba ake huyo aitwaye Anna!
MBUNGE Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Zuberi Kabwe amemtambulisha mchumba wake mpya anayetarajia kufunga nae pingu za maisha hivi karibuni.

Utambulishio huo wa mchumba wa Zitto ulifanywa na Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila (NCCR-Mageuzi) wakati wa sherehe ya Harusi yake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Annex. 
Hali ilikuwa hivi; baada ya Kafulila kutambulisha ndugu zake pamoja na wazazi wake ndipo alianza kutambulisha wageni wengine na kuanza na mchumba mtarajiwa wa Zitto Kabwe aliyemtaja kwa jina la Anna.

“Huyu wa kwanza anaitwa Anna anafanya kazi Ubalozi wa Ireland ni mchumba mtarajiwa wa Zitto Zuberi Kabwe, anayefuata kutoka kushoto kwa Anna wote mnamfahamu ndiyo Zitto mwenyewe na anayemfuata ni Mwalimu wangu wa chuo kikuu Kitila Mkumbo na mwisho ni mbunge mwenzangu David Silinde hao ndo walio nisindikiza,” alisema Kafulila.