YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Friday 30 May 2014

PICHA ZA GARI ALILOKUWEMO MAREHEMU TYSON WAKATI WAKITOKA MKOANI DODOMA NA KUPATA NALO AJALI

IMG_4162
Marehemu Geogre Tyson pichani hapa alikuwa yupo kijiji cha Chilonwa Chamwino kwenye utoaji wa madawati katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma. Baada ya kumaliza shughuli hii huku akiwa kama producer wa The Mboni Show mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni masaa 4 tu toka tuanze safari ya kurudi Dar es Salaam maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia GAIRO mjini.
Katika gari hilo walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha na wengine kupata majiraha mwilini pamoja na dereva wa gari hilo. Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa Morogoro katika  hospital ya mkoa Morogoro, baadae asubuhi mwili utaanza safari ya kuelekea Dar es Salaam.
IMG_4166 IMG_4213IMG_4214IMG_4215
Kweli ajuae mwisho wetu ni Mungu pekee. Tunaishi kama vile tunajua maisha yetu yataisha lini kumbe tunajidanganya. Haya matukio yote ni kwa ajili yetu kuamka na kujifunza kitu. Tumrudieni Mungu, tuungame dhambi zetu maana hakuna ajuae siku wala saa yake itakuwa lini. R.I.P Tyson na wote mliotutangulia.
Picha zote kutoka DJ Choka Music

SAD NEWS: MUONGOZAJI MAHIRI WA FILAMU NA VIPINDI TANZANIA GEORGE TYSON AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA GARI ILIYOTOKEA MKOANI MOROGORO

George Tyson enzi za Uhai wake

Taarifa zilizotufikia katika meza yetu ya habari Usiku huu ni kuwa Muongozaji mahiri katika Tasnia ya Filamu Nchini na Mzazi Mwenza wa Msanii Nguli wa Filamu nchini Vyonne Cherry Au Monalisa, Bwana George Tyson amefariki Dunia mara baada ya kupata ajali ya gari Mkoani Morogoro Katika Eneo la Gairo wakati wakitokea Mkoani Dodoma ambapo walienda kwaajili ya Kuadhimisha Miaka Miwili ya Kipindi Cha Mboni Show.

Bw Tyson Mauti yamemfika mara baada ya Gari walilokuwa Wakitumia kusafiria Kutoka Mkoani Dodoma Kupasuka Matairi na kupelekea Kupoteza maisha na kupelekea hali ya watu wengine wanne waliokuwemo katika Gari hilo kuwa mbaya baada ya Kuumia vibaya na kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwaajili ya Matibabu.

Ajali hiyo imetokea majira ya Saa Moja Usiku katika Eneo la Gairo

Tutaendelea Kupeana taarifa zaidi kadri tunavyozipata

Tunapenda kutoa Pole kwa Mmoja wa Majaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents ambae ni Mzazi Mwenza wa Marehemu George Tyson, Bi Vyonne Chery Kwa kuondokewa na Mzazi mwenzie ambae walibahatika Kupata Mtoto Mmoja aitwaye Sonia.

Timu nzima ta TMT inatoa Pole kwa Msiba Huu

BREAKING NEWSSS:::MWANAMKE AUAWA VIBAYA KWA KUKATWA KICHWA HUKO GEITA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA TUNAOMBA RADHI KWA PICHA

 Mwili wa Lushiku Tenganija ukiwa chini baada ya mauji hayo


Mwanamke mmoja ameuawa kikatili kwa kukatwa katwa na mapanga sehemu mbalimbali za Mwili wake kwa kudhaniwa kuwa anaimani za Kishirikina, Mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Lushiku Tenganija  Sono Msukuma aliyekuwa na Umri wa Miaka 59 wa kitongoji cha Senga kata ya Bugando Mkoani Geita ameuawa na mwili kuonekana muda wa Saa moja asubuhi jana  ukiwa kwenye barabara ya mtaa umbali wa mita kama mia tatu kutoka nyumbani alipokuwa akiishi Marehemu pamoja na wajukuu zake watatu.
Maremu amekatwa shingo kabisa na kutenganishwa na Mwili, mkono wa kushoto na kulia pamoja na bega la kulia. Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Bwana Joel Saanane (42) amethibitisha kutokea kwa Tukio hilo na kudai kuwa msako mkali unaendelea dhidi ya wauaji hao.

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU USDM AMEKUTWA AMEFARIKI BAADA YA KWENDA KUPUMZIKA HOSTEL..TIZAMA PICHA HAPA


 



APIGWA BAADA YA KUTUHUMIWA KIBA NG'OMBE


Mwili wa Kijana huyo Ukiwa umefunikwa na Majani Kabla ya Kuchomwa Moto
Mwili wa Kijana huyo ukiwa unachomwa Moto na wananchi wa Eneo hilo
 Akielezea Tukio Lilivyo tokea
 Ng'ombe Walioibiwa
 Wakichukua Mwili wa Kijana Huyo
 Wakichukua Mwili wa Kijana Huyo

**********************

WAKATI vyombo mbali mbali zikiendelea na jitihada za kuwaelimisha wananchi juu ya madhara ya kujichukulia sheria mkononi hali hiyo bado ni tete mkoani Mbeya.
Hali hiyo imezidi kujitokeza baada ya Wananchi wenye hasira kali wa Mwasanga Ivumwe jijini Mbeya kumpiga na kumchoma moto mwananchi mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja wakimtuhumu kwa Wizi wa Ng’ombe mmoja na ndama.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ameuambia mtandao huu kuwa tukio hilo lilitokea mapema leo asubuhi ambapo chanzo ni wizi wa Ng’ombe wa Kongoro Mwakitalima mkazi wa Isyesye kata ya Ilomba.
Alisema Ng’ombe huyo aliibiwa jana majira ya usiku ambapo mzee huyo alitoa taarifa kwa majirani ambao asubuhi walijihimu kutafuta ambapo walipofika maeneo ya  Ivumwe walikutana na mwendesha boda boda ambaye aliwaambia amekutana na mtu akiwa anaswaga hiyo mifugo.
Alisema baada ya kusikia hivyo waliamua kuanza kumfukuzia wakitumia bodaboda na ndipo walipofika eneo la Mwasanga relini walimkuta mtuhumiwa akiwa na hao Ng’ombe.
Alisema Wananchi mbali mbali walikusanyika na kuanza kumshushia kipigo kutokana na eneo hilo kukithiri kwa wizi wa mifugo lakini baada ya kipigo hicho mtuhumiwa alionekana kuwa ngangari jambo lililowatia hasira na kuamua kumchoma moto.
Shuhuda huyo aliendelea kusema baada ya kuanza  kumchoma lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida mtu huyo hakuweza kukata roho hadi alipookolewa na Askari wa jeshi la polisi walipofika eneo la tukio.
Hadi tunaingia mtamboni hakuna taarifa zilizothibitisha kama mtuhumiwa huyo bado yuko hai ama amepoteza maisha.
 

Thursday 29 May 2014

MAGAZETI YA LEO, TAREHE 30 MAY 2014


.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.