YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday, 21 June 2016

MANENO YA ABDUL JUMA MCHEZA WA YANGA MARA BAADA YA KUPOTEZA MECHI.


" Wachezaji tumeumia sana kwa matokeo ya kufungwa dhidi ya MO Bejaia, goli tulilofungwa lilitokana na walinzi kukosa mawasiliano kuukabili mpira uliopigwa kuelekea lango letu ___ Timu yangu ilicheza vizuri sana sema tu tukashindwa kutumia nafasi za kufunga tulizokuwa tumezipata

"Siwezi sema tumefungwa kwa sababu mimi sikuwepo hapana, pengo langu kwa kiasi fulani lilionekana maana washambuliaji akina Ngoma na Tambwe walikosa zile krosi walizozoea ambazo huwa nawalisha, mchezo ujao ni dhidi ya TP Mazembe ambayo ni timu kubwa barani Afrika wao pia wanatambua Yanga ni timu kubwa kwa sasa hivyo utakuwa ni mchezo mgumu na lazima tupambane tupate matokeo na naamini tutafuzu hatua inayofuata

"Bado sijaanza mazoezi mepesi nataraji kuanza kesho au Alhamisi itategemea na ushauri wa daktari, hapa naelekea kuonana naye ili anipe maendeleo ya jeraha" Alimalizia Juma Abdul,mlinzi wa Yanga aliyeko majeruhi.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg