YOUR MOST FAVORITE BLOG.

YOUR MOST FAVORITE  BLOG.
Calvin

Wednesday 10 September 2014

JIJI LIMEINGILIWA SASA,UNAAMBIWA HUYU NDIYE MWANAFUNZI WA KIKE WA DARASA LA TANO TISHIO KWA UTAPELI JIJINI DAR



Nyuma ya tukio la denti wa darasa la tano kwenye shule moja ya msingi iliyopo Mbezi-Shamba, Dar, aliyejitambulisha kwa jina moja la Irene (11) la kunaswa akifanya utapeli kwa kuwaibia raia, mazito yameibuka.

Denti wa darasa la tano anayetambulika kwa jina moja la Irene (11) aliyenaswa akiwatapeli raia.
Katika tukio hilo lililojiri hivi karibuni maeneo ya Posta Mpya, Dar, denti huyo alikuwa akisimama nyakati za asubuhi akivalia sare za shule huku akiombaomba kwa madai kuwa hana nauli ya kuvukia katika kivuko cha Kigamboni kwenda shule anayosoma.
Kwa mujibu wa mmoja wa mashuhuda, mtoto huyo alikuwa akisimama mbele  ya Kituo cha Daladala cha Posta mpya akijifanya ombaomba kwa madai kwamba hana  nauli.Ilisemekana kwamba siku nyingine mtoto huyo alikuwa akionekana akiuza simu kwa bei chee na alipohojiwa alikokuwa akizitoa alidai ameziokota.
Mwandishi wa Global na Global TV Online, Gabriel Ng'osha (kushoto) akipata undani wa habari katika tukio hilo.  
Dereva mmoja, Juma Hamis anayeegesha gari lake eneo hilo (Posta Mpya) alisema kuwa tabia ya mtoto huyo ilikuwa ni ya muda mrefu kwani alianzia Kariakoo, Dar akitapeli na kuiba madukani ambapo watu walimstukia hivyo akaamua kuhamia Posta.
“Mara kadhaa amenusurika kupigwa akidaiwa kuchomoa simu za watu kwenye mikoba ndani ya daladala.“Kukamatwa kwa Irene, watu wa maofisini na kwenye daladala wameshukuru kwani anafahamika na ni tishio kwa utapeli na ndiyo waliomchoma kwa polisi akadakwa baada ya kukutwa akijidai ni ombaomba,” alisema dereva huyo.
Ofisa wa Polisi kutoka 'Central Police' Posta akifafanua jambo kuhusiana na mkasa huo.
Jader Sapi, anayefanya kazi katika ofisi moja zilizo ndani ya jengo la IPS, alisema mtoto huyo aliwahi kuingia ofisini kwao na alipotoka, wafanyakazi wawili walilalamika kupotea kwa simu zao, kitu kilichowafanya wajue ni yeye.
Mama mmoja aliyeshuhudia Irene akichukuliwa na askari, alisema ameshawahi kumpa fedha mara kadhaa denti huyo, akiamini alivyomweleza kuwa hakuna na wazazi na hivyo hana nauli ya kumpeleka shuleni.
Akizungumza na gazeti hili akiwa mikononi mwa polisi kwenye Kituo Kikuu, Irene alisema ni mwanafunzi wa shule moja ya msingi (jina kapuni) iliyopo Mbezi-Shamba na siyo kama alivyokuwa akidanganya kuwa anasoma Kigamboni, Dar.
Wananchi wakishuhudia laivu tukio hilo lililotokea maeneo ya Posta mpya, Dar es Salaam.
Pia alikiri kwamba amekuwa akidanganya kuwa hana wazazi wakati ukweli ni kwamba wazazi wake wapo.“Ni shetani tu aliniingia nikawadanganya raia,’’ alisema Irene.
Baada ya kushuhudia tukio hilo, wanahabari wetu walimsaka mkuu wa shule anayosoma mtoto huyo, Yusuph Zenny ambaye alikiri kumfahamu Irene na kudai kuwa tayari taarifa kutoka Kituo Kikuu cha Polisi, Dar zilimfikia.
Alitobosa siri kuwa ameshapata malalamiko mara kadhaa kuhusiana na binti huyo na kwamba amekuwa akifanya uchunguzi ili kupata ukweli.
Hata hivyo, alisema anawasiliana na wazazi ili kulifuatilia sakata hilo hivyo kuwaomba wanahabari wetu wampe muda atatoa majibu au hatua itakayochukuliwa huku Irene akiwa bado mikononi mwa polisi kwenye dawati la jinsia.

No comments:

Post a Comment

gfjythfghgfhdfgergdfgbvdfgrfdgdfrgdrgdfrgrdegedrgdrfg