YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Thursday 6 March 2014

TUPILIA MBALI DIAMOND NA JAYDEE , HUYU NDIYE BILLIONEA WA KITANZANIA,,MFAHAMU HAPA


Diamond-Lady-jaydee


Hapa duniani kwasasa kuna mabilionea 1645 , kutokana na takwimu zilizotolewa na Forbes. Kwa mwaka jana bara la Afrika lilikua na mabilionea 20 lakini kwa mwaka huu wameongezeka mabilionea 9 na mmoja wapo ni mtanzania. Kwa upande wa sanaa ya hapa Bongo basi tunaweza kusema Diamond na Lady jaydee ndio wanaongoza kwa mkwanja labda ni kwasababu ya uwekezaji wao wanaofanya na kila kukisha kutuonesha mapesa na magari wanaomiliki lakini sio mbaya ukamjua tajiri namba moja Tanzania na namba mbili kwa Afrika mashariki akiachwa na Sudhir Ruparelia kutoka Uganda mwenye utajiri wa bilioni  1.1 za kimarekani .
Diamond-Lady-jaydee
Anaitwa Rostam Aziz, 53 ndio bilionea pekee Tanzania. Anamiliki asilimia 35 ya mtandao wa Vodacom, Mtandao mkubwa zaidi nchini wenye watumiaji zaidi ya millioni 10.Pia Rostam anamiliki mgodi wa Caspian Mining.pia anamilikia asilimia fulani kwenye bandari ya Dar-es-salaam. Na pia anafanya biashara za nyumba nchi za Tanzania, Dubai, Oman and Lebanon. Rostam ana utajiri wenye thamani ya bilioni 1 za kimarekani.
Rostam-Aziz-Forbes-vibe-co-tz
Ikumbukwe kwamba Akon ndio msanii tajiri kuliko wote Afrika na utajiri wake ni dola za kimarekani milioni 80 na kwa mwaka huu ameanza kampeni ya kuzipa mwanga nyumba zaidi ya milioni moja katika nchi za afrika magharibi na afrika ya kati.
Akon
Tujiulize ni lini wasanii wa kibongo watafika level kama alizofika Akon na sio kwa kipato bali kwa ile hali ya kurudisha shukrani kwa jamii na kuacha kuturingishia utajiri wao.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg