YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Thursday 16 August 2012

HII NDIO LIST KAMILI YA WACHEZAJI WALIOSAJILIWA YANGA KWA AJILI YA MSIMU MPYA.




2
.
Club ya soka ya Yanga imewasilisha jumla ya majina ya wachezaji  28 kwa shirikisho la soka nchini TFF, kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu nchini inayotazamiwa kuanza mapema septemba mosi.
Katibu mkuu wa Young Africans Mwesigwa Selestine amesema wamepeleka majina ya wachezaji wote 28 kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu, na hii ni kutokana na benchi la ufundi kuridhia kuwatumia wachezaji wote.Kwenye huo usajili uliowasilishwa August 15 2012, umeambatana na usajili wa wachezaji wa timu ya vijana U-20 ambapo majina ya wachezaji mahiri wa timu ya Taifa Saimon Msuva na Frank Domayo.
Usajili  kamili kwa timu ya wakubwa ni kama ifuatavyo: Walinda Mlango ni Yaw Berko, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Said Mohamed, walinzi wa pemebeni ni Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Juma Abdul, Oscar Joshua, David Luhende na Stephano Mwasika, walinzi wa kati Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondan, Mbuyu Twite, Ibrahim Job na Ladislaus Mbogo,  viungo wa ulinzi Athuman Idd ‘Chuji’, Juma Seif Kijiko na Salum Telela
Viungo wa pembeni ni Nizar Khalfani, Shamte Ally, Idrisa Rashid na Omega Seme, viungo washambuliaji Haruna Niyonzima, Rashid Gumbo na Nurdin Bakari, washambuliaji Said Bhanaunzi, Hamis Kiiza ‘Diego’, Didier Kavambagu na Jeryson Tegete, hiyo ni kwa upande wa timu ya wakubwa.
Kikosi cha wachezaji chini ya umri wa miaka 20 kina jumla ya majina 22 ambayo ni Geofrey Nyalusi na Yusuf Abdul kama makipa, walinzi ni Said Manduta, Zuberi Juma, Said Mashaka, Benson Michael, Issa Ngao, Rashid Said, viungo: Frank Domayo, Omary Nasry, Clever Charles, Mwinyi Bakari, Mpenda Abdallah, washambuliaji wa pembeni ni Abdulahman Ally, Hussein Moshi, Abdallah Salum, Rehani Kibingu, wWashambuliaji: Saimon Msuva, George Banda, Notikely Masasi, Suleiman Ussi, Kassim Jongo 

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg