YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Saturday, 18 August 2012

MAONI YA PROFESA J KUHUSU KUWEKA JINA LAKE BADALA YA NAMBA KWENYE GARI.
0
Gari analomiki Profesa Jay sasa hivi.
Kwa zaidi ya mwezi mmoja kama umekua ukipita millardayo.com najua utakua umekutana na story kadhaa za maoni ya mastaa wa bongo kuhusu mpango mpya ulioruhusiwa na Serikali wa kuweka jina badala ya namba kwenye gari kisha unalipia milioni 5 kwa miaka mitatu.
Leo ni zamu ya kuyafahamu maoni ya Legend wa bongofleva Profesa Jay ambae namkariri akisema “hiyo ishu sio ishu, wengi nimeangalia hata kwenye millardayo.com wengi kama hawaafiki hiyo ishu lakini huwezi kuwa na Spacio alafu ukaweka jina lako man, hauwezi kuweka kitu chenye thamani sawa na gari yako si bora ungenunua gari jingine tu bwana, lakini kama utakua na uwezo wa kununua gari nzuri unaweza kufanya hivyo vitu”
Prof ambae ana new single ambayo ina siku mbili tu toka itoke, amesema “mi binafsi nilikua ni mtu mmoja ambae nilishawahi kuwa na magari mengi Bmw, Mercedes benz lakini sasa hivi sifikirii sana au nikimaliza hapo ntakua na magari ambayo yanaweza kuwa hata ya kivita labda nitakayokuja nayo, so nikiwa na magari hayo ninayotaka mimi kwenye ndoto zangu nitaandika, nitaandika Profesa Jay is right here”

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg