YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Saturday 24 February 2018

NILITEULIWA ILI NIWATUMIKIE WATANZANIA KULIKO WAGENI KUTOKA NJE-BITEKO


Leo February 23, 2018 Serikali imesema kuwa sheria mpya ya Madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017 inaelekeza kuwa Madini yote nchini ni Mali ya Watanzania hivyo wanapaswa kutambua umuhimu wa rasilimali.
“Wawekezaji na wachimbaji wote wa madini nchini wanapaswa kutambua kuwa wanalo jukumu muhimu la kurejesha kwa jamii asilimia chache ya kile wanachozalisha kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha miundombinu, sekta ya elimu, afya” -Biteko
Naibu Waziri wa Madini Doto Mashaka Biteko amesisitiza hayo wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Nkasi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la mradi wa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe Mkoani Rukwa Magharibi mwa Tanzania.
“Nataka niwajulishe tu Watanzania wenzangu Rais  Magufuli aliniteua kusimamia Wizara ya Madini nikimsaidia Waziri wetu Anjelina Kairuki ili kuboresha sekta hii ya Madini hatimaye kuwanufaisha watanzania kuliko ilivyokuwa awali ambapo Madini yalikuwa yanachimbwa nchini lakini faida inaenda nchi zingine” -Biteko
Wawekezaji hao wanapaswa kutoa ajira zisizo za utaalamu kwa wananchi wanaozunguka migodi yao sambamba na watanzania wote huku akiwaagiza kuwaajiri wataalamu wa Madini wa ndani ya nchi kwa kazi ambazo wanaweza kuzifanya sio kuajiri wageni.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg