YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Wednesday, 15 August 2012

0
.
Ishu ya utoroshaji wa wanyama pori ambayo juzi imefanya watumishi watatu wa maliasili kupigwa chini iliingia kwenye page nyingine bungeni Aug 14 2012 baada ya msemaji rasmi maliasili na utalii mchungaji Peter Msigwa kuhoji uhalali wa kutokamatwa kwa ndege iliyobeba wanyama hao.
Amesema pamoja na kwamba Waziri wa maliasili na utalii ametangaza kuwafukuza kazi maafisa watatu, bado sio suluhisho la kudhibiti ujangili kwani mtandao ulioipitisha ndege ya jeshi la Qatar ni mkubwa na unahusisha wafanyakazi wa uhamiaji, Polisi na baadhi ya vigogo serikalini.
“serikali inahusika kwa sababu kuna wakubwa juu yake na kuwatoa wale ni kafara, watupe taarifa ilikuja hapa kufanya nini na ilipotoka hapa ilikwenda wapi, anadanya umma sasa hivi eti anataka kwenda Qatar, anahitaji kwenda Qatar? – Mch Peter Msigwa
Kwenye mistari mingine, mbunge huyu wa Iringa mjini 92.9 amesema hajahusika kuwatetea baadhi ya wamiliki wa vitalu vya wanyamapori kufuatia kuwa na hisa katika miradi hiyo.
2
.
Mara yako ya mwisho kumsikia Profesa Jay kwenye his new single ni lini? ……najua ni time kidogo toka atoe ‘Kamili gado’ ambapo this time karudi na new single ambayo Dully Sykes ametoa baraka zake na kuuza voco kwenye chorus, hii ni time yako kusikiliza mashairi, beat na ujuzi mwingine humu ndani.
Baada ya kuisikiliza.. hakikisha kabla hujaondoka umeacha comment juu ya mapokezi yako kuhusu this new single mtu wangu wa nguvu!
1
.
Huku michuano ya Olympic ikiwa imemalizika tayari, Kituo cha television cha CNN kimeripoti kwamba mwanamichezo Valerie Adams wa New Zealand mwenye umri wa miaka 31, ameshtushwa baada ya kupigiwa simu akiwa njiani kwenye gari yake kueleka nyumbani na kuambiwa kwamba yeye ndio bingwa mpya wa mchezo wa kurusha tufe kwenye michuano ya Olympic 2012.
.
Nadzeya Ostapchuk wa Belarus ambae alishinda hiyo medali ya Gold imegundulika kwamba alitumia dawa za kuongeza nguvu hivyo akaagizwa arudishe hiyo medali.
Kutokana na hiyo ishu, China imepanda kwa kupata tena medali nyingine ya bronz na kupata jumla ya medali 88 kwenye michuano ya Olympic iliyomalizika jumapili iliyopita London Uingereza ambayo kwa mwaka 2016 itafanyika nchini Brazil ikiwa ni nchi ya kwanza ya Amerika Kusini kuwa mwenyeji.
.
0
.
Siku nane zilizopita stori kubwa ya siku area 254, ni Mkali wa muziki wa genge Nonini Mgenge true kutangaza kusain dili la kuwa presenter kwenye radio moja Nairobi yani One Fm.
Baada ya kutangaza hilo dili ilitangazwa kwamba mshkaji atakua Gerald Hando wao kwenye show ya asubuhi kuanzia saa 12 asbh mpaka saa nne ambapo alichukua nafasi ya mtangazaji mwingine aliehamishiwa kwenye show nyingine.
Wengi wanadhani Nonini hii ndio mara yake ya kwanza kufanya kazi kama mtangazaji lakini ukweli ni kwamba alishawahi kufanya hiyo kazi siku kadhaa zilizopita YFM ambayo sasa hivi inaitwa hot 96.
Toka tumepata stori kwamba mshkaji amesain dili la kuwa mtangazaji, nilikua natamani sana kumsikia akiwa mbele ya mic atatema vipi madini, sasa nimefanikiwa kumdaka saa 12 asbh akiwa hewani live August 14 2012… unaweza kumsiliza kidogo akitangaza hapo chini.

kwa hapa Tanzania nakumbuka ni wasanii wawili tu wamewahi kuniambia waliipenda kazi ya kuwa watangazaji japo hawakuwahi kuifanya, ni Izzo Biznes a.k.a Emanuel Simwiga na Hemed Suleiman.’
0
.
.
.
.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg