YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday, 21 June 2016

TETESI ZA USAJIRI BARANI ULAYA.


Mabingwa wa Ulaya Real Madrid wameanza mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Ufaransa, Paul Pogba, 23, kutoka Juventus, kwa mujibu wa wakala wake (Marca), mabingwa wa EPL Leicester wako tayari kulipa pauni milioni 30 kumsajili mshambuliaji wa Watford Troy Deeney, 27, baada ya dau lao kukataliwa mara mbili (Mirror), kocha msaidizi wa Manchester United Ryan Giggs ambaye anatarajiwa kuondoka Old Trafford, huenda akawania kazi ya kuifundisha Nottingham Forest (Mirror), hata hivyo taarifa nyingine zinasema Giggs hana mpango wa kwenda Forest ambayo wamiliki wake wanamtaka meneja wa zamani wa Olympiakos Michel (Nottingham Post), meneja mpya wa Chelsea Antonio Conte anapanga kumsajili winga wa Lazio Antonio Candreva, 29, pamoja na beki wa Juventus Leonardo Bonucci, 29 (Sun), meneja wa Pari St-Germain Laurent Blanc ataondoka wiki hii (Europe 1), Liverpool wanapanga kupanda dau kumtaka winga wa England na Newcastle Andros Townsend, 24 (Mirror), Manchester City pia wanamtaka Townsend ambaye ada yake ni takriban pauni milioni 10.5 (Telegraph), Everton wameanza mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji kutoka Cameroon, Vincent Aboubakar, 24, kwa pauni milioni 16 kutoka Porto (Daily Mail), West Brom wanataka kumsajili kiungo Moussa Sissoko, 26, kutoka Newcastle (Birmingham Mail), meneja wa zamani wa Manchester United Louis van Gaal, meneja wa zamani wa Ajax, Frank de Boer na Andre Villas-Boas wanawania kazi ya kuifundisha AC Milan (La Gazzetta dello Sport), mshambuliaji wa AC Milan Fernando Torres, 32, anatarajiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja Atletico Madrid (Marca), Crystal Palace, Aston Villa na Norwich wanataka kumsajili kiungo wa Reading Aaron Tshibola, 21 (GetReading), Swansea wako tayari kuwapa mikataba mipya Leon Britton na Angel Rangel (South Wales Evening Post), meneja wa Sheffield Wednesday Carlos Carvalhal hawanii nafasi ya umeneja Southampton (Sheffield Star), mshambuliaji wa Manchester City Kelechi Iheanacho, 19, huenda akakosa mwanzo wa msimu baada ya kuitwa na timu ya taifa ya Nigeria kushiriki michuano ya Olimpiki mjini Rio (Manchester Evening News). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg