YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Tuesday 19 March 2013

MLOKOLE AMPIGA SHOKA MAMA YAKE, AMUUA CHEKI PICHA HAPA



Na Dustan Shekidele, Morogoro
KWELI kuelekea mwisho wa dunia, mengi yataonekana. Mtu unawezaje kumpiga shoka mama yako mzazi, aliyekutunza tumboni mwake kwa miezi tisa, akakunyonyesha, kukusomesha hadi kukua na kujitegemea?
Mwili wa marehemu Ndolukasi Lugamo ukitolewa eneo la tukio.
Frank Hillary, 27, aliyetambuliwa kuwa mlokole, amethubutu na kuweza kukatisha maisha ya mama yake, Ndolukasi Lugamo, 50, akitumia shoka kuondoa uhai wa mzazi wake.
Frank Hillary akiwa chini ya ulinzi.
Tukio zima, lilichukua nafasi Alhamisi iliyopita, Mtaa wa Malipula, Kata ya Chamwino, mkoani hapa na inadaiwa kwamba kabla ya mauaji, Hillary alimpiga vibao, mitama na mateke mama yake.
Muuaji Frank Hillary (27), akiwa mikononi mwa wanausalama.
HALI HALISI ILIVYOKUWA
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Pili Athuman, alidai kwamba siku ya tukio, kulitokea mabishano kati ya Hillary na mama yake.
“Yalikuwa mabishano kidogo lakini ghafla yule kijana alimvamia mama yake na kuanza kumpiga,” alisema Pili na kuongeza:
“Yule kijana ni mtoto wa pekee wa yule mama. Tunashindwa kuelewa mpaka sasa chanzo cha tukio hilo. Halafu wale watu ni walokole kabisa na siku zote walikuwa wanaishi kwa upendo.”
Wananchi wakiangalia shoka lililotumika kuondoa uhai wa Ndolukasi Lugamo.
Shuhuda mwingine, Julius Josephat alisema: “Mimi nashindwa kuelewa. Huyu marehemu na mwanaye walikuwa wanapendana sana, wakienda kanisani wanaongozana kama kumbikumbi.
“Kinachosikitisha zaidi ni kuwa mama yake aliumia mkono kama siku tatu kabla, akawa amefungwa plasta ngumu (POP), nahisi ndiyo maana alishindwa kujiokoa.”
Mwili wa marehemu pamoja na shoka lililotumika vikitolewa eneo la tukio kupelekwa kwenye difenda.
Naye Maria Maswika ambaye nyumba yake imepakana na ile ya mama Hillary, alieleza: “Leo (Alhamisi),  saa 4 asubuhi nilimsikia huyo mama akipiga kelele za kuomba msada, huku akiingia nyumbani kwangu.
“Nilipotoka chumbani, nilishuhudia kwa macho yangu yule kijana akimpiga shoka mama yake na kumuua palepale. Sababu ya ugomvi wao siielewi. Kwanza nashangaa sana, kwani yule mama wa watu alikuwa anampenda sana mtoto wake.”
Muuaji Frank Hillary akipigwa pingu na wanausalama.
HILLARY AKAMATWA
Mwandishi wetu alifika eneo la tukio mapema na kushuhudia wananchi wakimkamata Hillary, kumfunga kamba kabla ya polisi nao kuwasili, kuandika maelezo na kumchukua mtuhumiwa huyo wa mauaji ya mama yake mzazi.
RPC ANASEMAJE KUHUSU SHERIA?
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, ACP Faustine Shilogile, alisema: “Uchunguzi zaidi wa tukio unaendelea na utakapokamilika, tutamfikisha mtuhumiwa mahakamani.”
Paka anayetajwa kumilikiwa na marehemu akiwa pembeni ya mwili wa Ndolukasi Lugamo.
PAKA WA KUSHANGAZA
Kitu kilichowashangaza wengi eneo la tukio ni paka anayetajwa kumilikiwa na marehemu ambaye baada ya mama huyo kuuawa, yeye alikwenda kulamba damu kisha akalala kichwani kwenye mwili wa marehemu.
Mtuhumiwa Frank akipandishwa kwenye difenda.
TUTAFUATILIA
Uwazi linaendelea kufuatilia na litaweka bayana sababu hasa ya mauaji hayo na kilichompata kijana huyo mpaka akachukua uamuzi wa kumuua mama yake.
Safari ya kuelekea kituoni imeiva.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg