YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday, 13 November 2012

MIPASHO YA JK NA MAGUFULI KWA UPINZANI
0
Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais JAKAYA KIKWETE
Mkutano Mkuu wa Nane wa Chama cha Mapinduzi ambao leo unaingia siku yake ya tatu umeendelea kuibua mengi ikiwemo la Viongozi wa Vyama vya Upinzani kubainika kusifia maendeleo yaliyopatikana nchini kimya kimya kwa kuhofia Sera za vyama vyao zinazowataka kupinga kila jema linalofanywa na Serikali.
Hilo limebainishwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais JAKAYA KIKWETE wakati akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu juu ya kebehi zinazotolewa na wapinzani juu ya Serikali iliyopo madarakani katika kutekeleza majukumu yake.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na kupewa shukurani na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo.Kushoto ni Waziri wa Ujenzi,Mh. John Magufuli.
Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi DK JOHN POMBE MAGUFULI naye hakukaa kimya, ambapo ametumia fursa hiyo kumtaka Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema Taifa, FREEMAN MBOWE kuwaambia wanachama wake juu ya maendeleo yaliyoletwa na CCM kama alivyofanya wakati wa uzinduzi wa barabara ya kwa Sadala.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg