YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Thursday 18 April 2013

BREAKING NEWZ!!! MLIPUKO TENA WATOKEA MAREKANI TEXAS



Mamia ya watu wanahofiwa kufariki kutokana na mlipuko huo
Zaidi ya watu 100 wamejeruhiwa katika mulipuko uliotokea kwenye kiwanda cha mbolea kilichoko Kaskazini Magharibi mwa eneo la Waco, jimbo la Texas. Wengi wamekwama ndani ya majengo yanayendelea kuteketea kufuatia mulipuko huo.
Meya wa Mji kulitokea mulipuko huo, Tummy Muska ameelezea kutokea moto mkubwa uliolipuka sawa na bomu. Mulipuko huo umeharibu majengo ya kiwanda hicho, makaazi ya karibu kikiwemo kituo kimoja cha afya.
Wazima moto, magari ya kubebea wagonjwa na helikopta sita zimetolewa kushughulikia majeruhi na kutuliza hali ya sasa.
Majengo kadhaa yameendelea kuteketea karibu na kiwanda hicho cha mbolea.Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema zinasea kuna watu waliopoteza maisha.
Dean Wilson wa idara ya usalama ya Texas amesema nyumba 75 karibu na jengo hilo ziliharibiwa kabisa.
Amesema kufikia sasa hawezi kuthibitisha vifo vyovyote. Watu 38 wameripotiwa kua katika hali mahututi. Makundi ya wokozi yameanza kufika nyumba hadi nyingine kuwaokoa majeruhi na kutoa huduma ya kwanza.
Kituo cha Dharura kimewekwa kwenye uwanja wa mpira ulioko karibu.Gavana wa Texas amesema afisi yake imetoa raslimali zake kusaidia katika juhudi za wokozi.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg