YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday, 13 November 2012

HABARI ZA CCM NA NEC KUHUSU UCHAGUZI MKUU.


MATOKEO YA NAFASI YA UMAKAMU MWENYEKITI BARA NA VISIWANI YATANGAZWA RASMI

Tuesday, November 13, 2012

Matokeo ya nafasi za makamu mwenyekiti Zanzibar na Tanzania Bara yatangwazwa rasmi,ambapo hakuna kura iliyoharibika hivyo wamepita kwa asilimia 100%.
Dr. Ali Mohamed Shein ,Rais wa Zanzibar amepita kwa idadi ya kura 2397 na hakukuwa na kura za hapana, hivyo kutangazwa rasmi kuwa ndio Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,wakati huo huo Philip Mangula amechaguliwa kwa kura 2397, hakuna zilizoharibika ,hivyo Mh. Mangula ndio Makamu Mwenyekiti mpya kwa upande wa Tanzania Bara.

RAIS KIKWETE ALIPOTEMBELEA BANDA LA GAZETI LA UHURU

Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamoja Abdulrahaman Kinana wakiangalia picha za zamani katika banda la Magazeti ya Uhuru na Mzalendo.

Rais Jakaya Kikwete akiwa ndani ya banda la Gazeti la Uhuru na Mzalendo na amefarijika sana kuona gazeti hilo kongwe la chama kuendelea kuwa moja ya magazeti bora nchini,kushoto ni Mhariri Mtendaji,Josiah Mfungo.


UCHAGUZI KUMPATA MWENYEKITI MPYA WA CCM TAIFA NA MAKAMU WAKE WAWILI WAFANYIKA


 Mgombea wa Uenyekiti wa CCM, Taifa, Rais Jakaya Kikwete akipiga kura kuchagua wakati wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, jioni hii, kwenye ukumbi wa Kizota, Dodoma. Kulia ni  Mgombea Umakamu Mwenyekiti (Bara) Philip Mangula na watatu kulia ni Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Sheni.
 Wajumbe wakipiga kura kuchagua Mwenyekiti wa CCM Taifa, jioni hii, kwenye ukumbi wa Kizota, Dodoma. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

KIZOTA NI KILA KITU

Banda la Gazeti la Uhuru lililopo Kizota ,Dodoma limekuwa kivutio kikubwa sana kwani Viongozi,wajumbe na wanachama wamekuwa wakimiminika kuona picha za zamani na historia ya magazeti kinngwe nchini Uhuru na Mzalendo.


Aden Rage,Mbunge wa Tabora mjini,ambaye pia ni mwenyekiti wa timu ya mpira ya Simba,akiwa kwenye meza ya waandishi wa Habari, Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Maelezo,Assa Mwambene na kushoto ni mwandishi Eva-Sweet  Musiba.


Msanii wa TOT akionyesha ujuzi wa kucheza.


Waandshi wa habari wakiwa kazini wakati mkutano Mkuu wa Nane wa CCM ukiendelea,Kizota Dodoma leo.


Biashara zimepamba moto, hii inadhihirisha CCM inavyotua fursa.

Biashara ya vyakula imepamba moto eneo la Kizota.Bank nazo hazikuwa nyuma kutoa huduma kwenye Mkutano Mkuu wa nane wa CCM.


Gari la bank ya CRDB likiwa kwenye eneo la mkutano mkuu wa nane wa CCM ,Kizota Dodoma.KIKWETE AJIUZULU UENYEKITI SAA 9;15 ALASIRI, KUPISHA UCHAGUZI WA MWENYEKITI MPYA WA CCM TAIFA

 Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete na Makamu wake wa Uenyekiti Dk. Amani Abeid Karume (Zanzibar) na Pius Msekwa (Bara) wakiondoka meza kuubaada ya kujiuzulu nafasi zao kufuatia kumaliza muda wao wa uongozi. Baadaye Kikwete ambaye ameteuliwa na CCM kugombea tena nafasi hiyo ya Uenyekiti alikaa upande wa wajumbe kushubiri kuchaguliwa tena. Tukio hili limefanyika saa 9:15 alasiri.
 Kikwete na meza kuu wakiwa upande wa wajumbe wa Mkutano Mkuu, wakati uchaguzi Mkuu kumpata Mwenyekiti mpya wa CCM Taifa ambapo yeye ni mgombea pekee.
Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Benjamin Mkapa akiongoza Mkutano Mkuu kwa muda baada ya Kikwete kujiuzulu. Sasa mchakato wa upigaji kura kuchagua Mwenyekiti na kuwapata Makamu Wenyeviti Bara na Zanzibar unaendelea muda huu. FUatilia hapa kupata matokeo (Picha zote na Bashir Nkoromo)

'LIVE' KUTOKA MKUTANO MKUU WA CCM, KIZOTA, DODOMA, LEO

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisalimia baadhi ya wana-CCM, wakati akiingia kwenye ukumbi wa Kizota, kuendesha Mkutano Mkuu wa CCM unaomalizika leo
 Msinisahau katika Ufalme wenu: Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisalimia baadhi ya wana-CCM, wakati akiingia kwenye ukumbi wa Kizota, kuendesha Mkutano Mkuu wa CCM unaomalizika leo. Kikwete anapigiwa kura leo ili kuweza kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM.
 Msanii Vicky Kamata  akiimba wimbo maalum kunogesha Mkutano Mkuu wa CCM katika ukumbi wa Kizota, Dodoma.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na meza kuu, wakishiriki kucheza wimbo maalum ulimbwa na Vicky Kamata kabla ya kuanza mkutano huo.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na meza kuu, wakishiriki kucheza wimbo maalum ulimbwa na Vicky Kamata kabla ya kuanza mkutano huo.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu, Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia), Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salim Ahmed Salim, wakifuatilia matukio kwenye mkutano huo, ukumbini.
 Wake wa viongozi ,Mjane wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Fatma Karume, Mama Kawawa, Shadya Karume, Mwanamwema Shein na Tunu Pinda wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wajumbe na waalikwa wakimiminika kuingia kwenye viwanja vya Kizota, Dodoma wakati wa mkutano mkuu leo
 BIASHARA: Wajumbe na waalikwa wakinunua bidhaa zinazouzwa na wajasiriamali nje ya ukumbi wa Kizota, Dodoma wakati wa mkutano huo.
 Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Janeth Mbene akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya  Magu, Jacqueline Lina nje ya ukumbi wa Kizota.
  Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Janeth Mbene akizungumza na Kamanda Asas wa UVCCM, mkoa wa Iringa, nje ya ukumbi wa Kizota.
 Kamanda Asas wa UVCCM mkoa wa Iringa akitazama nakala ya UHURU alipotembelea banda la kampuni ya Uhuru Publications Ltd, wanaochapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, kwenye viwanja vya Kizota.
 Banda maalum la Mamalishe ndani ya viwanja vya Kizota
 Mtangazaji wa TBC Swedy Mwinyi, akiwa 'live' wakati wa mkutano mkuu wa  CCM, kwenye ukumbi wa Kizota, Dodoma, Kulia ni Swedy Mwinyi na Salum Othman wa Shirika la Utangazaji Zanzibar. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg