YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Saturday 18 August 2012

KAULI YA MWISHO YA DOGO JANJA KUHUSU KOLABO NA MADEE.




4
.
June 27 mwaka huu Exclusive on millardayo.com Madee wa Tiptop connection aliongea kwamba amemsamehe Dogo Janja kwa kila kosa alilomfanyia na wala hana kinyongo na yeye, anamtakia mafanikio mema kwenye maisha yake lakini bado anaendelea kukaribishwa Tiptop wakati wowote akihitaji kwenda.. vilevile pia yuko tayari hata kushirikiana nae kisanii kama kushirikiana kwenye nyimbo.
Aug 3 2012 Exclusive kwenye Amplifaya Dogo Janja alikiri kwamba mpaka wakati huo bado alikua hajaonana na Madee toka alipoondoka Tiptop lakini angependa kuonana nae na kuzungumza nae kama kaka, vilevile aliitumia hiyo nafasi kufuta maneno ya hasira aliyoyasema kwenye Amplifaya June 15 2012 wakati alipokosana na Madee na kuamua kurudi nyumbani kwao Arusha ambapo alisema hata siku moja hatomtafuta Madee wala kumpigia simu kutokana na kumuharibia maisha yake kimuziki.
Baada ya kuitoa hiyo kauli Aug 3 kuhusu kutaka kuonana na Madee, jana Aug 15 kupitia Amplifaya ya Clouds Fm, Janja amemaliza mjadala kwa kusema kama ikitokea akahitajika kufanya tena kazi za kisanii kwa kushirikiana na Madee (kolabo) yuko tayari wakati wowote.
Alisema “mi niko poa kabisa sina tatizo na mtu kwa sababu mimi naangalia mbeleni kuna nini na pia naumiza kichwa sana ili watanzania niwape vitu vipya, wapate burudani ya ukweli kutoka kwa Dogo Janja, umoja ni nguvu”

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg