YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday 11 March 2014

NMB WAAMUA KUSAIDIA VIJANA KWA KUFANYA HAYA,

three wheeler 1Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni tatu yaani Fair Deal Auto Private Ltd inayosambaza pikipiki za miguu miwili na mitatu aina ya Bajaji,kampuniyaCar & General Limited Ltd inayosambaza pikipiki za miguu mitatu aina ya TV’S King pamoja na kampuni ya Quality Motors inayosambaza pikipiki za miguu miwili aina ya Honda wameingia ubia ili kuwawezesha wananchi kupata mikopo nafuu ya kumiliki pikipiki za miguu miwili na mitatu.
NAGU 4Hii yote ni katika kuendeleza azma ya NMB inayolenga kubuni huduma na bidhaa mbalimbali za kibenki zinazogusa kwa karibu mahitaji ya wateja na watanzania kwaujumla.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mikopo hii jijini Mwanza,Waziri waUwezeshaji naUwekezaji kutoka ofisi ya Waziri Mkuu,Mhe.Dkt.Mary Nagu amesema>>’Mikopo hii ya pikipiki itawasaidia sana vijana na wananchi kwa ujumla kuweza kumiliki pikipiki zitakazowawezesha kuendesha maisha yao ya kila siku. Binafsi natambua ajira kwa vijana imekua ni changamoto maeneo mengi nchini hivyo basi ningependa kuwasisitiza vijana wachukue fursa hii inayotolewa na NMB kuweza kumiliki biashara zao wenyewe na kujikimu kiuchumi‘.
Vile vile kutoka NMB Mkuu wa Kitengo cha Biashara za kibenki Bw.Filbert Mponzi amesema kuwa bidhaa hii mpya inalenga kupunguza changamoto za ajira kwa vijana hapa nchini.
Marejesho ya mkopo huu wa pikipiki ya miguu miwili na mitatu yanatolewa ndani ya muda wa miezi 24 ambapo kwa kipindi hiki chote, mteja ataendelea kurejesha makato yake ya kila mwezi kwa kuzingatia taratibu za makubaliano yatakayofanyika baina ya mteja na benkiya NMB.
Mikopo hii pia inawekewa bima kwa ajili ya ulemavu au kifo kitakachomtokea mmliki wa pikipiki iliyochukuliwa mkopo,bima hii ni kwaajili ya kumpa unafuu mkopaji endapo atapata matatizo ya kiafya ambayo yatamfanya apate ulemavu au kupoteza maisha.
NAGU 6Kwa maelezo zaidi tembelea matawi ishirini na moja tu ya NMB nchi nzima yanayotoa mikopo hii,matawi hayo kwa Mwanza-Buzuruga na Kenyata Road,Dar es Salaam-Tegeta,Magomeni,Mwenge,Mbezi Beach, Temeke, Ilala,Mlimani City,Msasani na Airport,Arusha-Clock Tower na Arusha Market,Manyara-Babati naKatesh,Dodoma,Mbeya-Mwanjelwa,Mbalizi Road naUsongwe,Moshi-Nelson Mandela na Tanga-Madaraka

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg