YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Thursday 16 August 2012

WALIMU WAJIBU MAPIGO YA SERIKALI WAKATAA KULIPA HASRA YA MGOMO


CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT), kimesema hakipo tayari kulipa gharama ya hasara za uharibifu wa mali zilizotokana na mgomo wa walimu, kwa vile hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuwa wao ndio waliohusika na uhalifu huo.
Tamko hilo linakuja ikiwa ni siku chache tangu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dk. Shukuru Kawambwa, kulieleza Bunge kuwa CWT kama waratibu wa mgomo huo, wanapaswa kulipa fidia za uharibifu wa jengo na ofisi ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mji wa Tunduma na mali nyingine.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi mjini Tunduma baada ya kujionea uharibifu wa ofisi hiyo iliyovamiwa na wanafunzi Julai 30 wakidai haki ya kufundishwa, Kaimu Katibu wa CWT, Ezekiah Oluoch, alisema kama kuna walimu walihusika moja kwa moja, serikali iwachukulie hatua.
“Ninachoweza kusema kwa niaba ya CWT ni kutoa pole kwa uongozi wa mamlaka kwa kuvunjiwa ofisi na kuibiwa samani na kikundi cha wahuni, na tunalaani tukio lililotokea, lakini kwa sababu ofisi za CWT na mamlaka ni majirani wema, tutakapopata tathmini ya uharibifu huo tutatoa kifuta machozi ila si fidia ya ujumla, vinginevyo serikali itupeleke mahakamani,” alisema Oluoch.
Aliongeza kuwa, serikali haikitendei haki chama chao kwa kuwahusisha viongozi wake kuwa wanafadhiliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa ajili ya kuvuruga amani ya nchi, na kwamba ikithibitisha suala hilo, yeye atakuwa wa kwanza kujiuzulu wadhifa wake na kurudi kufundisha.
Kuhusu sensa ya watu na makazi itakayofanyika hivi karibuni na kuwashirikisha walimu, Oluoch alisema kuwa hawapo tayari kuwatetea walimu walioenguliwa majina yao katika mchakato huo wa kusimamia sensa, na hivyo akawaonya kujiepusha na vurugu zinazoweza kukwamisha.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mji wa Tunduma, Aidan Mwasiga, alisema kuwa uharibifu uliotokea siku ya mgomo wa walimu, CWT hawawezi kukwepa lawama kuwa chanzo, na kwamba suala hilo halihusiani na siasa.
Alizitaja baadhi ya athari zilizopatikana bada ya ofisi yake kuvunjwa kuwa ni pamoja na mji huo kukosa ushuru kutokana na nyaraka zote za kiserikali kuibwa, vikiwemo vitabu vya kukusanyia mapato.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg