YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Wednesday 13 August 2014

WANAWAKE WAPINGA JESHI KUPELEKA WAUME ZAO VITANI.

Wanawake wayazuia magari ya jeshi yaliyokuwa yakiwapeleka waume zao kupigana na Boko Haram

posted 1 day ago by admin
Ripoti kutoka Nigeria zinaeleza kuwa Jumamosi iliyopita kundi kubwa la wanawake lilijitokeza na kuzuia magari ya jeshi yaliyokuwa yamewabeba wanaume wao na wake zao yakielekea katika mji wa Gwosa, sehemu ambayo inadhibitiwa na kundi la Boko Haram.
Kwa mujibu wa Prime Times ya Nigeria, wanawake hao walizua geti la barracks katika mji wa Borno huku wengine wakilala barabarani kushinikiza waume zao wapewe vifaa vya kisasa na imara zaidi ndipo waende vitani kupambana na kundi hilo.
Hali hiyo imekuja baada ya kuripotiwa kuwa karibu wanajeshi 60 waliuawa Jumatano iliyopita katika eneo la Gwosa linalomilikiwa na Boko Haram na kudaiwa kuwa sababu kubwa ni zana duni walizokuwa nazo kulinganisha na zana za kisasa za kijeshi za kundi hilo.
Chanzo kimeiambia Prime Times kuwa wanawake hao walieleza kuwa hawataki kubaki wajane na yatima kama wenzao kwa sababu ya vita hiyo.
“Mwanamke mmoja alisema ‘hatutaki kuwa kundi lingine la wajane, wapeni waume zetu zana bora zaidi za kivita, silaha na magari bora zaidi la sivyo hawaendi kokote’.”
Wanajeshi wengine pia walionekana kuunga mkono madai ya wanawake hao na kusukuma lawama kwa maafisa wa serikali.
We are ever ready to tackle Boko Haram terrorists but our superior officers are the ones killing us by not giving us the right arms to execute the war. How could I go and face Boko Haram with AK47 that is charged with only three cartridges when the enemy is brandishing modern GPMG, AA, RPG and so on.”Alikaririwa mwanajeshi mmoja.
Kundi la Boko Haram bado linawashikilia mateka wanafunzi wa kike zaidi ya 200 na wanawake wengine huku likitekeleza mauji ya kutisha katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg