YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Thursday 30 June 2016

WAKUU WA WILAYA WAKILA KIAPO HIO JANA IKURU DSM.

Baadhi ya Wakuu wa wilaya wapya wakila kiapo cha uadilifu Ikulu, jijini Dar es salaam jana kabla ya kwenda kwenye vituo vyao vya kazi.

Wednesday 29 June 2016

WATOKA BUNGENI KWA MABANGO YENYE UJUMBE MZITO.

Leo hii wabunge wanaounda umoja wa ukawa wameendelea kutoka nje ya ukumbi wa bunge kwa kuonyesha mabango yenye ujumbe mzito kama yanavyo onekana katika picha.




Tuesday 28 June 2016

USAJIRI BARANI ULAYA. TETESI.





TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE 28.06.2016
Chelsea wanajiandaa kuingia katika mbio za kumwania kiungo wa Roma Axel Witsel, 27, ambaye yuko Ufaransa na timu yake ya taifa ya Ubelgiji katika Euro 2016 (Daily Mail), Barcelona huenda wakamnyatia beki wa Arsenal Hector Bellerin, 21, baada ya Dani Alves kuondona Barca na kwenda Juventus (London Evening Standard), Crystal Palace wamekubaliana ada ya uhamisho ya pauni milioni 31.6 ya kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji Mitchy Batshuayi, 22, anayechezea Marseille (Guardian), Manchester City huenda wakawazidi kete Manchester United na Benfica katika kumsajili winga Marlos Moreno, 19, anayeichezea Atletic Nacional ya Colombia kwa pauni milioni 8 (Daily Mail), Real Madrid wanapanga kumtoa mshambuliaji wake Jese, 23, kwa mkopo msimu ujao, licha ya mchezaji huyo kusakwa na Chelsea na Manchester United kwa mkataba wa kudumu (AS), meneja wa Hull City Steve Bruce anafikiria kumsajili mshambuliaji kutoka Paraguay anayecheza Augsburg Raul Bobadilla, 29, anayedhaniwa kuwa na thamani ya pauni milioni 5 (Daily Mirror), Leicester City wapo kwenye mazungumzo ya kumsajili kiungo Nampalys Mendy, 24, kwa pauni milioni 13, kutoka Nice (Leicester Mercury), Zlatan Ibrahimovic, 34, atafanya vipimo vya afya Old Trafford wiki ijayo kabla ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja (Sky Sports), beki wa Chelsea Baba Rahman, 21, anasakwa na Lazio ambao tayari wametoa dau la pauni milioni 13 kumtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana aliyenunuliwa na Chelsea msimu uliopita kwa pauni milioni 21.7 (Daily Mirror), Napoli wamekubaliana maslahi binafsi na Hector Herrera, 26, anayesakwa na Liverpool, lakini klabu hiyo ya Italia bado haijakubaliana na Porto ada ya uhamisho wa kiungo huyo (Tutto Mercatto), Arsenal wamepanda dau kumtaka mshambuliaji Gabriel Barbosa, 19, ambaye kifungu chake cha uhamisho ni pauni milioni 40, katika klabu yake ya Santos ya Brazil (ESPN Brazil), meneja wa Everton Ronald Koeman anajiandaa kumsajili kipa Maarten Stekelenburg, 33, ambaye alikuwa Southampton msimu uliopita kwa mkopo akitokea Fulham (Liverpool Echo). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Cheers!

Monday 27 June 2016

MAGAZETINI LEO 28/6/2016 STORI KUBWA ZA UTEUZI NA MAMBO MENGINE

 

















 






 

RAISI KUTETA NA LIONEL MESSI


OMBI LA RAIS WA ARGENTINA BAADA MESSI KUTANGAZA KUJIULU  SOKA LA KIMATAIFA:
Rais wa Argentina Mauricio Macri amemwita nyota wa soka wa nchi hiyo Lionel Messi kwa lengo la kumuomba atengue maamuzi yake ya kujiuzulu kucheza soka la kimataifa.

Messi alifikia maamuzi hayo baada ya timu yake kushindwa kwa mara ya pili mfululizo katika fainali za Copa America huku akiwa miongoni mwa wachezaji waliokosa mikwaju ya Penalti. ''Amemwita na kumueleza namna anavyoona fahari kwa kiwango kizuri kilichoonyeshwa na timu yake katika michuano hiyo huku akimtaka asisikilize maneno ya watu'' ilisema msemaji wa Rais Macri.
Ndani ya miaka mitatu Messi ametinga katika fainali tatu tofauti moja ikiwa ni ya kombe la dunia nchini Brazili mwaka 2014 ambapo walipoteza dhidi ya Ujerumani,na nyingine mbili za Copa America moja ikiwa mwaka 2015 na 2016 zote timu yake ikipoteza dhidi ya Chile.


KARIAKOO MIAKA YA 80'S

Kama hukupata bahati ya kuiona Kariakoo miaka hio sasa ilikuwa inafanana hivi.  Na hapa ni mtaa maalufu sana na wenye msongamano mkubwa wa watu mtaa wa kongo.

KITWANGA AKABIDHI OFISI RASMI KWA NCHEMBA

KITWANGA AKABIDHI OFISI : Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu  Nchemba (wa pili kushoto) akipokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Picha na  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

HT: Iceland 2 - 1 England

Timu ya England mpaka sasa ipo nyuma kwa bao mbili moja kwa dhidi ya Icelanf. Matokeo yakendelea kuwa mama yalivyo Engla itakua imejitoa EURO kwa mara ya pili.

RAISI MSTAAFU WA AWAMU YA PILI ATOA NENO KWA BAKWATA.

#Habari:Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi ameutaka uongozi wa baraza kuu la waislamu BAKWATA kuunda mfuko maalum wa fedha kwa ajili ya kugharamia shughuli mbalimbali za kimaendeleo kwa waumini wa kiislaam.

WAKUU WA WILAYA NA MIKOA WAPYA HAWA HAPA.


Rais Magufuli ateua maDC 139 na kupangua maRC

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R. Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Bi. Zainab R. Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Rais Magufuli pia amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Dkt. Binilith Satano Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambako atapangiwa majukumu mengine.
Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Charles F. Mlingwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Dkt. Charles F. Mlingwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Stanslaus Magesa Mulongo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Wakuu wapya wa mikoa walioteuliwa wataapishwa tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam na mara baada ya kuapishwa watakula kiapo cha maadili ya uongozi.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 139.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika uteuzi huo Rais Magufuli amezingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na umri ambapo kwa wale ambao umri wao ni zaidi ya miaka 60 ameamua wastaafu.
Mhe. Rais amewashukuru sana kwa utumishi wao mzuri na amesema pale ambapo itahitajika, serikali itaendelea kuwatumia katika majukumu mengine.
Katika uteuzi huo, Wakuu wa Wilaya waliopo sasa ambao wamebaki katika nafasi zao ni 39. Pia Rais Magufuli amewateua Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri 22 kuwa Wakuu wa Wilaya kutokana na utendaji wao mzuri.
Aidha, nafasi 78 za uteuzi wa Wakuu wa wilaya zimejazwa na watanzania wengine ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza wengi wao wakiwa ni vijana, wenye elimu ya kutosha na uzoefu katika maeneo mbalimbali.
Walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya ni kama ifuatavyo (Orodha imepangwa kulingana na mikoa)
ARUSHA
1. Arusha - Mrisho Mashaka Gambo
2. Arumeru - Alexander Pastory Mnyeti
3. Ngorongoro - Rashid Mfaume Taka
4. Longido - Daniel Geofrey Chongolo
5. Monduli - Idd Hassan Kimanta
6. Karatu  - Therezia Jonathan Mahongo
DAR ES SALAAM
1. Kinondoni - Ally Hapi
2. Ilala  - Sophia Mjema
3. Temeke - Felix Jackson Lyaviva
4. Kigamboni - Hashim Shaibu Mgandilwa
5. Ubungo - Hamphrey Polepole
DODOMA
1. Chamwino - Vumilia Justine Nyamoga
2. Dodoma - Christina Solomon Mndeme
3. Chemba - Simon Ezekiel Odunga
4. Kondoa - Sezeria Veneranda Makutta
5. Bahi  - Elizabeth Simon
6. Mpwapwa - Jabir Mussa Shekimweli
7. Kongwa - John Ernest Palingo
GEITA
1. Bukombe - Josephat Maganga
2. Mbogwe - Matha John Mkupasi
3. Nyang'wale - Hamim Buzohera Gwiyama
4. Geita  - Herman C. Kipufi
5. Chato  - Shaaban Athuman Ntarambe
IRINGA
1. Mufindi - Jamhuri David William
2. Kilolo  - Asia Juma Abdallah
3. Iringa  - Richard Kasesela
KAGERA
1. Biharamulo - Saada Abraham Mallunde
2. Karagwe - Geofrey Muheluka Ayoub
3. Muleba - Richard Henry Ruyango
4. Kyerwa - Col. Shaban Ilangu Lissu
5. Bukoba - Deodatus Lucas Kinawilo
6. Ngara  - Lt. Col. Michael M. Mtenjele
7. Missenyi - Lt. Col Denis F. Mwila
KATAVI
1. Mlele  - Rachiel Stephano Kasanda
2. Mpanda - Lilian Charles Matinga
3. Tanganyika - Saleh Mbwana Mhando
KIGOMA
1. Kigoma - Samsoni Renard Anga
2. Kasulu  - Col. Martin Elia Mkisi
3. Kakonko - Col. Hosea Malonda Ndagala
4. Uvinza  - Mwanamvua Hoza Mlindoko
5. Buhigwe - Col. Elisha Marco Gagisti
6. Kibondo - Luis Peter Bura
KILIMANJARO
1. Siha  - Onesmo Buswelu
2. Moshi  - Kippi Warioba
3. Mwanga - Aaron Yeseya Mmbago
4. Rombo - Fatma Hassan Toufiq
5. Hai  - Gelasius Byakanwa
6. Same  - Rosemary Senyamule Sitaki
LINDI
1. Nachingwea - Rukia Akhibu Muwango
2. Ruangwa - Joseph Joseph Mkirikiti
3. Liwale  - Sarah Vicent Chiwamba
4. Lindi  - Shaibu Issa Ndemanga
5. Kilwa  - Christopher Emil Ngubiagai
MANYARA
1. Babati  - Raymond H. Mushi
2. Mbulu  - Chelestion Simba M. Mofungu
3. Hanang' - Sara Msafiri Ally
4. Kiteto  - Tumaini Benson Magessa
5. Simanjiro - Zephania Adriano Chaula
MARA
1. Rorya  - Simon K. Chacha
2. Serengeti - Emile Yotham Ntakamulenga
3. Bunda  - Lydia Simeon Bupilipili
4. Butiama - Anarose Nyamubi
5. Tarime - Glodious Benard Luoga
6. Musoma - Dkt. Vicent Anney Naano
MBEYA
1. Chunya - Rehema Manase Madusa
2. Kyela  - Claudia Undalusyege Kitta
3. Mbeya  - William Ntinika Paul
4. Rungwe - Chalya Julius Nyangidu
5. Mbarali - Reuben Ndiza Mfune
MOROGORO
1. Gairo  - Siriel Shaid Mchembe
2. Kilombero - James Mugendi Ihunyo
3. Mvomero - Mohamed Mussa Utali
4. Morogoro - Regina Reginald Chonjo
5. Ulanga  - Kassema Jacob Joseph
6. Kilosa  - Adam Idd Mgoyi
7. Malinyi - Majula Mateko Kasika
MTWARA
1. Newala - Aziza Ally Mangosongo
2. Nanyumbu - Joakim Wangabo
3. Mtwara - Dkt. Khatibu Malimi Kazungu
4. Masasi  - Seleman Mzee Seleman
5. Tandahimba - Sebastian M. Walyuba
MWANZA
1. Ilemela - Dkt. Leonald Moses Massale
2. Kwimba - Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon
3. Sengerema - Emmanuel Enock Kipole
4. Nyamagana - Mary Tesha Onesmo
5. Magu  - Hadija Rashid Nyembo
6. Ukerewe - Estomihn Fransis Chang'ah
7. Misungwi - Juma Sweda
NJOMBE
1. Njombe - Ruth Blasio Msafiri
2. Ludewa  - Andrea Axwesso Tsere
3. Wanging'ombe - Ally Mohamed Kassige
4. Makete  - Veronica Kessy
PWANI
1. Bagamoyo - Alhaji Majid Hemed Mwanga
2. Mkuranga - Filberto H. Sanga
3. Rufiji  - Juma Abdallah Njwayo
4. Mafia  - Shaibu Ahamed Nunduma
5. Kibaha - Asumpter Nsunju Mshama
6. Kisarawe - Happyness Seneda William
7. Kibiti  - Gulamu Hussein Shaban Kifu
RUKWA
1. Sumbawanga - Dkt. Khalfan Boniface Haule
2. Nkasi  - Said Mohamed Mtanda
3. Kalambo - Julieth Nkembanyi Binyura
RUVUMA
1. Namtumbo - Luckness Adrian Amlima
2. Mbinga - Cosmas Nyano Nshenye
3. Nyasa  - Isabera Octava Chilumba
4. Tunduru - Juma Homela
5. Songea - Polet Kamando Mgema
SHINYANGA
1. Kishapu -  Nyambonga Daudi Taraba
2. Kahama - Fadhili Nkulu
3. Shinyanga - Josephine Rabby Matiro
SIMIYU
1. Busega - Tano Seif Mwera
2. Maswa  - Sefu Abdallah Shekalaghe
3. Bariadi - Festo Sheimu Kiswaga
4. Meatu  - Joseph Elieza Chilongani
5. Itilima  - Benson Salehe Kilangi
SINGIDA
1. Mkalama - Jackson Jonas Masako
2. Manyoni - Mwembe Idephonce Geofrey
3. Singida - Elias Choro John Tarimo
4. Ikungi  - Fikiri Avias Said
5. Iramba - Emmanuel Jumanne Luhahula
SONGWE
1. Songwe - Samwel Jeremiah
2. Ileje  - Joseph Modest Mkude
3. Mbozi  - Ally Masoud Maswanya
4. Momba - Juma Said Irando
TABORA
1. Nzega  - Geofrey William Ngudula
2. Kaliua  - Busalama Abel Yeji
3. Igunga  - Mwaipopo John Gabriel
4. Sikonge - Peres Boniphace Magiri
5. Tabora - Queen Mwashinga Mlozi
6. Urambo - Angelina John Kwingwa
7. Uyui  - Gabriel Simon Mnyele
TANGA
1. Tanga  - Thobias Mwilapwa
2. Muheza - Mhandisi Mwanaisha Rajab Tumbo
3. Mkinga - Yona Lucas Maki
4. Pangani - Zainab Abdallah Issa
5. Handeni - Godwin Crydon Gondwe
6. Korogwe - Robert Gabriel
7. Kilindi  - Sauda Salum Mtondoo
8. Lushoto - Januari Sigareti Lugangika
Wakuu wote wa Wilaya walioteuliwa wanapaswa kufika Ikulu Dar es salaam siku ya Jumatano tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi kwa ajili ya kiapo cha maadili ya uongozi na maelekezo mengine kabla ya kuapishwa na wakuu wa mikoa watakaporejea katika mikoa yao.

WAZEE WA ULAYA TIMU YA ITALIA WATOA DOZI KWA SPAIN.

TIMU YA TAIFA YA ITALIA JIONI YA LEO IMEIFUNGASHIA VILAGO MABINGWA WATETEZI WA KIKOMBE CHA UBINGWA WA ULAYA.