YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Monday, 25 March 2013

HILI NDO DANGURO JIPYA LA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI DAR  Dar es Salaam. Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Majani ya Chai iliyopo Kipawa jijini Dar es Salaam, wametajwa kujiingiza katika kashfa ya ngono, kuvuta na kuuza bangi katika moja ya nyumba zinazozunguka shule hiyo, gazeti la mwananchi linaripoti
Hilo ni tukio lingine jipya, kwani mwishoni mwa mwaka jana, kuliibuka matukio ya ajabu kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi, Ruaruke, Rufiji mkoani Pwani ambao walielezwa kujihusisha na uvutaji bangi hata kukonyeza na kubaka walimu wao.

Mkuu wa Sekondari hiyo, Jasinta Assey(Pichani juu) alikiri na kusema kwamba vitendo vya uvutaji bangi na biashara ya ukahaba kwa wanafunzi wake, vinachangiwa na askari wa Kituo kidogo cha Stakishari ambao alidai wanachukua rushwa kwa wauzaji wa bangi na nyumba bubu za wageni. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Shule hiyo, Jasinta Assey alisema ni kawaida ya polisi hao kwenda kwenye nyumba hizo kunakofanyika biashara hizo na kuchukua rushwa badala ya kutatua tatizo.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg