YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Saturday, 29 June 2013

TIZAMA YALIYOJIRI NJE YA HOSPITALI YA MEDICLINIC HEART ALIKOLAZWA MZEE NELSON MANDELA

Mke wa Mzee Nelson Mandela, Winnie Madikizela–Mandela  akizungumza na vyombo vya habari baada ya kumtembelea Rais wa zamani wa Afrka ya kusini Mzee Nelson Mandela hapo jana ijumaa
Akiendelea kuzungumza na vyombo vya habari nje ya hospitali alikolazwa mzee Nelson Mandela
Baadhi ya watu waliofika hospitalini hapo wakimpa moyo mke wa Mzee Nelson Mandela 

Endelea kusoma zaidi kwa kubofya hapa chini


Hiki ni chombo maalumu (kinachotumia remote) chenye mwonekano kama wa helicopter ambacho kimefungwa kamera kikiwa kinazunguka kwenye maeneo ya hospitali ya Mediclinic Heart iliyoko kwenye mji wa Pretoria nchini Afrika ya Kusini.
 Mtotot akiwa kapumzika nje ya jengo la Uhuru akiwa  ameweka picha ya Nelson Mandela kwenye maua hujo Pretoria, Afrika ya kusini hapo jana ijumaa
 Mtoto mdogo akiwa ameshika  picha ya rais wa kwanza mwafrika nchini afrka ya kusini mzee Nelson Mandela
Baadhi ya wanachi wakiomba kwa ajiri ya afya ya mzee Nelson Mandela
Mtoto Lesibana Kekana mwenye miaka mitano(5) akionesha upendo wa nchi yake baada ya kuonekana usoni ana bendera ya Afrika Kusini kwenye maeneo ya Soweto
Kweli kufa kufahana, baadhi ya wafanya biashara wakiuza khanga zenye pica ya Rais wa zamani, mzee Nelson Mandela nje kidogo ya hospitali ya Mediclinic Heart alikolazwa mzee Mandela

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg