YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Friday 31 October 2014

UNAAMBIWA CHIDI BENZI ALIFANYIWA KITU MBAYA NA MAHABUSU WENZAKE,USTAA WAMPONZA




Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rashidi Makwiro ‘Chid Benz’ akiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Rashidi Makwiro ‘Chid Benz’ alijikuta akizodolewa na mahabusu wenzake mara baada ya kuingizwa katika Karandinga kupelekwa Segerea baada ya kukosa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.Tukio hilo lilitokea Oktoba 28, mwaka huu ambapo Chid Benz alikuwa akipelekwa Segerea huku mahabusu waliokuwemo ndani ya gari hilo wakitoa maneno ya kumkejeli pale alipokosa kiti na kulazimika kusimana.
Mmoja wa mahabusu alisikika akimzodoa Chid Benz kwa kumwambia: ‘Ustaa wako hukohuko, simama’ ambapo msanii huyo hakuleta ubishi, alisimama na safari ya kuelekea Segerea ikaanza.Chid Benz akiwa chini ya ulinzi mkali Mahakamani hapo.
Chid Benz anadaiwa kukamatwa na madawa ya kulevya  aina ya Heroine yenye thamani ya Tsh. 38,638, Bangi zenye thamani ya Tsh. 1,720 pamoja na vifaa vya utumiaji wa kuvuta dawa hizo ambapo alikana mashitaka hayo na kurudishwa rumande hadi Novemba 11, mwaka huu kesi yake itakapotajwa tena.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg