YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Thursday 29 May 2014

TAARIFA KUHUSU MTOTO ALIYEFUNGIWA KWENYE BOKSI

MAJIBU ya vipimo vya afya vilivyofanyika juzi kwa mtoto  Nasra Rashid (4), aliyefichwa kwenye boksi mkoani Morogoro, kwa muda wa miaka minne, yanatarajiwa kutolewa leo.Mtoto huyo awali alilazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ambako waliamua kumhamishia Muhimbili ambako alifanyiwa vipimo mbalimbali kuchunguza afya yake.Wakati majibu hayo yakitarajiwa kutolewa leo, madaktari wanaomungalia mtoto huyo wamemuanzishia lishe maalumu ya maziwa, pamoja na dozi maalumu ya sindano ya kuzuia maumivu kutokana na kulalamika maumivu ya kifua.Taarifa hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, Dosis Ishenda, wakati akizungumza na Tanzania Daima.Alisema hali ya Nasra inaendelea vizuri na kwamba vipimo vyote vya msingi vimeshachukuliwa na majibu yake yatatolewa leo.“Hali yake inaendelea vizuri ingawa analalamika kuwa na maumivu ya kifua, pia madakatari wamemuanzishia lishe maalumu ya maziwa kwa ajili ya kumsaidia kupata nguvu,” alisema Ishenda.
Nasra, alifikishwa Muhimbili juzi saa saba usiku kutoka mkoani Morogoro baada ya hali yake kubadilika ghafla.Akiwa katika hospitali ya Muhimbili, alianza kupatiwa huduma za awali ikiwa ni pamoja na kupimwa uzito, damu na haja ndogo.Mei 21, mwaka huu, mwanamke aliyetambuliwa kuwa ni Mariamu Said mkazi wa Kiwanja cha Ndege, Morogoro, alibainika kumficha mtoto wa marehemu mdogo wake kwenye boksi kwa miaka minne, hali iliyowafanya wananchi wamshambulie kwa kipigo kutokana na unyama aliomtendea.Siri ya unyama huo iliibuliwa na majirani wa mtuhumiwa baada ya kutoa taarifa kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Dia Zongo kuhusu mtoto, Nasra Rashid, kufichwa ndani ya boksi tangu akiwa na umri wa miezi tisa.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg