YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Saturday 11 August 2012

Al-Shabaab kuwaua wanachama wake kunaashiria matatizo makubwa



Na Mahmoud Mohamed huko Mogadishu

Julai 30, 2012
Uamuzi wa Al-Shabaab wa kuwaua wanachama wake watatu kwa tuhuma za kupeleleza kwa ajili ya serikali za kigeni kunaonyesha ukosefu wa imani ndani ya vyeo vya kikundi cha wapiganaji, wachambuzi wa kisiasa na waangalizi wanasema
  • Mpiganaji wa al-Shabaab amesimama akilinda wakati mamia ya wakazi wakiangalia adhabu ya kukatwa viungo hadharani. Al-Shabaab hivi karibuni iliwaua wanachama wake watatu kwa tuhuma za kupeleleza kwa niaba ya serikali za kigeni. [Mustafa Abdi/AFP]
    Mpiganaji wa al-Shabaab amesimama akilinda wakati mamia ya wakazi wakiangalia adhabu ya kukatwa viungo hadharani. Al-Shabaab hivi karibuni iliwaua wanachama wake watatu kwa tuhuma za kupeleleza kwa niaba ya serikali za kigeni. [Mustafa Abdi/AFP]
Al-Shabaab ilisema watu watatu -- Ishaq Omar Hassan,miaka 22, Yasin Osman Ahmed,miaka 23, na Mukhtar Ibrahim Sheikh, miaka 33 -- walikuwa wanapeleleza kwa ajili ya Shirika la Upelelezi la Marekani na Shirika la Upelelezi la Uingereza MI6.
"Hassan na Ahmed wote wawili walihusika na vifo vya Bilal al-Berjawi na wengine watatu [wanachama wa al-Shabaab]," shirika hilo linalohusiana na al-Qaeda lilisema katika mtandao wake wa Twitter tarehe 22 Julai. "Wawili hao waliweka vifaa vya ufuatiliaji katika magari ya al-Berjawi & kaka zake ambayo waliyaongoza makombora yaliyoshambulia vitongoji vya Mogadishu."
Al-Berjawi, mwenye uraia wa nchi mbili za Lebanon na Uingereza ambaye alivuliwa uraia wa Uingereza, aliuawa katika shambulio la kombora mwezi Januari nje ya Mogadishu. Iliripotiwa kuwa alikuwa kamanda msaidizi wa al-Qaeda nchini Somalia.
Waliyoshuhudia huko Marka walisema watu hao watatu waliuawa na kikosi chenye silaha katikati ya mji.
"Wapiganaji wa al-Shabaab ilitumia vipaza sauti vilivyofungwa katika malori kuwaita watu kushuhudia mauaji na watu walipokusanyika uwanjani, dazani ya wapiganaji waliyofunika nyuso zao waliwafunga vitambaa machoni watu hao watatu na kisha kuwapiga risasi, wakiwaua hapo hapo," mkaazi wa Marka Mohamed Said, miaka 34, aliiambia Sabahi

Tatizo la Al-Shabaab la kujiamini.

Omar Dahir, mkurugenzi wa Kituo kilichopo Mogadishu cha Marekebisho na Mjadala, alisema matatizo ya al-Shabaab yanatokana na kuongezeka kwa mgawanyiko miongoni mwa wanachama na kunaweza kusababisha kusambaratika kwa haraka kwa kikundi katika siku karibu zijazo.
"Kuna kutojiamini ndani ya al-Shabaab, kwa kuwa kikundi hakiwaamini wanachama wake na sasa viongozi wake hawaaminiani," Dahir aliiambia Sabahi. "Uamuzi wa al-Shabaab kuwaua wanachama wake watatu huko Marka unaonyesha ukosefu wa imani ambao unakikabili kikundi."
"Hii inaweza kuwa mwanzo wa kuvunjika kwa mipango ya mapigano iliyoandaliwa ndani ya kundi hilo, ambalo tayari linasumbuliwa na mgawanyo mkubwa," Dahir alisema.
Alisema al-Shabaab inaweza kukimbilia kuwaua kwa siri wengi wa wanachama wake kwa kuogopa kuwa kufanya mauaji mara mingi mbele ya wananchi kunaweza kuyumbisha umoja wa kundi hilo.
"Kundi hili litamuua mwanachama yeyote anyeshukiwa kuwa na uhusiano na pande za nje kwa sababu wanaogopa kuwa mashirika ya upelelezi ya Ulaya yanaweza kupenyeza kwenye kundi hilo na kuwalenga viongozi wao wanaotakiwa," Dahir said.
Al-Shabaab ilisema katika mtandao wa Twitter kuwa imezindua kampeni kubwa ya kukabili upelelezi ili kusafisha nchi kutokanana na majasusi hao .
Mwaka uliopita , kiongozi wa al-Shabaab Mualim Hashi Mohamed Farah alisema Kitengo cha upelelezi cha Ulaya kimepenyeza kwenye safu ya maaskari wa al-Shabaab, na mawakala wa pande mbili wanaojifanya kuwa wapigananaji wa vita vitakatifu.
Huu sio muda pekee kwa al-Shabaab kuwaua washirika wake waliotuhumiwa kwa kupeleleza kwa niaba ya mawakala wa upelelezi wa Kimagharibi. Al-Shabaab ilimuua makamu wa kiongozi wao mkuu wa upelelezi, Ahmed Ali Hussein, pia anajulikana kama Ahmed Keyse,mwaka 2010 kwa "upelelezi " wa serikali za kigeni.
Tarehe 27 Julai, al-Shabaab ilisema iliwakamata "wapelelezi watatu wa TFG" ambao kwa sasa wanahojiwa. "Kama watatiwa hatiani watu hao watatu watauawa hadharani," al-Shabaab ilisema katika Twitter.

Tuzo yazidisha tatizo ndani kati ya al-Shabaab

"Vurugu za kujiamini zimetawala katika sura ya nchi ndani ya kundi la al-Shabaab,ambazo zimesababisha mauaji ya washirika wake," alisema Abdirahman Mohamud, mwangalizi wa makundi yenye msimamo mkali.
Tangu Marekeni ilipotangaza tarehe 7 Juni kwamba itatoa zawadi ya hadi Dola za Marekeni milioni 33 kwa taarifa zinazowahusu wapi walipo viongozi saba wa ngazi ya juu wa al-Shabaab, viongozi wanaotafutwa wamejificha dhidi ya sio tu kikosi cha upelelezi lakini pia dhidi ya macho ya jamii na washirika wao.
"Viongozi wa al-Shabaab sasa wana wasiwasi kwamba Marekeni kutoa tuzo ya fedha kutasababisha kutoa msukumo kwa baadhi ya washirika wa kundi, ambao watahamasishwa na uroho waa pesa, kuwasaliti viongozi wao na kutoa taarifa kuhusu walipo ili wajipatie zawadi za fedha," Mohamud aliiambia Sabahi.
"Kwa maoni yangu huo ni motisha kwa uamuzi wa al-Shabaab hivi karibuni kuwaua washirika wake watatu kwa tuhuma za kufanya upelelezi kwa niaba ya mawakala wa kipelelezi wa Marekani na Uingereza," alisema.
Mohamud alisema al-Shabaab imegawanyika katika kambi mbili, na kila moja "itafanya ukatili" dhidi ya nyingine.
Mwezi Machi, kiongozi wa al-Shabaab Hasan Dahir Aweys alilaumu kikundi cha wanamgambo kwa kuwaua wananchi bila ya malengo kwa jina la kiislamu na kwa kushirikishwa kwake na al-Qaeda. "
Kundi lenye msimamo mkali la al-Shabaab lilifanya mauaji mengi katika miaka michache iliyopita, yakilenga sio tu washirika wake lakini pia na wananchi wengi wa Somalia waliotuhumiwa wakifanya kazi na upelelezi kwa ajili ya mawakala wa upelelezi wa Kimagharibi au wakishirikiana na majeshi ya serikali ya Somalia au Umoja wa Afrika," alisema Abdullahi Osman, mchambuzi wa masuala ya kisiasa na mtaalamu katika masuala ya vikundi vya waislamu wenye msimamo mkali nchini Somalia.
Osman aliiambia Sabahi kwamba al-Shabaab wanawafanyia ugaidi wananchi wa Somalia na wanatishia kuwaua wale ambao wanashirikiana na serikali au Umoja wa Afrika waliopo nchini Somalia.
Alitoa wito kwa serikali ya Somalia kuimarisha jitihada zao ili kuyakomboa maeneo yaliyobakia chini ya udhibiti wa al-Shabaab kumaliza uhalifu wa kuchukiza unaofanywa na kikundi hicho.
"Al-Shabaab itaendelea kufanya vurugu za kutokuwa na hadhari na kutochagua kwa uangalifu dhidi ya wananchi wa Somalia hadi kundi hilo litakapotolewa nchini," alisema.

TEMBO AVAMIA MAKAZI YA WATU, NAO WAMFAIDI NYAMA.

Hallow people...

STORY KUBWA ZA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI TAREHE 12/8/2012


















5 THINGS YOU NEED TO KNOW ABOUT MITT ROMNEY'S VP PICK

Add caption

TATIZO NI MLEGEZOOO AU NI UWEZO WA KUKUSANYA DATA?S

Sasa hii taharifa inahusiana nini na taharifa zinazohitajika...

M4C YAFANA JANA JIJINI DAR, ZAIDI YA MILIONI 250 CASH ZAPATIKANA.

Mbowe na mlinzi wake

PALE UGWADU UNAPOZIDI HANA BUDI KUAMUA KUTUMI NGUVU ZA ZIADA

Kijana wa mujini akijaribu kumshawishi mtoto wa bushi...

MWANAMKE ALIEJIFUNGUA WATOTO WENGI KULIKO WOTE KWA MPIGO SIKU YA KUJIFUNGUA KWAKE

calvin
Mwanamke ajifungua watoto 11. kwa mpigo....

BORA MWANA AFE LAKINI SIO MIFUGO

Mama wa kiasia akinyonyesha moja ya mifugo yake

KUTANA NA WAPENZI HAWA WA SIKU NYINGI HUKO PORINI.

calviun
Bwana na Bibi deshi deshi deshii..
Inasemekana kwamba hawa wanyama ni kutoka katika bara la Africxa, maana hawa wanaitwa nyani wa kizungu. Sasa waweza kuona jinsi Walivodumu mpaka sasa....

BIASHARA YA MBWA YAPAMBA MO HUKO MAJUUTO

Biashara ya Mbwa huko China
Hasa mwezi huu wa Ramadhani huko mitaa ya China bihashara hii inalipa, Sasa siju hapa bongo ikoje hio.

THE CO HIMSELF ON THE FIELD

The boss himself....

Calvin Obeld Sahini

calvin
Calvin akizubaaa.