YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Sunday 10 August 2014

BAADA YA GWAJIMA KUNUNUA HERIKOPTA, KAKOBE ASEMA HAYA..

Screen Shot 2014-08-11 at 6.23.39 AM
Gazeti la KIU Aug 1 2014
Kama sehemu ya vyanzo vyako vya habari ni mitandao kama vile website, blogs, facebook, twitter na Instagram inawezekana hii stori ya Gwajima ambae ni Muhubiri wa Injili kununua Helikopta uliiona hata zaidi ya mara moja.
Hata hivyo Muhubiri mwenzake Askofu Zacharia Kakobe Aug 10 2014 amenukuliwa na gazeti la Nyakati na kuizungumzia hiyo Helikopta akisema ‘kitendo cha Gwajima kununua helikopta kwa ajili ya kazi zake za Injili kinastahili kufurahiwa na Wakristo wote wa kweli, tujifunze kupongezana.. nampongeza sana’
‘Kumiliki kwake Helikopta kutachangia katika kufuta dhana potofu ambayo imedumu kwa muda mrefu ya kuyaita Makanisa ya kilokole…. makanisa ya vichochoroni, Helikopta sio starehe na hata muundo wake sio wa starehe bali ni kazi, itamwezesha pia kufika maeneo ambayo gari sio rahisi kumfikisha kutoa neno la Mungu’ – Kakobe
Screen Shot 2014-08-11 at 6.36.10 AMKuhusu Askofu Kakobe kununua Helikopta yake, amesema >>> ‘mimi sio mtu wa mashindano na pia kila mtu anakwenda sawa kutokana na ono aliloitiwa, haya sio mambo ya kushindana… hicho ndicho kinacholeta shida mara kwa mara, Gwajima ana Helikopta ni kwa manufaa ya Ufalme wa Mungu, mimi nina chakwangu ni kwa utukufu wa Mungu, hakuna haja ya kuigana’

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg