YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday 18 June 2013

NAPE: CHADEMA NI WAHUTUHUMIWA NAMBA MOJA


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza  na waandishi wa habari leo mjini Dodoma.
Itakumbukwa tarehe 16/06/2013 ilikuwa ni siku ya uchaguzi mdogo wa madiwani kwa baadhi ya kata nchini. Uchaguzi huo umefanyika kwenye kata ishirini na mbili (22)  kati ya kata ishirini na sita (26) zilizotangazwa kufanya uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi wazi.

 Matokeo tuliyoyapata toka kwenye maeneo yaliyofanya uchaguzi yanaonyesha kuwa kati ya kata 22 zilizofanya uchaguzi CCM tumeshinda kata 16 sawa na asilimia 72.72% na wenzetu wamechukua kata 6 zilizobaki sawa na asilimia 27.28%.

 Tunawashukuru sana kote walikoonyesha imani yao kubwa kwa Chama chetu kwa kutupa dhamana ya kuendelea kuwatumikia. CCM inawaahidi utumishi uliotukuka. Hata wale 27.28% walioamua kuwajaribu wenzetu, tunawatakia kila lakheri, kwani wametumia haki yao ya kidemokrasia kuchagua wanaodhani watawasaidia kufikia malengo yao ya kimaendeleo. Uchaguzi kwenye kata hizi zote umeisha sasa tuwatumikie wananchi.

 Kata nne za jiji la Arusha hazikufanya uchaguzi baada ya kuahirishwa kufuatia tukio la kusikitisha la kulipuka kwa bomu kwenye mkutano wa kampeni wa Chadema mjini Arusha tarehe 15/06/2013.

 CCM tunalaani tukio hilo la mlipuko wa bomu na matukio yanayofanana na hayo katika nchi yetu. Tunawapa pole wale wote walioathirika na tukio hilo. Ni vizuri serikali ikalichunguza swala hili kwa kutumia muda mfupi na kuhakikisha waliohusika wanapatikana na kuchukuliwa hatua zinazostahili.

 Pamoja na kulaani na kuitaka serikali kukomesha vitendo hivi nchini, ni wakati muafaka kwa vyama vya siasa nchini kujitazama upya kwani kuna kila dalili kuwa tukio hili kama alivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari mhe. Mbowe Mwenyekiti wa Chadema Taifa kuwa ni la kupangwa, inawezekana limepangwa na Chadema wenyewe.

 Hali ya kisiasa jijini Arusha kuelekea uchaguzi huo ilikuwa wazi kuwa wana Arusha walishaamua kuzirudisha kata hizo nne kwa CCM, hasa baada ya kuchoshwa na maandamano na vurugu za kila siku jijini Arusha. Aidha kauli za kukata tamaa za viongozi wa Chadema na vitendo vyao ni dalili tosha kuwa tukio hili lilipangwa na Chadema wenyewe.

 CCM tunaendelea kusisitiza na kulaani juhudi za wenzetu kujaribu kujenga umaarufu wa chama chao juu ya damu za Watanzania. Juhudi hizi zinapaswa kulaaniwa na wazalendo wote ndani na nje ya nchi. Tukumbuke asiyekubali kushindwa, si mshindani. Si busara wala uungwana na ni kinyume na utu kutumia majanga ya kutengeneza kama mtaji wa kisiasa.

 Lakini CCM tunalaani pia kitendo cha viongozi wa Chadema kujaribu kutumia baadhi ya misiba na majeruhi wa tukio hili kisiasa na mwisho wa siku kwenda kuwatelekeza hospitali baadhi yao baada ya kuwaahidi kubeba gharama zote za matibabu na mazishi.Tunaipongeza serikali kwa kuingilia kati na kuwasaidia waathirika hawa na kuhakikisha wanapata huduma inayostahili.

 CCM inarudia kueleza masikitiko yake kwa waathirika wa tukio hili la kinyama na kikatili lisilostahili kuvumiliwa hata kidogo. Kama Chama tumeguswa sana na tukio hili pamoja na kulilaani, tunawasihi watanzania tushindane na kutofautiana bila kupigana na kuvunja tunu ya nchi yetu ya amani na utulivu. Katika demokrasia ya vyama vingi swala la kuvumiliana ni swala la msingi sana katika kufikia ukomavu wa demokrasia hiyo.

 Imetolewa;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa CCM Itikadi na Uenezi.
17/06/2013
Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi

MBOWE:MABOMU YAMERUSHWA NA POLISI KWA MAAGIZO



"Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema polisi wanahusika na milipuko katika mkutano wa CHADEMA na kuua watu watatu.

Mh Mbowe amesema ana ushahidi na picha za video za tukio hilo.

Mh Mbowe alisema hayo akihojiwa na ITV" From Jamii forums

Pia nape nae amekaririwa akisema chadema wenyewe ndio wamehusika na bomu hilo...
Sasa hapo sijui tumwamini nani ?
My take 
---------
Hapa inawezekana hakuna kati yao aliyehusika but ni mtu we pembeni sasa havi amekaa anakunywa kahawa akichekelea jinsi wanavyozozana....Hivyo wasubiri uchunguzi wa Dola ..haya wanayoyasema bila uchunguzu yanatuchanganya tu ..

Monday 17 June 2013

VIDEO HII IKIMUONYESHA MSICHANA ALIYEKAMATWA NA KILO 5 ZA HEROIN EGYPT AFANYIWA MAHOJIANO LIVE.





Msichana anaejulikana kwaJina la Fatma aka Brown Berry Aliyekamatwa Egypt na madawa ya Kulevya Afanyiwa Mahojiano, Angalia na sikiliza kwa makini mahojiano ya Fatma a.k.a brown Berry hapo chini

TOA MAONI YAKO HAPA

GERALD HANDO WA CLOUDS FM NUSURA AFUMULIWE NA BASTOLA LEO



MTANGAZAJI maarufu wa Clouds FM, Gerald Hando leo alfajiri alizua kizaazaa na kupelekea kutishiwa bastola na mtu ambaye jina lake halikufahamika mara moja.
Chanzo cha Saluti5 kimesema Hando aligonga gari la mtu huyo maeneo ya Kwa Kopa, jambo lililopelekea mtu huyo ashuke kwenye gari lake bastola ikiwa mkononi na kutishia kumfumua Hando.
Kama mtu huyo alidhani kutoa bastola ndio suluhisho basi alikosea sana, Gerald Hando anayetangaza kipindi cha "Power Breakfast" naye alishuka kwenye gari lake na kufungua shati lake na kuanza kumuamrisha mtu huyo afyatue bastola.
Huku akiporomosha matusi kwa ukali Hando alisema: “Piga hiyo bastola yako, shoot me.”
Hando aliendelea kuwa mkali huku akipigapiga kifua chake hali iliyovuta watu wengi kwenye tukio hilo ambao waliwasihi wote wawili kutuliza mzuka na kumfanya mtu huyo aliyekuwa na gari aina ya Rav 4 arudishe bastola yake kwenye gari na kutafuta njia nyingine ya kulimaliza tatizo lililotokea.

MSIKILIZE MR SUGU AKIONGEA ALIPOKUWA JUKWAANI KATIKA SHOW YA LADY JAY DEE



Mr II Sugu akiingia kwenye jukwaa la Machozi Band kwenye show ya miaka 13 ya Lady Jay Dee .. Video
TOA MAONI YAKO HAPA

MACHANGUDOA WANAOFANYA BIASHARA YAO SINZA WAKAMATWA





Mgambo wa jiji la Dar es Salaam wakiwa katika zoezi la kuwakamata Madada wanaofanya biashara ya kuuza miili yao wajulikanao kama Machangudoa katika eneo la Sinza. Picha mbalimbali zikionyesha namna walivyokuwa wakipakiwa ndani ya Gari tayari kwa kupelekwa katika vyombo vya sheria

PICHA MBALI MBALI YA KINACHIJIRI KATIKA KUANDAA UTARATIBU WA KUMUAGA LANGA


You might also like:

MAPENZI YA JINSIA MOJA YADAIWA KUSHAMIRI HALMASHAURI YA MOROGORO


HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro inakabiliwa na changamoto ya kukua kwa maambukizi ya Ukimwi, baada ya kushamiri kwa biashara ya mapenzi ya jinsia moja. Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Naibu Meya Manispaa ya Morogoro, Lidya Mbiaji, alisema kuwa kumekuwa na tatizo kubwa la kushamiri kwa vichocheo vya ngono, hali inayochangia kukua kwa kiwango cha maambukizi ya Ukimwi katika mkoa huo.

Pia alisema ongezeko la nyumba za kulala wageni nalo limekuwa kichocheo kikubwa cha kushamiri kwa biashara ya ngono zembe.

Aliionya jamii kuepukana na mila na desturi zinazochangia kuleta vichocheo vya kuongezeka kwa maambukizi ya ukimwi, ikiwemo ngoma za unyago zijulikanazo kwa jina maarufu la kunemwa pamoja na mabanda ya kuonyesha video ambayo nje yamekuwa yakionyesha mechi za soka, lakini ndani ya mabanda hayo huonyesha picha za ngono na kusababisha kuleta hamasa ya watu kufanya ngono.

Pia aliviomba vyombo vya habari kusaidia kuelimisha jamii namna ya kujiepusha vitendo vinavyochangia maambukizi ya ukimwi, kwani hali si shwari kutokana na makundi ya watu wanaofanya biashara ya ngono kuvamia Manispaa ya Morogoro.

Alisema hata kwa wasomi wa vyuo vikuu, hali pia si shwari, kutokana tafiti kuonyesha kuwa wana kiwango cha juu cha kufanya ngono zembe, hivyo kulitisha taifa kupoteza wasomi wake mara baada ya kumaliza masomo yao.

“Kumekuwa na makundi makubwa ya jamii yanayoingia katika hatari ya kupata maambukizi…ukiangalia kundi la wanafunzi, watu masikini na wanawake, hasa wajane changamoto hii inawagusa moja kwa moja,” alisema Mbiaji.