YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Sunday 27 July 2014

RAIS KIKWETE ATUNUKU WAHITIMU WA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI KATIKA MAHAFALI YA KOZI YA PILI


 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Kanali
James Ruzibiza Stashahada ya Usalama na Stratejia (Diploma in Security
and Strategic Studies) katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa
cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai
26, 2014. Kanali Ruzibiza, ambaye anatokea Rwanda, ni mmoja wa washiriki
tisa wa kozi waliotoka nchi za nje. Washiriki wengine kutoka nje y nchi
walitoka Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Uganda, zambia na Zimbabwe.
Jumla ya wahitimu 30, wakiwemo maafisa wandamizi katika utumishi wa
umma, ambapo 11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine vya usalama na idara mbalimbali. 
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Luteni Jenerali
C.L. Makakala Shahada ya Uzamili ya Falsafa ya Usalama na Stratejia
katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC)
chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014. Luteni
jenerali Makakala, ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi wa
kwanza, amekuwa mtunukiwa wa kwanza wa Shahada hiyo hapo chuoni.
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia baada ya kutunuku shahada katika  mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi  (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014.Jumla ya wahitimu 30 wamehudhuria kozi hiyo wakiwemo maafisa wandamizi katika utumishi wa umma, ambapo 11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine  vya usalama na idara mbalimbali. Washiriki wengine tisa wametoka  nchi  za nje ambazo ni Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Rwanda Uganda, Zambia  na Zimbabwe.
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaambia kuwa sasa ni
zamu yao kupiga picha ya kumbukumbu bila yeye wahitimu wa Kozi ya Pili
ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es
salaam leo Julai 26, 2014.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg