YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Wednesday 25 July 2012

HII NDIO STORI KAMILI KUHUSU MWENYEKITI WA CCM MISUNGWI KUPIGWA CHINI.


Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza imetengua na kumvua nafasi Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Benard Pollycarp baada ya kukaidi maagizo na maelekezo yaliyotolewa na kamati hiyo kwa kamati ya siasa ya wilaya ya Misungwi hivi karibuni.
Katibu wa siasa na uenezi wa CCM Mwanza Simon Mangelepe amesema kutokana na maagizo iliyokua imeyatoa kwa kamati ya siasa ya wilaya ya Misungwi, ilimwita na kumuhoji Mwenyekiti huyo kisha kumtaka apime uzito wa tuhuma na kujiuzulu.
Pollcarp anatuhumiwa kwa kuhusishwa na ubadhilifu na wizi wa fedha za Halmashauri ya wilaya ya Misungwi kwenye taarifa ya mkaguzi mkuu wa hesabu CAG Ludovick Uttouh iliyozitaja halmashauri 33 nchini ambazo zimeripotiwa kutafuna fedha kinyume na taratibu.
Wakati uongozi wa CCM Mkoa ukichukua hiyo hatua tayari kuna stori za chinichini kwamba mwenyekiti huyo amekua akiendesha mipango ya chini kwa chini kuwahamasisha baadhi ya madiwani 26 wanaomuunga mkono waendelee kujiandaa kukihama chama hicho na kujiunga na chama kimoja cha siasa kwa madai kwamba taarifa ya CAG iligushiwa na kuchakachuliwa kwa lengo la kisiasa ikidaiwa kufanywa na kigogo mmoja wa ngazi ya kitaifa ambae anatoka kwenye wilaya ya Misungwi.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg