YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Monday 7 October 2013

PICHA 6 ZA JENGO LA TTCL MAKAO MAKUU LILIPOKUWA LIKIWAKA MOTO LEO ASUBUHI



Jengo la TTCL, Makao makuu, EXTELECOMS limeungua moto kuanzia majira ya leo saa 12:00 asubuhi hadi saa 1:20.

Moto huo ulikuwa unawaka katika ghorofa ya sita ya jengo hilo na ulikuwa unawaka katika vyumba vitatu kwa mara moja.

Mwandishi wetu alifanikiwa kufika  katika jengo hilo na kujionea   mishe mishe za  wafanyakazi  wakiondoa magari yao na magari ya shirika hilo kongwe nchini.

Magari ya kikosi cha zimamamoto kutoka kikosi cha ukoaji cha Jiji la Dar es Salaam yaliwasili saa 12:20, lakini kulikuwa na ubishani kati ya wafanyakazi wa zima moto na wale wa TTCL, baada ya wafanyakazi wa Zimamoto kulaumu kuwa walienda pale siku kadhaa zilizopita kukagua jengo lakini walifukuzwa kama mbwa,

Licha ya Kikosi hicho kuwahi hawakuwa na maji yenye pressure na ngazi za nje kufika hadi ghorofani, hali iliyopelekea watu kutumia ngazi za ndani kuingia kwenye jengo hilo hali ambayo ni hatari kwa maisha yao.

Gari ya Ultimate Security walifika mnamo saa 12:30 na kwa ushirikiano moto uliweza kufanikiwa kuzimwa.




No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg