YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Wednesday 7 August 2013

MFANYABIASHARA MKUBWA WA MADINI JIJINI ARUSHA AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI NA WATU WASIOJULIKANA.



Pichani juu askari wakikagua mwili wa  Erasto Msuya, mmoja wa Wafanyabiasha wakubwa wa Madini jijini Arusha aliyejulikana ambaye pia ni mmiliki wa SG HOTEL mkoani humo, baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi na kufa papo hapo.

 Kwa mujibu wa baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa mfanya biashara huyo alifariki dunia mara baada ya majibishano ya risasi baina ya majambazi hayo na mfanya biashara huyo ambapo alizidiwa  nguvu na kupigwa risasi na kufariki dunia

Habari zinaeleza na kubainisha zaidi kuwa Marehemu alikuwa akitokea KIA kwenda BOMA ambako alikuwa ameitwa na watu (ambao hawakujulikana mara moja) ili wakafanye biashara. 

Habari zaidi tuvute subra kidoogo, tutazidi kufahamishana kadiri ya taarifa zitakapokuwa zikiingia. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-Amen.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg